Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Think out of the box. Ukienda Korea Kaskazini, Mungu wao ni Kim Il Sung na uzazi wake. Ukienda India kwa Wahindu kuna Miungu lukuki kila mmoja ana nafasi yake katika maisha. Na wote wanaishi vizuri kwenye imani zao. Point hapa usijikite tu kwenye imani za Ukristo/Uislamu. Hii dunia imani zipo nyingi sana na tofauti na maisha yanasonga kwa maelfu ya miaka. Funguka akilini.
Andiko langu halijajikita katika hizo imani mbili tu,linaapply kwa imani zote…hizo mbili nmezitumia kama mfano tu
 
Imagine!! What if nilichokiona ilikuwa ni sehemu ya project ya blue beam?.
Ukiwa hutaki/uwezi onyesha wapi nimesema ni Mungu basi chochote unachokiandika ni invalid.
Hukuona sehemu nilposema ' sitaki kuiongelea isije sema ninaihubiri? " kwanini umei- out singled sentensi ya Mungu na kuacha zingine?.
Bure kabisa.
Basi tufanye post yako lengo kuu ni kuongelea project blue beam.

Haya project blue beam inahusiana nini na huu uzi?
 
Andiko langu halijajikita katika hizo imani mbili tu,linaapply kwa imani zote…hizo mbili nmezitumia kama mfano tu
Wewe akili yako imejikita kwenye dini zinazoamini Mungu ni mmoja kwa maana ya Ukristo/Uislamu. Ni wazi hujui unachozungumza sababu kama ungetilia maanani kuwa kuna jamii zenye imani tofauti zaidi ya Ukristo na Uislamu dunia hii, hiyo mantiki uliyotumia ingekuwa batili.
 
Nimejikita katika arguments zinawekwa na watu wa zile imani zinazoamini ulimwengu uliumbwa na Mungu.

,.Kama kuna imani haiamini hivyo sawa, na sijui wao watakuwa wanasema ulimwengu uliumbwaje na sijui zaidi, ila haikuwa main target yangu kwenye hii topic.
 
Basi tufanye post yako lengo kuu ni kuongelea project blue beam.

Haya project blue beam inahusiana nini na huu uzi?
Haingoleai chochote ila nimeiandika kama changamoto tu. ni sawa na vitu vingine vingi nilivyoviongolea.
Kama una akili timamu ungejikita pale nilivyosema" dunia iko fully mysterious, ni zaidi ya waielezeavyo Atheist ama believers, lakini sasa wewe ni kichwa kitupu, umechagua engo unayohisi ni rahisi kwako na kuanza kuandika unacho hisi sahihi.

Basi sawa nmekuelewa
 
Nimejikita katika arguments zinawekwa na watu wa zile imani zinazoamini ulimwengu uliumbwa na Mungu.

,.Kama kuna imani haiamini hivyo sawa, na sijui wao watakuwa wanasema ulimwengu uliumbwaje na sijui zaidi, ila haikuwa main

Utakuwa unaumiza kichwa chako bure kila siku na maswali yasiyo na majibu ngoja nikurahisishie: Logic haina nafasi kwenye mambo ya imani au systems of belief. Hao Wahindi na Wachina mabilioni unataka kusema hawana akili wanapoamini hizo imani zao zisizoendana na Ukristo na Uislamu? Dhana ya Atheism inatokana na Ukristo na Uislamu na imani ya kuwa Mungu ni mmoja.
 
Atheism hawaamini katika existing God kwa hiyo acha uwongo.
 
Utakuwa unaumiza kichwa chako bure kila siku na maswali yasiyo na majibu ngoja nikurahisishie: Logic haina nafasi kwenye mambo ya imani au systems of belief. Hao Wahindi na Wachina mabilioni unataka kusema hawana akili wanapoamini hizo imani zao zisizoendana na Ukristo na Uislamu? Dhana ya Atheism inatokana na Ukristo na Uislamu na imani ya kuwa Mungu ni mmoja.
Kama watu wanaamini katika Mungu, awe mmoja au wawe wengi , awe Yesu au ng’ombe..ni sawa tu kwa imani zao lakini wasitulazimishe na sisi kuamini kuwa huyo Mungu yupo na aliumba huu ulimwengu.
Hoja yangu ipo kwa imani zote zinazoamini kuhusu uwepo wa creator god
 
Wanaoamani Mungu hutumia uumbaji kama hoja kuu ya kuamini Mungu yupo, siwalaumu because after all bila uumbaji tusingekuwepo kubishana hapa kama mungu yupo au la! Na uwepo wake usingekuwa na maana.

Hoja yao ipo hivi:

1. kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Kuna matatizo kwenye kila statement hapo,. Ngoja tuzichambue

1. Kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

Hatuna ushahidi wa hili.

Kwanza tunaishi kwenye sayari ndogo inayozunguka nyota moja kati ya nyota billioni 100 zinazounda galaxy. Ulimwengu unaoonekana tu una galaxy billion 100-200. Kwahyo hapo idadi ya nyota ni kama billioni 100 mara billioni 100 kwa idadi ya chini, na bado kuna ulimwengu ule ambao hatuuoni ambao unaweza kuwa mkubwa kuliko huu tunaouona kwa vifaa vyetu.

Kwahyo hatuwezi kuhitimisha kitu hakiwezekani kwenye huu ulimwengu kwa kutumia reference ya sheria tunazoziona kwenye haka kapocket kadogo ka ulimwengu tunakoishi. Inawezekana huko nyota ya mbali kuna viumbe wameweza kutengeneza something from nothing.

Sisi hatuwezi kuhitimisha chochote itakuwa ni sawa na mgeni kutoka Kigoma afikie kwa shemeji yake Chanika, aitalii nyumba ya shemeji kuanzia sebuleni,uani mpaka chooni halafu aseme ameshaijua Dar nzima na hakuna nyumba ya muundo tofauti na hiyo ya shemeji yake. Hakuna TV kama ya shemeji yake na hakuna gari kama la shemeji yake Dar nzima.

Pili, hata kwenye hiki kipoketi cha ulimwengu tunachoishi hatuna uhakika kuwa tunajua sheria zote za ulimwengu.

Ukimwambia mzee aliyekufa miaka 50 iliyopita kuwa Kuna teknolojia ya kuongea na mtu ana kwa ana sekunde hiyohiyo huku mkisikiana kama mko pamoja(Videocall) Atabisha kuwa hiko kitu hakiwezekani kama tunavyobisha kuwa something hakiwezi kutoka from nothing.

Hivyo hatuna ushahidi wowote wa kuhitimisha kuwa haiwezekani kitu kitokee bila chanzo.

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

Hata kama tukikubali kuwa Ulimwengu una chanzo,bado haithibitishi kuwa hiko chanzo lazima kiwe nje ya ulimwengu au kiwe na uwezo zaidi ya ulimwengu…Maji kwenye glass hayana madhara lakini yakiungana kutengeneza bahari yanaweza kuzamisha meli na kuleta Tsunami.

Pia hiko Chanzo kinaweza kuwa ulimwengu wenyewe,
Hizo sifa unazompa Mungu inawezekana ni sifa za ulimwengu.Yani ikiwa ulimwengu umejitengeneza,upo kila sehemu na unaweza kila kitu.
Maana Mtu ukibisha kwa kusema ulimwengu lazima uwe na chanzo kwasababu kila kitu kina chanzo basi ntakuambia na mungu pia yupo kwenye hiyo “kila kitu kinahitaji chanzo” na ukibadilisha kuwa kila kitu kinahitaji chanzo kasoro Mungu tu basi ntakuuliza nini kinampa Mungu hiyo kasoro?? Kwanini isiwe kila kitu kinahitaji chanzo kasoro ulimwengu wenyewe? Au chanzo kingine kisicho huyo ‘Mungu’?

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Na hata kama tukikubali ulimwengu umeumbwa bado haitoshi kujua kuwa huyo aliyeumba ni Mungu na wengine huenda mbali hadi kumpa sifa zingine kama i)aliwahi kuwa binadamu akaja kufa duniani, au wengine husema huyo ii)Mungu haelewi lugha tofauti na kiarabu

Haya yote mmejuaje? Je kama hiko chanzo ni kitu kingine ambacho hakipo tena ulimwenguni,yani kiliumba halafu kikaondoka kikauacha ulimwengu ujiendeshe kwa sheria kilizouwekea? Una uthibitisho gani kuwa hiko chanzo cha ulimwengu ndio hiki unachoita Mungu na si kingine??

Kwasababu kusema ulimwengu uliumbwa haitoshi kuwa kama ushahidi wa kuwa aliyeuumba ni Mungu.

Au una ushahidi kuwa lazima kiwe Mungu na especially huyo Mungu wako na sio Mungu wa Zumaridi? Au kitu tofauti na Mungu?? Vipa kama Mungu aliumba Ulimwengu halafu akaondoka akaendelea na mishe zake akawcha ujiendeshe na tukifa ndio imetoka hiyo?? Kwanini iwe ni Mungu wako tu?? Una uthibitisho?

Nachosema Mimi ni kuwa Mungu yupo, ila hatuna ushahidi wa hilo.kama unao naomba

Maana ukisema ushahidi ni kitabu chako cha dini kilikuambia hivyo basi hiko hiko kitabu naomba ukiulize haya maswali unipe majibu
Kwani unaathirika nini ukiamini uwepo wa Mungu?

Akili ya mwanadamu bado inaendelea kuyajua mambo mengi ambayo hayajadhihiri kwa sasa kwahiyo kuna mambo mengi huwezi kuyapatia majibu kwa sasa, kama ulivyosema hapo juu kwamba miaka 50 iliyopita hapakua na videocall, he miaka 1000 ijayo kutakuwaje??
 
Back
Top Bottom