Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Hawa ndiyo wale waganga wanawaambia wakaue albino wanaenda kuuwa ili wapate vyeo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wao viongozi ndio inabidi wakemee huu ujinga wa kuamini waganga wa kienyeji. Mganga atakwambia chochote kutokana na anavyoisoma akili yako ili mdomo uende kinywani.

Lakini wao ndio wako mstari wa mbele kuamini huu upumbavu. Wanachotwa akili kiurahisi na kitoto sana.

Hawa viongozi hawana uwezo wa kujiongoza na kujiongeza, wataweza kuongoza nchi?
 
Kuna watu wanaraha sana nchi hii anajiaminisana kuwa yeye sio mwanasiasa hivyo Kwa kuwa haombi kura anaweza kugonga na gari na aktengeneza mazingira kuwa break ilikatika na akaeleweka. Hili SI kosa kabisa yule panya rood Dangote anayetumia viwembe katwezwa utu huyu anayetumia chupa Yuko huru.
 
Hongereni wananchi wa Babati.

Haki imeshinda,Umoja wenu ndiyo ulinzi wenu sasa mtuhumiwa wetu yupo katika mikono salama ya Jeshi la Polisi Tz.

Jaribio lake la Kutoroka mkono wa sheria limezimwa na Wananchi na sasa Polisi wamemtia mbaroni mualifu wetu.

Sasa anachukuliwa MAELEZO YA ONYO katika Ofisi za RCO,Manyara

Pauline Gekul alipanga kutokea Nairobi,Kenya [emoji1139] leo alfajiri baada ya jana Gekul kupata taarifa za kutaka
1.kushtakiwa na 2.Kufukuzwa uanachama wa CCM Wilayani Babati.

Umoja mlio onyesha wananchi wa Babati usiishie hapo tu.

Jutitokeze Kwa wingi Mahakamani ili haki iweze Kuonekana ikitendeka.

Najua Babati inafuraha kama imepata uhuru tangu Jana,lakini tuendelee na kazi ya doria.

Ukatili na ualifu dhidi ya utu unapaswa Kupingwa na dini zote,Itikadi zote na jamii yote mahala popote.

View attachment 2826266

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnafaidika nini kwa kuzusha mambo ya uongo..?
Chadema mmekuja kuwa wajinga sana.
 
Nimeisikiliza hii audio kwa makini... alichokosea bwana Emmanuel kwa mtazamo na maoni yangu ni kauli. Baadhi ya Vitisho alivyotoa ni hatari na sheria inaweza kumuadabisha ila huyo Paulina naona anapayukapayuka tu! Anaonesha wazi kweli akili na busara hana!

Pia bwana Emmanuel amekosea sana kuingilia kati makosa aliyoyafanya dada yake.
 
View attachment 2825594
EMMANUEL GEKUL ambaye ni mdogo wake mbunge wa Babati Mjini (CCM), Pauline Gekul akimtishia kumuua kwa kumkata kichwa na kumpiga risasi PAULINA SLAA NARSIS mkazi wa Babati Mjini akimtuhumu kusambaza video za Hashimu Ally.

HASHIMU ameeleza jinsi alivyotekwa, kuteswa akiwa ameshikiwa bastola na kuwekewa chupa sehemu yake ya haja kubwa kwa amri ya Pauline Gekul, akiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria. Wakazi wa Babati Mjini walichukizwa na kitendo hicho, wengine wakaamua kusambaza taarifa ile WhatsApp.

EMMANUEL GEKUL anasikika katika video hiyo yenye sauti akimchimba mkwara mzito na kumueleza PAULINA SLAA NARSIS atamkata kichwa na kumpiga risasi kwa kusambaza video hizo za Hashimu. Gekul ametukana matusi mengi ya nguoni. Gekul anatamba kwamba anaweza kumuua na Babati ikatulia.

PAULINE na EMMNAUEL wanapata kiburi kwa nani? RPC Manyara upo? RCO upo? Raia wa Babati anatishiwa maisha yake kwa sababu ya kusambaza taarifa za UOVU wa PAULINE GEKUL? Familia ya GEKUL imelimeza jeshi la polisi Manyara na Babati wanaitawala kifalme? Tunataka EMMANUEL anachukuliwa hatua za kisheria iwe fundisho.

PAULINA SLAA NARSIS ametoa taarifa za kutishiwa kuuwawa kwa kuchinjwa na kupigwa risasi na EMMANUEL GEKUL, lakini hadi sasa hakuna lolote ambalo linaendelea. RPC unajua vizuri hili suala. EMMANUEL GEKUL anasema jeshi la polisi Manyara kwake siyo lolote na haogopi. Je, ni kweli familia ya GEKUL imelishika jeshi la polisi Manyara?

IGP, tunataka jeshi la polisi Manyara na Babati, lichunguzwe na ikibainika kuna watu wanakula njama za kutenda uhalifu kwa kushirikiana na familia ya GEKUL, wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria. Hatuwezi kuwa na watu katika utumishi wa jeshi la polisi wanaoshirikiana na wahalifu kutenda UHALIFU wa kutisha kwa binadamu wenzao.
Ni series ya kutafutana kisiasa, na bahati mbaya mtafutwaji hakugundua mapema.
 
Huyu Pauline aliwezaje kuwa naibu waziri? Anaonekana mweupe kabisa kichwani hata kwa uzungumzaji wake tu.
 
Back
Top Bottom