Atheists wana mtindio wa ubongo

Atheists wana mtindio wa ubongo

Ndio maana nimekuuliza, utajuaje kukosa kwako majibu kunatokana na wewe kukosa majibu na sio kwamba unakosa majibu kwasababu uhalisia wa hicho kitu haupo?
Nimekwambia kuwa, kuna maswali mengine majibu yake yapo, lakini hayajulikani. Hilo nawe unalifahamu.
 
Ni kwasababu hata wewe unamuelezea Mungu kwa niaba yake

Kwa niaba yake umeamua kumsemea kuwa yeye ni mjuzi wa uumbaji

Kama unakataa kujibu maswali ya msingi kwasababu ya kudai "ni kwa niaba ya Mungu" basi kanusha madai yako yote uliyoyasema mwanzo ukimuelezea Mungu, kubali kuwa ni ya UONGO ili kweli isionekane kuwa unaongea kwa niaba yake.

Vinginevyo.....

Nilikuambia kabla hujazaliwa, Mungu alijua kuwa utazaliwa?

Alijua ni lini, wapi, na mzazi gani ambaye atakuzaa?

Au hakujua?

Siku yako ya kufa anaijua?

2025 kuna uchaguzi je Mungu ashajua yatayojiri mwaka huo au naye anasubiria mpaka watu wapige kura, wahesabu na Nec watangaze ndio naye ajue?
Kusema kwa niaba ya Mungu ni lazima utumwe na Mungu mwenyewe. Mimi sijatumwa na Mungu. Nayasema hayo yote kutokana na historia yake. Hivyo, mimi sio muongo, kwa kuwa historia haiongopi.

Bado nasisitiza, Mungu ndiye mjuzi pekee wa kila kiumbe. Kwa mambo ya tabia, Mungu alitoa mwongozo jinsi ya kuishi kwa uwiano katika mazingira yetu.
 
Okay kumbe saizi ni simple kutoa jibu kwa niaba ya Mungu?

Halafu sijajua kwanini unajitangulizia mpira kwa mbele kama Twisila

Kwasababu hakuna sehemu nimetaja mambo ya tabia wala uumbaji kwenye hoja yangu.

Kama Mungu ni mjuzi wa kila kitu, na aliona kila kitu kitachoenda kutokea kwenye ulimwengu atakaokwenda kuumba, ikiwemo mabaya, kwanini pamoja na kulijua hilo kuumba ulimwengu usioweza kuruhusu uovu?
Mimi sijibu kwa niaba ya Mungu, kwa sababu Mungu hajanituma.

Ni kweli hakuna sehemu umetaja mambo ya tabia. Lakini majibu ya maswali yako yanalemga kwenye tabia. Hata hivyo, sihitaji kibali kutoka kwako ninapojenga hojs zangu.

Mara kwa mara unarudia kuuliza maswali yaleyale ambayo nilikupa majibu yake.

Narudia kujibu kwamba sio ulimwengu unaoruhusu kutendeka maovu. Hakuna hati iliyotolewa na ulimwengu ya kuruhusu maovu kutendeka. Maovu yote ni zao la tabia batili za binadamu. Ili kuepukana na maovu ni lazima tuishi kwa kufuata mwongozo tuliopewa.
 
Kutokumbuka ni jambo la kisayansi na lina umhimu wake pia.
Uliniuliza mipaka ya ujuzi wa Mungu. Hujawa specific ni ujuzi wa nini. Lakini nilikujibu specifically, Mungu ni mjuzi wa uumbaji wa viumbe vyote.
Nilikuambia ujuzi wote (omniscient), nikimaanisha ujuzi wa kila kitu bila kuwepo limitation ya aina yeyote

Nikakuwekea na mfano wa ujuzi wote usio weza kuathiriwa na muda yani kujua yale yaliyopita, yaliyopo na yatakayo jiri mbeleni

Ukiniambia Mungu ni mjuzi wa uumbaji wa viumbe vyote maana yake umem-limit, kabla ya uumbaji huyo Mungu hakuwa na ujuzi wote au kabla ya uumbaji huyo Mungu hakuwepo.

Mungu wako ni mjuzi wa yote asiye na mipaka au kuna vitu vinafanyika bila yeye kujua?
 
Pia nilikujibujibu swali hilo anayejua ni Mungu kwa sababu hukuridhika na specific answer. Ulitaka general answer ambalo mimi silijui.
Unaongea kwa niaba yake? wewe umejuaje kama hilo swali anayejua ni Mungu?
 
Kwa hiyo, kuna maswali najua majibu yake na mengine sijui, kwa kuwa ni ya nafsi ya Mungu.
Kama hujui majibu yake tutajuaje kuwa hicho kitu unachotaka kutuambia kuwa kipo (Mungu) ni kweli yupo au hakipo ila umetumia njama kuturubuni kudai kipo ila huna majibu?
 
Nimekwambia kuwa, kuna maswali mengine majibu yake yapo, lakini hayajulikani. Hilo nawe unalifahamu.
Namimi nimekuambia, watu kulijua hilo huoni waongo wengi wakitumia nafasi hiyo kupenyeza madai ya uongo ambayo hata wakiulizwa watasema "hatuna majibu ila yapo lakini hayajulikani"

Sasa leo hii mtu akakuambia madai ya uongo kuwa ni ya kweli ila hana majibu yake lakini akakuambia majibu yake yapo, utajuaje kuwa hicho kitu alichokuambia ni cha kweli au ni cha uongo ametumia njia ya kusema hana majibu kama upenyo wa kupitisha conspiracy yake ya uongo?
 
Kusema kwa niaba ya Mungu ni lazima utumwe na Mungu mwenyewe. Mimi sijatumwa na Mungu. Nayasema hayo yote kutokana na historia yake. Hivyo, mimi sio muongo, kwa kuwa historia haiongopi.

Bado nasisitiza, Mungu ndiye mjuzi pekee wa kila kiumbe. Kwa mambo ya tabia, Mungu alitoa mwongozo jinsi ya kuishi kwa uwiano katika mazingira yetu.
Historia gani?
 
Nadhani huwa hatuwajibu ma atheist kwa hoja zilizo Shiba na zenye mantiki tumeishia ku crame our own dogmas ambazo na wao wanazijua

Kuna Muda huwa nahisi tatizo kubwa sana lipo kwetu na si kwao angalia hata Aina ya ujibuji wa sisi believers kwa atheists ni lugha za ku attack tu na si vinginevyo
 
Nilikuambia ujuzi wote (omniscient), nikimaanisha ujuzi wa kila kitu bila kuwepo limitation ya aina yeyote

Nikakuwekea na mfano wa ujuzi wote usio weza kuathiriwa na muda yani kujua yale yaliyopita, yaliyopo na yatakayo jiri mbeleni

Ukiniambia Mungu ni mjuzi wa uumbaji wa viumbe vyote maana yake umem-limit, kabla ya uumbaji huyo Mungu hakuwa na ujuzi wote au kabla ya uumbaji huyo Mungu hakuwepo.

Mungu wako ni mjuzi wa yote asiye na mipaka au kuna vitu vinafanyika bila yeye kujua?
Mimi najua ujuzi wa uumbaji. Kutojua ujuzi wote wa Mungu hakuhalalishi kuwa nam-limit Mungu. Ujuzi mwingine usiohusu uumbaji sina ufahamu nao.
 
Unaongea kwa niaba yake? wewe umejuaje kama hilo swali anayejua ni Mungu?
Hapana siongei kwa niaba ya Mungu. Nimeandika hivyo kwa sababu swali lako lilimlenga Mungu moja kwa moja.
 
Kama hujui majibu yake tutajuaje kuwa hicho kitu unachotaka kutuambia kuwa kipo (Mungu) ni kweli yupo au hakipo ila umetumia njama kuturubuni kudai kipo ila huna majibu?
Uwepo wa Mungu ni jambo la kihistoria, na historia daima haiongopi. Mungu yupo.
 
Namimi nimekuambia, watu kulijua hilo huoni waongo wengi wakitumia nafasi hiyo kupenyeza madai ya uongo ambayo hata wakiulizwa watasema "hatuna majibu ila yapo lakini hayajulikani"

Sasa leo hii mtu akakuambia madai ya uongo kuwa ni ya kweli ila hana majibu yake lakini akakuambia majibu yake yapo, utajuaje kuwa hicho kitu alichokuambia ni cha kweli au ni cha uongo ametumia njia ya kusema hana majibu kama upenyo wa kupitisha conspiracy yake ya uongo?
Labda nitoea mfano:
Mtu yeyote ukimwambia hakika ipo siku atakuja kufa, atakwabia ndio najua. Lakini ukimuuliza atakufa lini, atakwambia hajui. Kwa hiyo jibu lake lipo lakini halijulikani.
Kutojua siku ya kifo hakumaanishi kuwa hakuna kifo. Ndio maana nasema, kuna maswali mengine majibu yake yapo, lakini hayajulikani.
 
Sijui wewe uliyeleta habari za historia ulizipatia wapi

Kwani mi ndio niliyeleta habari za historia humu?
Uliniuliza Historia yake kutoka wapi, kwa maana ya kwamba unajua vianzo kadhaa vya historia. Hapo umeniaminisha kuwa unajua dhahiri historia ni nini.
 
Nadhani huwa hatuwajibu ma atheist kwa hoja zilizo Shiba na zenye mantiki tumeishia ku crame our own dogmas ambazo na wao wanazijua

Kuna Muda huwa nahisi tatizo kubwa sana lipo kwetu na si kwao angalia hata Aina ya ujibuji wa sisi believers kwa atheists ni lugha za ku attack tu na si vinginevyo
Inawezekana ni kweli. Lakini wao zaidi wanajianda kwa mabishano ya kutafuta ushindi.
 
Back
Top Bottom