crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,250
- 893
Aisee Hapo kwenye red inaonyesha ww ni mjukuu wa Pengo aisee!! Wapi kwenye tamko kuna kulazimishana? Yaani "Mapengo" mko wengi kumbe
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama Kardinali wa kanisa Katoliki Tanzania, hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.
Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.
Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.
NB: Attachment ni mahubiri ya Mwadhama Kardinali Pengo ambayo ndiyo yamemfanya Gwajima aongee hayo