Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Huyu muumba aliyemuumba mtoto mchanga wa siku sita kisha akambamiza na ukuta na kumuua katika tetemeko la Turkey au Syria ni muumba wa aina gani? Hicho kichanga kilitenda dhambi gani? Kwanini alimuumba kisha akamuua?
Anayeunda compyuta nzuri kisha akachukua nondo na kuibomoa bila shaka utamuita punguwani. Anayefanya hivyo kwa kichanga je?
Yule rabii wa Israel aliyesema mtetemeko wa Turkey na Syria ni adhabu ya mungu alikuwa maana gani? Hata masheikh na wachungaji wetu wanasema hivyo. Yaani kichanga kimeadhibiwa ! DU!
 
Mimi ndio nilikuuliza hilo swali

Sijui kama hata unaelewa nachokiandika

Mimi niliuliza hilo swali nikilinganisha na mfano wako wa nyumba ambao nimeukubali.

Hoja yangu kuu ya kuukubali mfano wako wa nyumba kuwa imejengwa ulitokana na backup ya kimazingira niliyoshuhudia nyumba zikijengwa.

Sasa kwenye ishu ya ulimwengu unao uthibitisho wowote unaoonesha records za limwengu zikumbwa ili tufikirie kuwa huu ulimwengu wetu utakuwa umeumbwa?
Mimi nimekuuliza kukuonyesha ya kuwa sharti lako la kuwa na backup ni dhaifu, ndiyo maana swali Hilo umeshindwa kulijibu mpaka muda huu.
 
Hahitaji ushauri wako wala wangu kuamua mambo yake, hahitaji ridhaa ya yoyote kupanga mambo yake, hahitaji kumridhisha yoyote yule hata wewe😂
Nami siko hapa kutoa ushauri kwa Mungu, nafanya reasoning kulingana na nyinyi jinsi mnavyomueoezea Mungu kwa sifa zake za ukuu.

Nahoji dhana ya uwepo wa Mungu kulingana na sifa mlizompa.

Ni sawa na mzazi ambaye umesimuliwa kuwa ni mzazi bora sana kwa watoto wake. Anawapenda sana watoto wake na hayupo tayari kuona watoto zake wanapata matatizo.

Halafu siku ukamkuta huyo mzazi anawafungia watoto wake wenye umri chini ya miaka 7 kwenye chumba chenye wanyama wakali wakutisha kama mamba, na mijoka yenye sumu kali.

Ukaja ukamuuliza yule mtu aliyekuambia habari za huyo mzazi kivipi huyo mzazi afanye huo ukatiri, ye akujibu kuwa anafanya hivyo kulingana na yeye anavyoona na sio wewe unavyotaka.

Unafikiri utetezi huo unaweza kukubaliwa na mtu gani ambaye rational kuwa huyo mzazi anaupendo wote kwa watoto zake?
 
Safi, kwahiyo unakubali uwepo wake? Maana tayari unahoji sifa zake tayari upo halfway kukiri uwepo wake
Kuhoji sifa ya kitu wala haikuhitaji ukubaliane na uwepo wa hicho kitu

Hata humu nimeshuhudia wakristo wakihoji habari ya farasi mwenye mbawa aliyetumika kumsafirisha Muhammad kwenda mbingu ya saba

Kuhoji kwao hakukuwa na maana kuwa wanakubaliana na uwepo wa farasi yule au tukio hilo kuwa ni la kweli.

Kama ambavyo uliweza kuhoji habari za pazi aliyebebwa na jogoo kichwa chini miguu juuu, hakikufanya ukubali kuwa jambo lile unalikubali.

Naweza nika hoji kitu ili nikuoneshe kuwa hicho kitu ni uongo tofauti na jinsi kilivyokuwa addressed
 
Una reasoning ya kitoto sana

Nakuuliza umejuaje hii ni nyumba unasema ni kwasababu ya uhalisia

Mtu ambaye amekaa bush miaka yote hajawahi kuona nyumba, ukimuonesha nyumba atakuwa na ufahamu wa kujua hii ni nyumba?
Na ulivyo ulivyo mjinga kwahiyo bush wanaishi kwenye nini ? Nyumba mpaka iwe imejengwa Mjini nini tena kwa matofali nini ? Muda huo huo unaniambia nina reasoning ya kitoto huku hujui maana ya nyumba. Wewe wa kupigwa makofi.

Kwahiyo vile wanavyo Jenga vijijini ni viota vya ndege au magari yale ? Kijana huna akili kabisa, yaani imekaa unaminyana hapa kumbe hata nyumba juju ni nini na unaona kwa ujinga wako vijijini hamna nyumba.
 
Nani kasema? Nani wa kumpangia eti “hakupaswa” nani ameset hiyo standard kuwa ni lazima Mungu abehave hivi na vile?
Swali sio nani kasema

Hoja ya msingi ni kweli anasifa hiyo ya upendo wote?

Ni kweli katika vitu allnavyodaiwa kuviumba vinakinzana na sifa yake?
 
Na nitafurahi ukinambia kuna binaadamu wamekumbwa na tetemeko huko mbinguni
Kwani we unajenga vipi hoja mbona hueleweki?

Hoja zako hazioneshi kuwa hakuna ubaya, ila zinaonesha uwezekano wa kutokuwepo kwa aina fulani ya ubaya

Mi najadili ubaya haijalishi kwa kiwango gani
 
Elewa nilichokiandika, napinga sharti unalo liweka. Sasa kama hata unachokiandika hukielewi hili ni tatizo lako.

Hata tunaposema Allah yupo ujue Kuna ishara za kuonyesha uwepo wake, kuanzia katika fitra (Innate disposition) na vingine. Nacho kataa hapa ni kile unacho DAI lazima uwe ume experience hicho kitu kwanza wakati siyo sahihi, kama nilivyokurudishia swali hilo juu ya jeep ushawahi ku experience kutokuwepo kwa ulimwengu mwingine mpaka ulimwengu huu uwe haujaumbwa ? Hujajibu swali hili.
Ishara ni kitu kingine hicho kinachojitegemea

Nataka uthibitishe Allah yupo bila kutumia kitu kingine
 
Ndiyo nakwambia kwakuwa the universe keeps expanding chances are there’s plenty of spaces probably we’ll never be able to fill

Sio suala la km ngap za mraba, look at the sky huwezi hata pata picha?
Sa mbona unajipinga mwenyewe?

Mwanzo umesema watu wanakufa ili kubalnce uhai kwasababu watu wasingekufa ulimwengu usingetosha

Nilivyokuuliza kuwa huko mbinguni kuna nafasi kuyasi gani kuweza kuhimili watu zaidi ya bilioni 7

Unakuja kusema ulimwengu unatanuka na kuna spaces nyingi ambayo ni kubwa kiasi hatuwezi kuienea yote.

Kwa hiyo nishike lipi?
 
Unataka kujua chanzo chake kibinadamu zaidi kitu ambacho hakiwezekani, jifunze pia kufikiri kiutu-uzima.
Nataka kujua chanzo chake kibinadam ndio, ulitaka nijue kinamna gani sasa wakat mi ni binadam!? Wewe umetumia nini kujua, kimalaika?
 
Then ukichambua unatuthibitishia vipi sisi ili tuamini kuwa ni cha kweli?
Unataka nikuthibitishie nn? Kuna mtu hapo nilimwambia kua tz walingundua fossils za dinosaurs, akabisha. Mtu kama huyo unamwaminishaje kama anabisha kitu ambacho kimetokea, kimekua documented. Ukitaka kwenda kushuhudia unaenda, ila yy bado anabisha! Mada ya huu uzi ni vice-versa kabisa, lol. Na tunazid kuona kila response inaotolewa na theists

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhalisia upo hauhitaji ushahidi kama uwepo wa Dunia, uwepo wako na mfano wa hivi.
Nimekuuliza swali utajuaje unachokiona wewe ni uhalisia na sio umepotoka tu?
 
Back
Top Bottom