Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
Wanaoamani Mungu hutumia uumbaji kama hoja kuu ya kuamini Mungu yupo, siwalaumu because after all bila uumbaji tusingekuwepo kubishana hapa kama mungu yupo au la! Na uwepo wake usingekuwa na maana.
Hoja yao ipo hivi:
1. kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,
2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu
3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu
Kuna matatizo kwenye kila statement hapo,. Ngoja tuzichambue
1. Kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,
Hatuna ushahidi wa hili.
Kwanza tunaishi kwenye sayari ndogo inayozunguka nyota moja kati ya nyota billioni 100 zinazounda galaxy. Ulimwengu unaoonekana tu una galaxy billion 100-200. Kwahyo hapo idadi ya nyota ni kama billioni 100 mara billioni 100 kwa idadi ya chini, na bado kuna ulimwengu ule ambao hatuuoni ambao unaweza kuwa mkubwa kuliko huu tunaouona kwa vifaa vyetu.
Kwahyo hatuwezi kuhitimisha kitu hakiwezekani kwenye huu ulimwengu kwa kutumia reference ya sheria tunazoziona kwenye haka kapocket kadogo ka ulimwengu tunakoishi. Inawezekana huko nyota ya mbali kuna viumbe wameweza kutengeneza something from nothing.
Sisi hatuwezi kuhitimisha chochote itakuwa ni sawa na mgeni kutoka Kigoma afikie kwa shemeji yake Chanika, aitalii nyumba ya shemeji kuanzia sebuleni,uani mpaka chooni halafu aseme ameshaijua Dar nzima na hakuna nyumba ya muundo tofauti na hiyo ya shemeji yake. Hakuna TV kama ya shemeji yake na hakuna gari kama la shemeji yake Dar nzima.
Pili, hata kwenye hiki kipoketi cha ulimwengu tunachoishi hatuna uhakika kuwa tunajua sheria zote za ulimwengu.
Ukimwambia mzee aliyekufa miaka 50 iliyopita kuwa Kuna teknolojia ya kuongea na mtu ana kwa ana sekunde hiyohiyo huku mkisikiana kama mko pamoja(Videocall) Atabisha kuwa hiko kitu hakiwezekani kama tunavyobisha kuwa something hakiwezi kutoka from nothing.
Hivyo hatuna ushahidi wowote wa kuhitimisha kuwa haiwezekani kitu kitokee bila chanzo.

Hata kama tukikubali kuwa Ulimwengu una chanzo,bado haithibitishi kuwa hiko chanzo lazima kiwe nje ya ulimwengu au kiwe na uwezo zaidi ya ulimwengu…Maji kwenye glass hayana madhara lakini yakiungana kutengeneza bahari yanaweza kuzamisha meli na kuleta Tsunami.
Pia hiko Chanzo kinaweza kuwa ulimwengu wenyewe,
Hizo sifa unazompa Mungu inawezekana ni sifa za ulimwengu.Yani ikiwa ulimwengu umejitengeneza,upo kila sehemu na unaweza kila kitu.
Maana Mtu ukibisha kwa kusema ulimwengu lazima uwe na chanzo kwasababu kila kitu kina chanzo basi ntakuambia na mungu pia yupo kwenye hiyo “kila kitu kinahitaji chanzo” na ukibadilisha kuwa kila kitu kinahitaji chanzo kasoro Mungu tu basi ntakuuliza nini kinampa Mungu hiyo kasoro?? Kwanini isiwe kila kitu kinahitaji chanzo kasoro ulimwengu wenyewe? Au chanzo kingine kisicho huyo ‘Mungu’?

Na hata kama tukikubali ulimwengu umeumbwa bado haitoshi kujua kuwa huyo aliyeumba ni Mungu na wengine huenda mbali hadi kumpa sifa zingine kama i)aliwahi kuwa binadamu akaja kufa duniani, au wengine husema huyo ii)Mungu haelewi lugha tofauti na kiarabu
Haya yote mmejuaje? Je kama hiko chanzo ni kitu kingine ambacho hakipo tena ulimwenguni,yani kiliumba halafu kikaondoka kikauacha ulimwengu ujiendeshe kwa sheria kilizouwekea? Una uthibitisho gani kuwa hiko chanzo cha ulimwengu ndio hiki unachoita Mungu na si kingine??
Kwasababu kusema ulimwengu uliumbwa haitoshi kuwa kama ushahidi wa kuwa aliyeuumba ni Mungu.
Au una ushahidi kuwa lazima kiwe Mungu na especially huyo Mungu wako na sio Mungu wa Zumaridi? Au kitu tofauti na Mungu?? Vipa kama Mungu aliumba Ulimwengu halafu akaondoka akaendelea na mishe zake akawcha ujiendeshe na tukifa ndio imetoka hiyo?? Kwanini iwe ni Mungu wako tu?? Una uthibitisho?
Nachosema Mimi ni kuwa Mungu anaweza kuwepo, ila hatuna ushahidi wa hilo. Na hatuna sababu za kuamini hilo kama unao naomba
Maana ukisema ushahidi ni kitabu chako cha dini kilikuambia hivyo basi hiko hiko kitabu naomba ukiulize haya maswali unipe majibu