Ni kwasababu hata wewe unamuelezea Mungu kwa niaba yake
Kwa niaba yake umeamua kumsemea kuwa yeye ni mjuzi wa uumbaji
Kama unakataa kujibu maswali ya msingi kwasababu ya kudai "ni kwa niaba ya Mungu" basi kanusha madai yako yote uliyoyasema mwanzo ukimuelezea Mungu, kubali kuwa ni ya UONGO ili kweli isionekane kuwa unaongea kwa niaba yake.
Vinginevyo.....
Nilikuambia kabla hujazaliwa, Mungu alijua kuwa utazaliwa?
Alijua ni lini, wapi, na mzazi gani ambaye atakuzaa?
Au hakujua?
Siku yako ya kufa anaijua?
2025 kuna uchaguzi je Mungu ashajua yatayojiri mwaka huo au naye anasubiria mpaka watu wapige kura, wahesabu na Nec watangaze ndio naye ajue?