Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Kama unaona ulikuwa sahihi na sio phenomenon kwasababu tu mlikuwa sita

Ebu jaribu kufikiria nyie 6 kati ya mamilioni wanaouona mwezi ila hawakuliona hilo tukio?

Bila kusahau na ma satellite yaliko huko angani ambayo muda wote yanaaangalia nini kinafanyika kwenye mwezi.

Unatushawishi tuamini kuwa hivyo vifaa vyote pamoja na uwezo wake havikuweza kuona isipokuwa watu 6 wa familia moja?
Hivi, kinachofanya 1+1 iwe 2 ni kwasababu wengi wanakubali kuwa ni mbili ama ni kwasababu ni 2 hata ikiwa wengi watakataa kuwa si 2?.
 
Sasa huo si ujinga. Mbona hapa hakuna logic. Yaani unamwambia Mungu akuambie ujikate paja? Ili iweje sasa? Hayo mabangi yenu nayo sometimes ni shida.
Sio mabangi bana huwezi kusema unaongea na Mungu wakati unajibzana na akili yako...hivi hivi ndo story zinnatungwa vitabu vinaandikwa na wajinga mnaamini.
Sasa huo si ujinga. Mbona hapa hakuna logic. Yaani unamwambia Mungu akuambie ujikate paja? Ili iweje sasa? Hayo mabangi yenu nayo sometimes ni shida.
Wanakuambia Mungu kanitokea Mimi na sio wewe na akikutokea wewe anakuambia unachotaka. Mungu ni mmoja lakini anamwambia kila mtu vitu tofauti na anachagua wa kutokea. Hebu acheni bana sisi sio watoto
 
Ni fact

Wewe hapa huongelei facts, ndio maana kwenye maelezo yako umesema ni muujiza.
Definitely ni fact, najua!! So, why tukio langu/ letu liamliwe na idadi ya watu ikiwa ni kweli ama ni uwongo?.

Nb:-hukujisumbua kuuliza nimesema ni muuajiza katika frame hipi.
Kuna mchezaji wa ajentina alisema "kushinda kombe la dunia ilikuwa ni muuajiza".
Je, hiyo kauli ina lina-nullify fact Kuwa Ajentina ilishinda kwa wachezaji kupiga penalties.
So, popote unapoona neno miujiza limetumika si lazima iwe kama insu ya Mussa kupasua bahari kwa fimbo.
 
Kama ni fact inatakiwa iwe universal kila mmoja ajue, wataalamu wa anga watujuze.

Njoo na sababu kwanini tuwapuuze mamilioni ya watu pamoja na teknolojia ya anga halafu tukuamini wewe na wenzako watano?
 
wewe ni SCAR, NON JF USERS hawakujui je, hiyo ni fact Kuwa existence yako mystery?.
Dhana ya kuwa kila fact ni lazima kila mtu aijue umeitoa wapi? Na kwanini iwe hivyo na si kinyume chake?
 
Wanaoamani Mungu hutumia uumbaji kama hoja kuu ya kuamini Mungu yupo, siwalaumu because after all bila uumbaji tusingekuwepo kubishana hapa kama mungu yupo au la! Na uwepo wake usingekuwa na maana.

Hoja yao ipo hivi:

1. kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Kuna matatizo kwenye kila statement hapo,. Ngoja tuzichambue

1. Kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

Hatuna ushahidi wa hili.

Kwanza tunaishi kwenye sayari ndogo inayozunguka nyota moja kati ya nyota billioni 100 zinazounda galaxy. Ulimwengu unaoonekana tu una galaxy billion 100-200. Kwahyo hapo idadi ya nyota ni kama billioni 100 mara billioni 100 kwa idadi ya chini, na bado kuna ulimwengu ule ambao hatuuoni ambao unaweza kuwa mkubwa kuliko huu tunaouona kwa vifaa vyetu.

Kwahyo hatuwezi kuhitimisha kitu hakiwezekani kwenye huu ulimwengu kwa kutumia reference ya sheria tunazoziona kwenye haka kapocket kadogo ka ulimwengu tunakoishi. Inawezekana huko nyota ya mbali kuna viumbe wameweza kutengeneza something from nothing.

Sisi hatuwezi kuhitimisha chochote itakuwa ni sawa na mgeni kutoka Kigoma afikie kwa shemeji yake Chanika, aitalii nyumba ya shemeji kuanzia sebuleni,uani mpaka chooni halafu aseme ameshaijua Dar nzima na hakuna nyumba ya muundo tofauti na hiyo ya shemeji yake. Hakuna TV kama ya shemeji yake na hakuna gari kama la shemeji yake Dar nzima.

Pili, hata kwenye hiki kipoketi cha ulimwengu tunachoishi hatuna uhakika kuwa tunajua sheria zote za ulimwengu.

Ukimwambia mzee aliyekufa miaka 50 iliyopita kuwa Kuna teknolojia ya kuongea na mtu ana kwa ana sekunde hiyohiyo huku mkisikiana kama mko pamoja(Videocall) Atabisha kuwa hiko kitu hakiwezekani kama tunavyobisha kuwa something hakiwezi kutoka from nothing.

Hivyo hatuna ushahidi wowote wa kuhitimisha kuwa haiwezekani kitu kitokee bila chanzo.

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

Hata kama tukikubali kuwa Ulimwengu una chanzo,bado haithibitishi kuwa hiko chanzo lazima kiwe nje ya ulimwengu au kiwe na uwezo zaidi ya ulimwengu…Maji kwenye glass hayana madhara lakini yakiungana kutengeneza bahari yanaweza kuzamisha meli na kuleta Tsunami.

Pia hiko Chanzo kinaweza kuwa ulimwengu wenyewe,
Hizo sifa unazompa Mungu inawezekana ni sifa za ulimwengu.Yani ikiwa ulimwengu umejitengeneza,upo kila sehemu na unaweza kila kitu.
Maana Mtu ukibisha kwa kusema ulimwengu lazima uwe na chanzo kwasababu kila kitu kina chanzo basi ntakuambia na mungu pia yupo kwenye hiyo “kila kitu kinahitaji chanzo” na ukibadilisha kuwa kila kitu kinahitaji chanzo kasoro Mungu tu basi ntakuuliza nini kinampa Mungu hiyo kasoro?? Kwanini isiwe kila kitu kinahitaji chanzo kasoro ulimwengu wenyewe? Au chanzo kingine kisicho huyo ‘Mungu’?

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Na hata kama tukikubali ulimwengu umeumbwa bado haitoshi kujua kuwa huyo aliyeumba ni Mungu na wengine huenda mbali hadi kumpa sifa zingine kama i)aliwahi kuwa binadamu akaja kufa duniani, au wengine husema huyo ii)Mungu haelewi lugha tofauti na kiarabu

Haya yote mmejuaje? Je kama hiko chanzo ni kitu kingine ambacho hakipo tena ulimwenguni,yani kiliumba halafu kikaondoka kikauacha ulimwengu ujiendeshe kwa sheria kilizouwekea? Una uthibitisho gani kuwa hiko chanzo cha ulimwengu ndio hiki unachoita Mungu na si kingine??

Kwasababu kusema ulimwengu uliumbwa haitoshi kuwa kama ushahidi wa kuwa aliyeuumba ni Mungu.

Au una ushahidi kuwa lazima kiwe Mungu na especially huyo Mungu wako na sio Mungu wa Zumaridi? Au kitu tofauti na Mungu?? Vipa kama Mungu aliumba Ulimwengu halafu akaondoka akaendelea na mishe zake akawcha ujiendeshe na tukifa ndio imetoka hiyo?? Kwanini iwe ni Mungu wako tu?? Una uthibitisho?

Nachosema Mimi ni kuwa Mungu anaweza kuwepo, ila hatuna ushahidi wa hilo. Na hatuna sababu za kuamini hilo kama unao naomba

Maana ukisema ushahidi ni kitabu chako cha dini kilikuambia hivyo basi hiko hiko kitabu naomba ukiulize haya maswali unipe majibu
Na kama kile kitabu cha waarabu kilitokea Kwa mungu Kwa hyo tuseme mungu alikua anatengeneza makalatasi huko juu
 
wewe ni SCAR, NON JF USERS hawakujui je, hiyo ni fact Kuwa existence yako mystery?.
Dhana ya kuwa kila fact ni lazima kila mtu aijue umeitoa wapi? Na kwanini iwe hivyo na si kinyume chake?
Kwanza unatakiwa ujue nje na ndani ya JF mi sio SCAR

Pili unatafuta equivalent ya stori mbili ambazo hazifanani.

Fact ni uhalisia unaopimika na kuthibitishwa eidha kwa vipimo au logic.

Katika vigezo hivyo hakuna namna yeyote unayoweza kuelezea tukio la watu sita kushuhudia watu wakitembea kwenye mwezi.

Wakati vipo vipimo ambavyo muda wote viko stand by ku observe kila tukio linalofanyika mwezini.

Pili mjengengo wa stori yako umekaa mythical yani namna ulivyouelezea mwezi ni tofauti kabisa na sifa zake ambazo zinajulikana.

Nadhani ndio sababu ukaamua kusema miraculous ulijua lack of better explanations wouldn't make you story to be taken seriously.
 
Hata mimi sijasema nje ya Jf Unaitwa Scar .
Tufanye nje ya Jf unaitwe Mwakaleli ama Scar ilo ilo, ila bado hiyo haiondoi swali langu nililo kuuliza.
Turudi kwenye swali langu:- kwanini TUKIO langu liamliwe na idadi ya watu na si kitu kingine?.
Kwamba, leo fact inapimwa kwa wingi wa watu?.

Nb:- kumbuka hadi sasa wewe ndiye umeamua kulichagulia UPANDE WA KU-SIDE (MYTHICAL)SIMULIZI LANGU na si mimi MSIMULIAJI.
So, andika chochote unachokijua ila tambua kuwa sasa wewe ndiye author wa nilichokisimua.
Maana mimi nilisema hii dunia iko beyond na masimulizi ya believers na atheists ila umeamua kuli-side andishi langu katika upande wa mythical na sababu ya kufanya hivyo unaijua wewe.
Labda uniambie ni kwanini hukuliegeza katika upande wa atheism na badala yake ukachagua upande wa pili wake?.
 
nakuelewa sana mkuu sema basi tu sijui why jamaa anakuwa mgumu hivyo
 
Sijasema fact inaamuliwa kwa wingi wa watu.

Hujaona hapo nimekutajia hadi vigezo vya kupima fact?

Hujaona nimetaja observation ya vipimo na logic?

Hujajua point ya mimi kusema mamilioni ya watu imetokana na wewe kukomalia kuwa stori yako ni ya kweli kwasababu haukuwa peke yako mlikuwa 6?

Mimi nimeiita mythical kwasababu ni stori ya kufikirika isiyofungamana na sifa za mwezi ambazo tunazijua.

Hata kama hujasema stori yako sio mythical ila ukiisimulia sifa ambazo hazipo kwenye kitu ambacho kinafahamika (zina contradict sifa halisi), sisi tutasema tu ni mythical au imaginary stories hata kama wewe hukutaja hayo maneno
 
nakuelewa sana mkuu sema basi tu sijui why jamaa anakuwa mgumu hivyo
Katika wale 6 aliosema na we ni mmoja wao?

Kwenye ulimwengu wa watu bilion 7 na ushenzi ni watu 6 tu ambao mna taarifa za tukio la kustaajabisha kama hilo kuhusu mwezi?
 
Katika wale 6 aliosema na we ni mmoja wao?

Kwenye ulimwengu wa watu bilion 7 na ushenzi ni watu 6 tu ambao mna taarifa za tukio la kustaajabisha kama hilo kuhusu mwezi?
hapana wala hata simjui sema nimefatilia mwanzo hadi mwisho wa majadiliano yenu.

Kwa jinsi nilivyomuelewa jamaa anajaribu kujenga hoja apart from atheist n believers faiths kuna nguvu za kimiujiza that work miraculuous zilizomo ndani na nahisi nje ya ulimwengu wetu.

Hiyo ndio hoja ya let the caged bird sings anayojaribu kueleza hapa kwa jinsi nilivyomuelewa
 
Nguvu za kimiujiza ni wrong interpretation ya vitu.

Kitu ambacho hujui mechanism yake imekuwaje mpaka iwe hivyo, ndio hapo utajikuta umekiita muujiza.

Ngoja nikupe short story

Kipindi ambacho niko shuleni nilibahatika kuishi hostel na room ambayo nilikua nalala nilikua nashea kitanda na mtoto wa mchungaji

Siku moja usiku tukiwa tumelala likapita tetemeko, lilitikisa kwa muda mrefu kidogo, wanafunzi wengi tulitoka nje kuhofia kubomokewa na nyumba.

Lakini kwa bahati mbaya rafiki yetu mlokole hakupata bahati ya kutoka. Kesho yake asubuhi akawa anatusimulia kua usiku alitembelewa na wachawi ambao walikua wanatikisa kitanda huku na huku kila kona ya kitanda.

Jamaa akaenda mbali kabisa kusema kua roho mtakatifu alimuingia na akajikuta amesimama na kuanza kufanya maombi yaliyochukua muda kidogo mpaka pale wachawi walipoishiwa nguvu na kukimbia.

Tukamuambia kua hawakua wachawi ilikua ni tetemeko, akabisha ikibidi aende kumuuliza mlokole mwenzie naye akasema ni kweli ilikua ni tetemeko.
 
Back
Top Bottom