Mkuu mi kama atheist nashukuru kwa busara yako kwa namna ulivyoamua kutuita
Ila ulichosahau ni kitu kimoja
Watu wanasifia magari, Pc nk kutokana na comparison walizofanya za kuangalia ufanisi wa bidhaa moja dhidi ya bidhaa nyingine.
Hao atheist wanaosifia magari, computer nk, wanafanya hivyo kwa references.
Kwamba watu wanasema hii bidhaa ni bora kwasababu kuna specs hii ambayo kwenye bidhaa hii nyingine haipo
Viwanda vinavyotengeneza hizo bidhaa vinathibitishika kuwa vipo bila kuhitaji kitu kingine cha ziada kama ishara ya kuonesha ndio source ya hizo bidhaa
Huyo mtu hawezi kushindwa kukuthibitishia kampuni la Dell au Hp kuwa lipo.
Ni maswala ya taaluma ambayo kila mtu anaweza akafanya endapo akifundishwa.
Sasa
Unaposema huu ulimwengu umesababishwa na Mungu, references yako inakuwa nini?
Tunaweza tukathibitisha hicho chanzo bila kutumia kitu kingine kinachopimika kuwa ndio uthibitisho wa Mungu asiyepimika?
Lakini pia
Unaposema huu ulimwengu ni bora au umekamilika unakuwa umeupima na kuufananisha na ulimwengu gani mwingine mpaka ukafikia hitimisho kuwa ulimwengu huu ni mzuri?
Aliyesema laptop Hp omen ya gaming ni bora aliangalia toleo la chini yake au alifananiaha na brand nyingine kwenye maswala ya kiuwezo akaona Hp Omen ni laptop bora
Sasa ulimwengu huu mnaosema ni mzuri au ni bora, ni bora ukiufananisha na ulimwengu upi?