Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Sayansi ni nature, elimu ya kiutafiti inayochunguza vitu vilivyotuzungukaUtafiti wa kisayansi ni kutafuta ushaidi wa jambo fulani, na kuna wakati inakosa majibu. Kushindwa kupata jibu la kisayansi, hakuhalalishi kuwa hakuna jibu, bali ni kufikia ukomo wa uwezo wake.
Madai ya uwepo wa Mungu ni supernatural claims zinaohusiana na habari za kiroho
Ni kweli Sayansi haiwezi kuthibitisha aina hiyo ya madai kwa jinsi yalivyokaa, lakini kama utakumbuka sayansi pia haiwezi kuthibitisha habari za Spiderman, Harrypoter, Batman, Super heroes, Unicorn nk.
So point yako ni nini?
Kwamba kwakua sayansi haiwezi kuthibitisha madai ya hivyo vitu basi busara ni kusema haiwezi na sio kwamba hakipo?
No haiwezi ikawa hivyo
Tukisema tuachane na sayansi kwasababu haijui kitu kwenye mambo ya kiroho ambayo ndio sehemu iliyomuongelea Mungu, so turejee kwenye maandiko matakatifu
Ila kabla hatujarejea, kumbuka tuna maelfu ya vitabu vinavyodaiwa kuwa ni vitabu vya Mungu (maandiko matakatifu)
Ni maandiko gani matakatifu yaliyo matakatifu zaidi kuliko mengine?
Au ni toleo gani la maandiko ambalo tunapaswa kulitumia kama reference?
Kama hoja ya "ufunuo" inafikiriwa kuwa ni hoja ya kukubalika basi kuna haja ya kueleza kwanini andiko moja lipingane na andiko lingine wakati yote hudaiwa kuandikwa kwa ufunuo?