Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Muigizaji nchini, Aunt Ezekiel, amemmwagia sifa kedekede mumewe, msanii wa muziki Kusah, na kumwelezea kama mwanaume aliyeumbwa mahsusi kwa ajili yake kutokana na moyo wake wa kujitolea na kuwajibika kikamilifu katika familia.
Aunt Ezekiel aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati wa maandalizi ya tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva. Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Kusah.
Katika maelezo yake, Aunt Ezekiel alifunguka kuwa Kusah amekuwa akigharamia elimu ya mtoto wake aliyezaa na aliyekuwa mpenzi wake, Mose Iyobo, katika shule ya gharama kubwa ya Feza.
"Kusah naweza kusema ni mwanaume aliyeumbwa kwa ajili yangu. Siyo rahisi mwanaume kulipa ada ya mamilioni kwa mtoto asiye wake huku baba wa huyo mtoto yupo hai. Kusah analipa ada ya mwanangu niliyezaa na Iyobo, halafu shule yenyewe ni Feza, pale ada yake ni mamilioni lakini Kusah analipa. Kusah ni mwanaume hasa, yule mwingine nilikosea," alisema Aunt Ezekiel.