Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Ningekutana na Pengo ningemuomba aache kuhubiri, maana waamini wake tuamue wenyewe bila kushawishiwa na dini zetu kama uovu tuupe ndiyo au hapana.
Kusema ukweli japo siwezi kunena kama Gwajima - lakini kama mkatoliki Baba Askofu kanikera sana!
 
Kwanza mimi sio CCM, pili mimi sio Mkristu, ila kwa hili la kumtukana PENGO, nipo tayari kwenda mahakamani kumshitaki GWAJIMA...This is too much

Nenda kafungue kesi kesho asubuhi kibaraka wa ccm wewe
 
Check your facts!
Kuwa kadinali haimaanishi kuwa wewe ni mkuu wa kanisa.
Pamoja na hayo, ukweli unabaki kuwa kanisa halina mamlaka ya kuwaamlia waumini kura ya kupiga. Kanisa laweza kuwaelimisha wauminj mabaya na manzuri ya Katiba pendekezwa ila uamuzi wa kupiga kura ya HAPANA au NDIYO unabaki kuwa maamuzi binafsi na huru kwa muumini mwenyewe na si kanisa.
 
Nenda kafungue kesi kesho asubuhi kibaraka wa ccm wewe

Kwa taaarifa yako mimi ni kiongozi Mwandamizi wa ADC, sijawahi kujiunga na CCM na wala sina mpango huo.. Mpe taarifa Gwajima kuwa sasa ataozea Jela.
 
Mzinzi keshamwaga mboga sasa tusubiri fisadi aje kumwaga ugali...lile andiko maarufu la wagalatia hawana akili ndio linatimia sasa
 
Gwajima ni jembe sana, hakika Huyu ndiye nabii wa kizazi hiki, enyi watanzania tumsikilize na kumuheshimu mpakwa mafuta wa Bwana, safari hii nikienda dar lazima nipite kusali kanisani kwake sabau naona ndipo kuna maneno matukufu yenye uzima.
 
Wakuu mimi naomba nchangie hoja katika uzi uliopo juu ya hayo yalioitwa matusi kwa Kardinali Pengo, binafsi nime msikiliza Gwajima na Pengo pia nimemsikia ktk crip yake...hapo jinsi ilivyo nikwamba,,maaskofu walifikia uamuzi katika baraza lao juu ya hii mahakama ya kadhi sasa Pengo baada ya kuhusishwa aliungana na hao maaskofu na kusaini ule waraka na kusema kama kitu kimetoka kwa maaskofu wa makanisa yote nchi ,,basi kitakuwa kizuri na kwa manufaa ya wengi...

Sasa badae inaonekana Pengo aliitwa mlango wa nyuma na vigogo akapewa ABCD.... na akarudi kwenye vyombo vya habari ndio akatamka yaani hapo ameonyesha hana msimamo juu ya uamuzi wake....lakini ijulikane kuwa Pengo amechagua kuwa kinyume na hata maaskofu wengine wa Romani catholic ukiacha wa makanisa mengine.

Sasa jambo hilo si Gwajima tu,ila ni wengi ambao hawakupenda kwa Pengo kutokuwa na msimamo na kuonyesha kitu mfano wa usaliti juu ya wenzie.
 
Hakika Gwajima ni mpakwa mafuta na nabii mwema sana, tunataka manabii wenye ujasiri wa kusema ukweli kama huyu.
 
Ningekutana na Pengo ningemuomba aache kuhubiri, maana waamini wake tuamue wenyewe bila kushawishiwa na dini zetu kama uovu tuupe ndiyo au hapana.
Kusema ukweli japo siwezi kunena kama Gwajima - lakini kama mkatoliki Baba Askofu kanikera sana!

At least indirect umekiri kuwa Gwajima ni mkosefu...
 
Hakika Gwajima ni mpakwa mafuta na nabii mwema sana, tunataka manabii wenye ujasiri wa kusema ukweli kama huyu.

Shardcole, Tunza heshimayako mkuu, angeweza kutumia maneno mengine lakini sio kumuita Kardinal maneno ya karaha kama yale. Nikuhakikishie tu kwamba Gwajima atasota sana Lumnde kama hatoomba radhi.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Pengo yeye kapata wapi hayo mamlaka ya kutetea hiyo katiba ya Sita na Chenge? Wacha porojo!

Nafikiri hujaelewa, hajaitetea katiba alichosema kila mtu ana haki ya kupiga ndio au hapana, na sio kulazimisha watu wapige ndio au hapana, jamani msimuhukumu Askofu wa watu, waliolazimisha ni CCM watu wasome ndio, na Maaskofu watu waseme hapana.
Siku nyingine Usione uvivu kusoma maelezo marefu ungeelewa usikurupuke.
 
hivi hajaona saizi Yake mpaka amtukane PENGO, mzeeupako mwingila hawapo !Dawa ya mjinga ni kumpuuza, Pengo wala hatomjbu

Radical problems requires radicle solutions! Pengo aliteleza kiasi kwamba ametia shaka imani iliyokuwepo kuwa anabusara. Acha wasioweza kuficha maneno wamshambulie na yeye aone ubaya wa kushambulia
 
Kwani Pengo wakati wa kikao alikua akifanya nini? Hakuyakumbuka hayo aliyoyatolea tamko by then? Au aliyasema na hakuna aliyeafikiana naye?

Kwa jinsi tamko lake lilivyo na ukweli na hekima, kama aliraise hiyo issue wakati wa kikao, hakuna mjumbe mwingine yeyote aliyeweza kuliona na kulielewa jambo hili? Alishindwa kuwaconvince?

Hayo maswali yananitatiza...kwa nini atoe tamko pembeni?
 
Shardcole, Tunza heshimayako mkuu, angeweza kutumia maneno mengine lakini sio kumuita Kardinal maneno ya karaha kama yale. Nikuhakikishie tu kwamba Gwajima atasota sana Lumnde kama hatoomba radhi.

Kwa kosa gani atasota rumande.
 
Last edited by a moderator:
Serikali inapowaambia watu wapigie kura ya Ndio katiba Mbona pengo hakusema watu waachwe waamue wenyewe?

Hiyo ilikuwa haimuhusu kwani umeshasema Serikali, Pengo sio kiongozi wa serikali, iliyokuwa inamuhusu ni sehemu ya kanisa na kama yeye kiongozi wa kanisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…