NINGEPENDA WATU WAJUE HILI.
God is rather TRUTH than REALITY. Kuna tofauti kubwa sana kati ya hiyo misamiati, na maelezo/uthibitisho wake unatolewa na FACTS na LOGICS.
Twende Pamoja...
REALITY inatangulia; je ni kitu gani?
Reality ni uhalisia unaothibitishwa na macho.
Sijui hii definition umetunga au umetoa wapi ila kwenye dictionary ya Mirriam Webster anasema Reality are the things in life that are
commonly observed and
verified to
exist, things that are
consistent and
not random or
influenced by
conformity or
mass hysteria. Something that is
perceived as
real and is physically experienced by the
senses.
Kwahyo uhalisia (reality) unathibitishwa sio na macho tu, bali na sense zote 21+ za mwili ikiwemo
Touch,smell,taste,proprioception, magnetoception,Equilibrioception(balqnce gravity),Thermoception, Noicoception(Pain),Thirst,Hunger,Time perception, introspection,Body awareness,pressure,kinestgetics etc.
Reality doesn't need explanations at all since its empirical and everybody can talk about it. Therefore, the talk about reality is called FACT.
Actually reality needs to be explained thats why we have science and scientific theories.
Kila mtu anajua ukirusha apple juu litaanguka chini ila explanations ya nini kinasababisha hayo tunahitaji Einstein's theory ya relativity inayoelezea jinsi Gravity inavyochipukia baada ya matter kubend space.
Kila mtu anajua kuna radi ila tunahitaji science ituelezee radi inatokeaje?
FACTS- ni maelezo kuhusu reality. Aidha ufafanuzi ama maelezo tuu. Mfano; wewe ndiye unatumia simu yako, unaiona kwa rangi, jina, pamoja na ukubwa. Hiyo ni reality, huhitaji maelezo kujua ulichoshika ni kitu gani, na kama ukianza kutoa maelezo hayo yanaitwa FACTS.
Umenipata sio?
Nimekupata sasa, kumbe fact ni maelezo tu. Inamaanisha tukienda ndani zaidi kumbe Fact ni branch tu kwenye maelezo. Inamaana maelezo yapo ya aina nyingi.
Kuna maelezo ya uongo ambayo hayaendani na uhalisia tunayaita Uongo/Lies / False facts.
na kuna maelezo yenye ukweli(Truth) unaoendana na uhalisia. Ndio tunayaita facts. Tupo pamoja.
TRUTH- Truth ni Kipande cha REALITY ambacho hakionekani kwa macho. Truth is likely to be told, but reality has to be seen.
Again reality sio lazima ionekane kwa macho. Tunajua upepo upo ni reality ingawa hatuuoni kwa macho.
kwahyo hapa kuna false dilema. Unaact kama vile option zilizopo ni mbili tu kuona au kuambiwa wakati kuna kunusa,kuhisi,kusikia nk.
Mtu akikuambia kuwa jana alikula ugali, huwezi kusema huo sio uhalisia eti kwasababu wewe hukumuona.
Hapa tunatakiwa tujue hivi kuna Maelezo, kuna Ukweli, na Kuna uhalisia.
Kwa definiton yako mwenyewe Fact ni Maelezo ya kweli ambayo yanaelezea uhalisia (bila kujali kama wewe unayeelezwa umeona au hujaona)
Kwahyo kama maelezo ya jamaa aliyesema kala ugali jana yanaweza kuwa fact au uongo lakini inategemea kama ni ya kweli au uongo.
Kama ni kweli alikula basi yanakuwa facts na kama anadanganya basi yanakuwa uongo.
Hii yote haijalishi kama anayeambiwa alikuwepo/aliona au la.
Wanadamu wanafahamu nguvu ya macho yao, lakini hawawezi ku 'deny' hadhi, kazi na nguvu ya viungo vingine kama Masikio katika kujenga na Kulinda Ufahamu. Hapa ndipo inapatikana TRUTH. Hatuwezi kusema jambo, ama kitu fulani hakipo ati kwa sababu hatujawahi kukuiona. NO!
Kumbe unajua hilo, sasa kwanini maelezo yako ya juu yalikuwa yameegemea tu kwenye kuona?
Mfano; most people know the TRUE you, not the REAL you. Hatusemi kwamba, the real you doesn't exist ati kwa sababu hatujawahi kukuona. Mfano, wewe ni Mzinzi, na ndiye wewe unafahamu,'real you' sio kwa sababu hatujakuona basi wewe sio mzinzi, NO! logics zitathibitisha, kwa sababu tabia ni ngozi. Ngozi huonekana na haibadiliki.
The true you is the real you. Kama watu wanajua wewe sio mzinzi kumbe wewe ni mzizi basi watu wanajua the False you, lakini the true you ni ile real you ambayo ni mzinzi.
Ukweli haujalishi kama watu wanaujua au hawaujui. Ukweli ni ukweli tu.
Na ukasahau ulivyosema juu mwanzo kuwa God ni truth sio reality..... Kwa mfano wako huohuo wa watu kujua true you ambayo ni uongo kuwa wewe sio mzinzi kumbe kiuhalisia wewe ni mzinzi.
Basi watu wanaweza kujua Mungu yupo truth kumbe in reality Mungu hayupo.
Sasa, maelezo kuhusu TRUTH yanaitwa Logics.
hizi definition unazitoa wapi? Logic ni kitu kingine kabisa, ni utaratibu kwenye reasoning. Unahusisha statement zaidi ya 1.
Kitu kinaweza kuwa false lakini logical.
Mfano:
Sijawahi kuona kunguru asiye mweusi
Nimeona kunguru wote duniani
Hivyo hakuna kunguru asiye Mweusi duniani.
sasa hizo statement kwa sheria za logic ni kweli ziko logical
Lakini zinaweza kuwa sio true kwasababu mimi sijaona kunguru wote duniani.
Hatuwezi kusema God is not real, ati kwa sababu hukuwahi kumuona. No!! Don't be Clunk.
Kwanini hatuwezi?
Sayansi imezungumza mambo mengi ambayo hatuwezi kuyaona, mathalani Hormones, nerve pulses, n.k.
Haya yote yameonekana kwa msaada wa vifaa kwenye Microscope wewe uko nchi gani?
Microscope inakuza tu upeo wa macho yetu
kuonA vitu vidogo.
Labda nikuulize, UNAAMINI KUNA UMEME? Umewahi kuuona? Usiniambie umeme ni huo Mwanga wa taa ya hapo chumbani kwako, huo mwanga. Upo hata kwenye nyota.
Yani ni sawa na mtu kuuliza unaamini kuna Maumivu? Usiniambie kuona mtu analia baada ya kupigwa ngumi ni ushahidi wa maumivu kwasababu hata Wale waigizaji wa azam Tv wanaigiza kwa kulia na kupigana kumbe hawaumii.
Mi nilishapigwa shoti mkuu, sihitaji kuona mwanga wa taa kuamini kuna umeme.
Watu wanaotaka ushahidi kuhusu Mungu (Muumba) wataka kufahamu kuhusu nini kitaridhisha macho yao, na usipowapa hawaamini, wakati huo wanadai HAWAAMINI.
Mkuu mbona unakomaa na macho tu?? Wapi nimelimit macho tu?
wewe thibitisha kivyovyote vile hata ukiamua kutuonesha kwa Macho huyo Mungu ni sawa pia. ila hata ukitupa uthibitisho tofauti ni sawa pia.
Hivi unaelewa maana ya kuamini na kutoamini? Unasema huamini halafu unataka evidences. Maana yake wewe ni Muumini wa EVIDENCE.
kuamini ni ile kuwa uhakika kichwani mwako kuwa jambo flani ni la kweli.
Unawezs ukaamini jambo kuwa ni kweli kumbe sio la kweli.
sasa mimi napenda kuamini jambo la kweli na kutoamini uongo.
ili nijue jambo kama ni kweli au la inabidi NITHIBITISHE kama linaendana na Uhalisia au la.
Kwahyo Mimi ninaamini vitu ambavyo nitajiridhisha kwa vithibitisho kuwa ni vya kweli wakati wewe unaamini kitu chochote.
Mark Manson kwenye kitabu chake cha Everything is Fucked anasema, 'Hakuna asiye amini' Yes, ni kweli. Atheists ni waumini wazuri wa Sayansi, hivyo WANAAMINI katika Evidence. Nigger! Believing is human tenet. Very natural from the deep self.
Mimi sijasema Atheist hawaamini chochote. Imani sio jambo baya na ni la lazima. Shida ni je unachoamini ni cha kweli?
Je huo ukweli umeuthibitisha pasi na shaka?
Je umethibitisha kuwa Mungu yupo?
na sio Atheists wote wanaamini katika sayansi.. Kuna watu wanaamini tupo kwenye simulation ndani ya computer ya aliens. Hao hawaamini Mungu na pia hawaamini Bigbang wala evolution.
Shida ya hao watu (Kama ilivyo kwa waamini Mungu) ni je, wana uthibitisho wa hiyo imani?
Atleast Sayansi ni field inayojikita kuutafuta ukweli kwa kutumia Evidence na repeatable experiments.
Science is the best tool that humans have fore seeking the truth.
Narudia tena WATU. Don't be fooled. Mungu yupo na anatupenda. Usiwe mtumwa wa uhuru wako. Keep the focus.
Sasa unasema Yupo kwa uthibitisho upo? Namimi nasema Vampires wapo msitoke usiku. Keep the focus.
Hiyo Atheism ni Tamanio la Kutowapo Mwenyezi Mungu ili binadamu alishe bila kikwazo matamanio ya nafsi yake.
Atheism sio tamanio.
Mimi ni atheist ninayetamani Mungu awepo ila ndio hivyo
Ni kama yatima anayetamani Siku moja Aje mzee kujitambulisha mimi ni baba yako, lakini ndo hivyo tena anabaki kuwa yatima tu.