Viongozi wa kisiasa wajifunze kuweka heshima na hadhi ya nchi mbele.
Kwa mfano Marekani, wakiwa ndani ya nchi yao watapingana sana ikiwamo masuala ya siasa za nje, republican watamsema Obama kamakuhusu kuuawa kwa balozi nchini Libya, kuhusu Russia, kuhusu Ukrain, kuhusu Israel na kadhalika ni sawa pia na Obama pia alivyokuwa anamsema Bush alipokuwa madarakani kuhusu vita vya Iraq kwa mfano.Hii ni jadi ya kawaida kwenye siasa.
Lakin mwanasiasa mkubwa mwenye nafasi ya kuwa Rais akitoka nje ya Marekani anabadilika ghafla, akitoka nje y nchi nae ni Mmarekani, anawajibu wa kulinda heshima ya nchi yake, ndio jadi ya kisiasa, taifa kwanza, siasa zetu ni ndani ya mipaka ya nchi yetu, nje ya mipaka sisi ni Watanzania, ni wajibu wetu kulinda hadhi na heshima ya Mama Tanzania.
Hivyo kama Dr Slaa ameunga mkono hayo ameidharirisha nchi yake na amejishushia hadhi yake pia mwenyewe.Nchi yetu Kwanza