Augustino Mrema: Behind the Scene

Augustino Mrema: Behind the Scene

Ni kiongozi pekee wa upinzani aliyepigwa mabomu kuliko wote.
Mpiga mabomu baadaye akaja kuwa IGP (mahita)
 
ni mwanasiasa pekee aliyewahi kuwa mbunge kwenye vyama vitatu tofauti...vunjo akiwa ccm, temeke akiwa nccr, na sasa vunjo tena akiwa na TLP, Jogoo
 
Alitoa somo kwa Rais wa nchi kutokwenda katika kampeni za chaguzi ndogo kwani baada ya Ben na serekali yake kuangukia pua pale temeke alikoma kwenda kwenye kampeni za by-election.
 
  1. Mujahidina waliovunja mabucha ya Kitimoto pale magomeni kagera hawatomsahau kwa kichapo walichoshushiwa
  2. Ni waziri pekee aliekuwa anaingia front line kusaka polisi wanakula rushwa kuvusha mali za magendo.
  3. Mkristu ambae mda wote ametinga kibarakashea
  4. alianzisha utaratibu wa kuwazawadia wananchi wanaofichua uhalifu. kwa kuwapa 10%
  5. Alianzisha utaratibu wa kukutana na wananchi one to one ambapo baadae mzee Mwinyi akau copy
 
Alisema yeye ni Jogoo na Mrema mdogo aliyekuwa ana gombea Vunjo ni Mtetea..... Mrema is really brainy..... ni ugonjwa gani sijui umemkabaaa.... anadhoofika daily.....
 
Alisema yeye ni Jogoo na Mrema mdogo aliyekuwa ana gombea Vunjo ni Mtetea..... Mrema is really brainy..... ni ugonjwa gani sijui umemkabaaa.... anadhoofika daily.....

Unamaanisha lile jogoo la Lusinde pale Usa River?? Lol... walau nimetabasamu.
 
hii thread kaanzisha mwenyewe mzee wa kiraracha pole sana mzee

Mkuu najua hujapendezwa na kile kilicho elezwa hapo juu, ila ki'ukweli yakupasa kumpatia Mrema heshima. huyu mzee anafanya kazi zake vizuri sana, yan beyond our expectations, pamoja ni mzee anawakamata mafisadi vyema! MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE APEWE. BIG UP DR. MREMA!
 
Join Date : 18th March 2007
Location : Bremen
Posts : 2,834
Rep Power : 5267
Likes Received195
Likes Given141


majungu.blogspot.com...nasikia utaaaaaaaaaamuuuuuuuuuuu
 
Mwache huyu mzee apumzike na hata afya yake imekuwa mgogoro, naona kama unampigia Debe!!!
 
Heshima kwako Idimi Mnazi mwenzangu wa mashetani wekundu.


Naomba niweke records sawa.Cheo cha naibu waziri mkuu kiliwahi kushikwa na Mheshimiwa Salim A Salim kipindi hicho Rais alikuwa Mzee Ruksa waziri mkuu alikuwa Mzee J Warioba kabla hajapigwa chini na nafasi yake kushikwa na Cigweimisi Malecela.Mrema A L alipewa nafasi ya nibu waziri mkuu baada ya kumaliza mgogoro wa Meru ambao ulikuwa umetia doa serekali ya Mzee Ruksa.

Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Katika kikao cha saba cha bunge lilohitimishwa jana, kamati yake ya Hesabu za serikali a mitaa ilitoa ripoti moja nzuri sana juu ya ubadhirifu mkubwa ulioonekana katika serikali za mitaa. Kamati yake, tofauti na kamati nyingine za bunge, ilithubutu kutaja kwa majina na mahali walipo wahusika wa ubadhirifu wa mali za halmashauri na kutoa mapendekezo mazuri sana ya hatua za kuchukua dhidi ya wahalifu hao na namna ya kuzuia wizi huo kwa siku zijazo. Mheshimiwa huyu aliongea kwa uchungu sana namna anavyoumizwa na wizi huu, huku huduma za kijamii zikizorota kwa kukosa pesa.

Behind the Scene (vibwagizo)

  • Mrema ni mtu pekee ambaye amewahi kupewa cheo kisichotambulika katika katiba ya nchi (Naibu waziri Mkuu), enzi za mzee Ruksa. Enzi hizo pia alikuwa ni waziri wa mambo ya ndani na utendaji wake ulijulikana sana.
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mbunge katika majimbo mawili tofauti. Alikuwa mbunge wa Jimbo la Temeke mkoani Dar Es Salaam mnamo mwaka 1996 baada ya mahakama kutengua ubunge wa Ally Kihiyo, ambaye alighushi elimu yake katika wasifu wake, na kwa sasa Mrema ni mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro
  • Ni mtu pekee ambaye amekuwa mwenyekiti wa vyama viwili tofauti vya kisiasa kwa nyakati fofauti na amegombea uraisi kupitia vyama hivi viwili tofauti. Alikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mnamo mwaka 1995 enzi hizo Mabere Marando akiwa katibu mkuu na aligombea ubunge mwaka huo. Alihama NCCR na kuhamia TLP ambako alimpindua Leo Lwekamwa na kumtimua Thomas Ngawaiya aliyemkuta hapo, na amegombea uraisi mara mbili kwa tiketi ya chama hiki.
  • Ni mmoja wa wabunge waliokunywa 'Kikombe' cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo

Mwenye vibwagizo zaidi aongezee
Nawasilisha
 
Ni mwanasiasa mbunifu vituo vidogo vya polisi ni ubunifu wake.
 
Ni mwanasiasa mbunifu vituo vidogo vya polisi ni ubunifu wake.
Alimpiga mkwara singa singa akafa kwa presha mjini Arusha, baada kutaka Yeye (mr singh) na wakili wake wamuone ndani ya siku saba ! Siku ilipofika Mrema akapokea summons ya Mahakama Kuu. Akamtaka radhi Wakili !
 
Back
Top Bottom