TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

Augustino Lyatonga Mrema ndiye aliyeasisi vuguvugu la mageuzi nchini kwenye ngazi za uchaguzi na ile 1995 wale mliokuwepo mnajuwa kabisa bila Nyerere kuingilia Kati Nccr Mageuzi ingekuwa Chama Tawala

Mrema amekuwa msema kweli asiyetawaliwa na tamaa

Mrema hakuwa mbinafsi ndio sababu alipowasapoti Kikwete na Maguful kwenye Uchaguzi hakuwalazimisha wanachama wa TLP kufuata Msimamo wake

Rest in peace Lyatonga

Vijana msilale bado mapambano - 1995
 
Nakumbuka mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi 1995, uwanja wa shule ya uhuru palivyofurika,
Hofu iliwajaa watawala hadi kuchakachua matokeo yaliyompa Ben ushindi,
Pumzika kwa amani meku Mrema
 
Enzi za uhai wake wakati anagombea urais kupitia upinzani Nyerere aliiba kura na kupora chaguzi ili kuinusuru CCM[emoji16][emoji16][emoji16]
Pia walimfanyia kampeni chafu, walipandikiza mwanamke mmoja akadai amezaa na Mrema kisha akamtelekeza,

Akawa anashinda getini kwa Mrema masaki kwanye nyumba aliokuwa anakaa,
Kabla ya Mrema kufukuzwa na kuhamia Sinza,
CCM ni mabingwa wa siasa chafu na fitna,
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma Salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania

"Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa chama cha TLP Bw. Agustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo asubuhi Jijini Dar es Salaam. Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania. Pole kwa familia na wana TLP. Mungu amweke mahali pema.Amina"

==
==
Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.


Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12: 15.


Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro na amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Chanzo
Code:
https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/augustino-mrema-afariki-dunia-3921264
https://www.ippmedia.com/sw/habari/augustino-mrema-afariki-dunia
 
MUNGU AMPOKEE MJA WAKE AMUWEKE MAHALI PEMA PEPONI.

NAFUU KWA UPINZANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…