Tumuite Mungu, japo nikiulizwa kwanini awe ni Mungu na si kitu kingine tu nisichokijua, nitakuwa sina jibu.
Hii dunia ni full mysterious, actually hakuna anajua chanzo cha ulimwengu na uhai but kuna Imani ina make logic sense ukisikiliza, sihitaji kuelezea isije semwa ninaihubiri.
Kuna nguvu inaendesha hii dunia na haijali hisia zetu,it acts accordingly na haitafuti waumini wa kuiamini.
Sikumbuki mwaka, coz ni kitambo niliwai ona watu wakitembea kwenye mbalamwezi wakati nimetoka nje kukojoa.
Nilihisi ni wenge BCBG, Nikarudi ndani kumuambia Mama kuwa kuna kitu cha ajabu nje, watu wanatembea kwenye mwezi.. Ilimchukua sekunde kadhaa kuhisi kuwa uenda kuna kitu si cha kawaida nimekiona nje ndiyo maana ninamuamsha ili akakione. akaamuka na Dada zangu wakaamka kwenda kushuhudia nilichokuwa nina kisema!!.
Ni yale majira ya mwezi Unatokeza fully, umbo lote unaliona.. Ni kama vile sinema watu wanatembea kwenye mwezi.
Niliowaita kuona ilo tukio waliogopa sana!! dada yangu ninaemfuta mara 3 akasema " twende kwa mzee wa kanisa, uenda leo ni siku ya mwisho".
Baada ya hapo ile sinema ikakata mwezi ukarudi katika hali yake.
Hadi leo wengine wamezeeka, nikijalibu kuwa kumbushia hiyo ilo tukio kila mmoja ana maoni yake.
Hivi juzi nimekuja kujua kuhusu mradi wa blue beam, uenda tulichokishuhudia ni blue beam ama ni tukio la miujiza tu kama miujiza mingine.. But definitely nimewai ona watu wakitembea kwenye mwezi. mwezi huu huu UnAujua, nimeona bila vifaa vya kitaalamu.
Ulimwengu ni zaidi ya unavyoelezwa na atheists ama believers.