Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Atheism sio kuamini Hakuna Mungu, ila ni kutoamini kuwa kuna Mungu

Kwani unaathirika nini ukiamini uwepo wa Mungu?

Akili ya mwanadamu bado inaendelea kuyajua mambo mengi ambayo hayajadhihiri kwa sasa kwahiyo kuna mambo mengi huwezi kuyapatia majibu kwa sasa, kama ulivyosema hapo juu kwamba miaka 50 iliyopita hapakua na videocall, he miaka 1000 ijayo kutakuwaje??
Siathiriki chochote nikiamini na hata nisipoamini siathiriki chochote maana hii concept haina uthibitisho na wala haina impact yoyote kwenye huu ulimwengu
 
Kwani unataka nini? Mbona sielewi,Basi tupigane
Hiii!! Haki ya Mungu tena, katika kupigana ngumi, hunipigi.
Siandiki kwasababu nipo nyuma ya keypads bali ndiyo uhalisia.
Ndiyo, Nimewai chezea kichapo Bar hadi leo kipo kwenye kumbukumbu zangu , ila wapigaji wenyewe hadi leo wanakili wazi kuwa waliniotea. and in that moment I was hospitalized from that beating wapigaji waliwai kwenda kufanya reconciliation kwa familia yangu mapema ili Iyongo(zali) liishe.
Sasa, japo we ni onymous sikujui unabi ufanye kitu cha ziada kunikalisha.
 
Kwani unaathirika nini ukiamini uwepo wa Mungu?

Akili ya mwanadamu bado inaendelea kuyajua mambo mengi ambayo hayajadhihiri kwa sasa kwahiyo kuna mambo mengi huwezi kuyapatia majibu kwa sasa, kama ulivyosema hapo juu kwamba miaka 50 iliyopita hapakua na videocall, he miaka 1000 ijayo kutakuwaje??
We unafaidika Nini usiamini yupo. Why ni lazma kuamini yupo?
 
Hiii!! Haki ya Mungu tena, katika kupigana ngumi, hunipigi.
Siandiki kwasababu nipo nyuma ya keypads bali ndiyo uhalisia.
Ndiyo, Nimewai chezea kichapo Bar hadi leo kipo kwenye kumbukumbu zangu , ila wapigaji wenyewe hadi leo wanakili wazi kuwa waliniotea. and in that moment I was hospitalized from that beating wapigaji waliwai kwenda kufanya reconciliation kwa familia yangu mapema ili Iyongo(zali) liishe.
Sasa, japo we ni onymous sikujui unabi ufanye kitu cha ziada kunikalisha.
A true warrior fights with his sword, he does not fight with his tongue
-Samurai Jack
 
Tumuite Mungu, japo nikiulizwa kwanini awe ni Mungu na si kitu kingine tu nisichokijua, nitakuwa sina jibu.
Hii dunia ni full mysterious, actually hakuna anajua chanzo cha ulimwengu na uhai but kuna Imani ina make logic sense ukisikiliza, sihitaji kuelezea isije semwa ninaihubiri.

Kuna nguvu inaendesha hii dunia na haijali hisia zetu,it acts accordingly na haitafuti waumini wa kuiamini.

Sikumbuki mwaka, coz ni kitambo niliwai ona watu wakitembea kwenye mbalamwezi wakati nimetoka nje kukojoa.
Nilihisi ni wenge BCBG, Nikarudi ndani kumuambia Mama kuwa kuna kitu cha ajabu nje, watu wanatembea kwenye mwezi.. Ilimchukua sekunde kadhaa kuhisi kuwa uenda kuna kitu si cha kawaida nimekiona nje ndiyo maana ninamuamsha ili akakione. akaamuka na Dada zangu wakaamka kwenda kushuhudia nilichokuwa nina kisema!!.
Ni yale majira ya mwezi Unatokeza fully, umbo lote unaliona.. Ni kama vile sinema watu wanatembea kwenye mwezi.
Niliowaita kuona ilo tukio waliogopa sana!! dada yangu ninaemfuta mara 3 akasema " twende kwa mzee wa kanisa, uenda leo ni siku ya mwisho".
Baada ya hapo ile sinema ikakata mwezi ukarudi katika hali yake.
Hadi leo wengine wamezeeka, nikijalibu kuwa kumbushia hiyo ilo tukio kila mmoja ana maoni yake.
Hivi juzi nimekuja kujua kuhusu mradi wa blue beam, uenda tulichokishuhudia ni blue beam ama ni tukio la miujiza tu kama miujiza mingine.. But definitely nimewai ona watu wakitembea kwenye mwezi. mwezi huu huu UnAujua, nimeona bila vifaa vya kitaalamu.
Ulimwengu ni zaidi ya unavyoelezwa na atheists ama believers.
Najaribu kufikiria hapa

Mwezi unao onwa na mamilioni ya watu, lakini ni familia moja tu ya watu kadhaa ndio iliyoweza kushuhudia hilo tukio

Au phenomenon ya movements za mawingu ndio iliyowachanganya?

Maana kuna stori nyingi sana zinazohusishwa na mwezi.

Home tulikuwa tukiangalia mwezi tulikuwa tunasema tunaona bikira maria amempakata Yesu.

Je hutoi nafasi ya wrong interpretation kwenye tukio lako we na familia yako?
 
Mimi na Mungu iko hivi..
Huwa mimi na yeye Tunazungumza.
Namuuliza swali ananijibu, animbiaga hapendi nini na anapenda nini na kuna vitu kanipa na kuna vitu kaniahidi atamipa.

Sifa yake kubwa yeye ndie kaniumba. na Kaumbo dunia yote na ulimwengu.
Waumini wa Mwamposa muwe mnaangalia na mazingira sio kila sehemu ni kawe
 
We unafaidika Nini usiamini yupo. Why ni lazma kuamini yupo?
Taarifa za kwamba kuna Mungu, nimezipata kutoka kwenye dini ambayo pia imeweka utaratibu wa namna ya kuishi na hiyo ndio ninayofaidika nayo.

Ni bora uamini uwepo wa Mungu kwa kuzingatia kwamba bado akili yako haijatumika kwa uwezo wake wote kupinga uwepo wa Mungu,

Ninaposema akili yako ninamaanisha kama mwanadamu, kwa mfano miaka 1000 iliyopita mwanadamu na malighafi zote za kutengeneza gari zilikuwepo lakini alitumia wanyama kusafiri.
 
Kwa hiyo mbona hupigi mawe watu wanaofanya mapenzi alafu hawajaona. Je ni namna sahihi ya watu kuishi? Dini ni utapeli Kama utapeli mwingine tu
 
Huyo Mungu wako unayemsema na akili yako ndo maana hawezi kukuambia kitu ambacho hutaki. Kama unabisha mwambie akuambie ujikate paja..
Sasa huo si ujinga. Mbona hapa hakuna logic. Yaani unamwambia Mungu akuambie ujikate paja? Ili iweje sasa? Hayo mabangi yenu nayo sometimes ni shida.
 
Najaribu kufikiria hapa

Mwezi unao onwa na mamilioni ya watu, lakini ni familia moja tu ya watu kadhaa ndio iliyoweza kushuhudia hilo tukio

Au phenomenon ya movements za mawingu ndio iliyowachanganya?

Maana kuna stori nyingi sana zinazohusishwa na mwezi.

Home tulikuwa tukiangalia mwezi tulikuwa tunasema tunaona bikira maria amempakata Yesu.

Je hutoi nafasi ya wrong interpretation kwenye tukio lako we na familia yako?
Sijui niweke vipi maneno yangu. Itoshe kusema tukio nilioliona/tulioliona ni miraculous.. Mwezi ulikuwa umejizoom kiasi kwamba kama ni movie Basi utaju huyu sharukan ama yule ni Amrish pool.
Ikiwa ni phenomenon ya movement ya wawingu tu ingelikuwa ni jambo gumu zaidi ya watu sita kuwa fooled na hali hiyo.
Kila mtu alikuwa katika hofu ila sikuwai sikia majirani zetu ama mtu mwingine nje family yetu akiongelea tukio ilo.
 
Wanaoamani Mungu hutumia uumbaji kama hoja kuu ya kuamini Mungu yupo, siwalaumu because after all bila uumbaji tusingekuwepo kubishana hapa kama mungu yupo au la! Na uwepo wake usingekuwa na maana.

Hoja yao ipo hivi:

1. kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Kuna matatizo kwenye kila statement hapo,. Ngoja tuzichambue

1. Kila kitu kilichopo kina chanzo hakiwezi kutokea from nothing,

Hatuna ushahidi wa hili.

Kwanza tunaishi kwenye sayari ndogo inayozunguka nyota moja kati ya nyota billioni 100 zinazounda galaxy. Ulimwengu unaoonekana tu una galaxy billion 100-200. Kwahyo hapo idadi ya nyota ni kama billioni 100 mara billioni 100 kwa idadi ya chini, na bado kuna ulimwengu ule ambao hatuuoni ambao unaweza kuwa mkubwa kuliko huu tunaouona kwa vifaa vyetu.

Kwahyo hatuwezi kuhitimisha kitu hakiwezekani kwenye huu ulimwengu kwa kutumia reference ya sheria tunazoziona kwenye haka kapocket kadogo ka ulimwengu tunakoishi. Inawezekana huko nyota ya mbali kuna viumbe wameweza kutengeneza something from nothing.

Sisi hatuwezi kuhitimisha chochote itakuwa ni sawa na mgeni kutoka Kigoma afikie kwa shemeji yake Chanika, aitalii nyumba ya shemeji kuanzia sebuleni,uani mpaka chooni halafu aseme ameshaijua Dar nzima na hakuna nyumba ya muundo tofauti na hiyo ya shemeji yake. Hakuna TV kama ya shemeji yake na hakuna gari kama la shemeji yake Dar nzima.

Pili, hata kwenye hiki kipoketi cha ulimwengu tunachoishi hatuna uhakika kuwa tunajua sheria zote za ulimwengu.

Ukimwambia mzee aliyekufa miaka 50 iliyopita kuwa Kuna teknolojia ya kuongea na mtu ana kwa ana sekunde hiyohiyo huku mkisikiana kama mko pamoja(Videocall) Atabisha kuwa hiko kitu hakiwezekani kama tunavyobisha kuwa something hakiwezi kutoka from nothing.

Hivyo hatuna ushahidi wowote wa kuhitimisha kuwa haiwezekani kitu kitokee bila chanzo.

2. Hivyo Ulimwengu una chanzo, hiko chanzo lazima kitakuwa nje ya ulimwengu na kitakuwa na uwezo zaidi ya ulimwengu

Hata kama tukikubali kuwa Ulimwengu una chanzo,bado haithibitishi kuwa hiko chanzo lazima kiwe nje ya ulimwengu au kiwe na uwezo zaidi ya ulimwengu…Maji kwenye glass hayana madhara lakini yakiungana kutengeneza bahari yanaweza kuzamisha meli na kuleta Tsunami.

Pia hiko Chanzo kinaweza kuwa ulimwengu wenyewe,
Hizo sifa unazompa Mungu inawezekana ni sifa za ulimwengu.Yani ikiwa ulimwengu umejitengeneza,upo kila sehemu na unaweza kila kitu.
Maana Mtu ukibisha kwa kusema ulimwengu lazima uwe na chanzo kwasababu kila kitu kina chanzo basi ntakuambia na mungu pia yupo kwenye hiyo “kila kitu kinahitaji chanzo” na ukibadilisha kuwa kila kitu kinahitaji chanzo kasoro Mungu tu basi ntakuuliza nini kinampa Mungu hiyo kasoro?? Kwanini isiwe kila kitu kinahitaji chanzo kasoro ulimwengu wenyewe? Au chanzo kingine kisicho huyo ‘Mungu’?

3. Kwahyo ulimwengu umeumbwa na huyo aliyeuumba tunamwita Mungu

Na hata kama tukikubali ulimwengu umeumbwa bado haitoshi kujua kuwa huyo aliyeumba ni Mungu na wengine huenda mbali hadi kumpa sifa zingine kama i)aliwahi kuwa binadamu akaja kufa duniani, au wengine husema huyo ii)Mungu haelewi lugha tofauti na kiarabu

Haya yote mmejuaje? Je kama hiko chanzo ni kitu kingine ambacho hakipo tena ulimwenguni,yani kiliumba halafu kikaondoka kikauacha ulimwengu ujiendeshe kwa sheria kilizouwekea? Una uthibitisho gani kuwa hiko chanzo cha ulimwengu ndio hiki unachoita Mungu na si kingine??

Kwasababu kusema ulimwengu uliumbwa haitoshi kuwa kama ushahidi wa kuwa aliyeuumba ni Mungu.

Au una ushahidi kuwa lazima kiwe Mungu na especially huyo Mungu wako na sio Mungu wa Zumaridi? Au kitu tofauti na Mungu?? Vipa kama Mungu aliumba Ulimwengu halafu akaondoka akaendelea na mishe zake akawcha ujiendeshe na tukifa ndio imetoka hiyo?? Kwanini iwe ni Mungu wako tu?? Una uthibitisho?

Nachosema Mimi ni kuwa Mungu anaweza kuwepo, ila hatuna ushahidi wa hilo. Na hatuna sababu za kuamini hilo kama unao naomba

Maana ukisema ushahidi ni kitabu chako cha dini kilikuambia hivyo basi hiko hiko kitabu naomba ukiulize haya maswali unipe majibu
Kiranga
 
Sijui niweke vipi maneno yangu. Itoshe kusema tukio nilioliona/tulioliona ni miraculous.. Mwezi ulikuwa umejizoom kiasi kwamba kama ni movie Basi utaju huyu sharukan ama yule ni Amrish pool.
Ikiwa ni phenomenon ya movement ya wawingu tu ingelikuwa ni jambo gumu zaidi ya watu sita kuwa fooled na hali hiyo.
Kila mtu alikuwa katika hofu ila sikuwai sikia majirani zetu ama mtu mwingine nje family yetu akiongelea tukio ilo.
Kama unaona ulikuwa sahihi na sio phenomenon kwasababu tu mlikuwa sita

Ebu jaribu kufikiria nyie 6 kati ya mamilioni wanaouona mwezi ila hawakuliona hilo tukio?

Bila kusahau na ma satellite yaliko huko angani ambayo muda wote yanaaangalia nini kinafanyika kwenye mwezi.

Unatushawishi tuamini kuwa hivyo vifaa vyote pamoja na uwezo wake havikuweza kuona isipokuwa watu 6 wa familia moja?
 
Back
Top Bottom