Aunt Ezekiel: Kusah ni mwanaume hasa , yule mwingine nilikosea

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Muigizaji nchini, Aunt Ezekiel, amemmwagia sifa kedekede mumewe, msanii wa muziki Kusah, na kumwelezea kama mwanaume aliyeumbwa mahsusi kwa ajili yake kutokana na moyo wake wa kujitolea na kuwajibika kikamilifu katika familia.

Aunt Ezekiel aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati wa maandalizi ya tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva. Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Kusah.

Katika maelezo yake, Aunt Ezekiel alifunguka kuwa Kusah amekuwa akigharamia elimu ya mtoto wake aliyezaa na aliyekuwa mpenzi wake, Mose Iyobo, katika shule ya gharama kubwa ya Feza.

"Kusah naweza kusema ni mwanaume aliyeumbwa kwa ajili yangu. Siyo rahisi mwanaume kulipa ada ya mamilioni kwa mtoto asiye wake huku baba wa huyo mtoto yupo hai. Kusah analipa ada ya mwanangu niliyezaa na Iyobo, halafu shule yenyewe ni Feza, pale ada yake ni mamilioni lakini Kusah analipa. Kusah ni mwanaume hasa, yule mwingine nilikosea," alisema Aunt Ezekiel.





 
Kama ingekuwa mimi huyo kusa ningemkataza kusema hili maisha yake yote,how uufunue ufala wangu mbele ya jamii?yaani kwa hiyo wanaume wote sasa mpaka baba wa mtoto tunajua kwamba dogo anasomesha bao la mtu!
 
Sema kusaha mwanaume kweli maan sio rahisi ila yangu macho siku baba akiwashe kutaka mtoto wake
 
Ukisifiwa ujue unaongezewa dozi ya ufala
 
Ngojea wakiachana tutajua ukweli,hata Shilole kwa Uchebe na Mzuwanda ilikiwa hivi hivi,baada ya kubwagana akaamua kuyabwaga.
 
Too much pepee ptu ptu ptuu (Kanumba Voice)

Chalii anasetiwa na mshangaz uliomaliza ngwe, ex nayeye ajibu mapigo na Masha manyonyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…