Aunty Ezekiel na Demonte wameremeta Dubai

Aunty Ezekiel na Demonte wameremeta Dubai

Kwa macho yangu ya kibinadamu, naona kama bwana harusi mdogo sijui!

Anyways, hayo ni ya kibinadamu bado nawatakia heri kwenye maisha yao ya ndoa. Tusimshambulie Aunt jamani, kwani kila binadamu ana nafasi ya kubadilika na kusonga na maisha kiupya...remember every devil has a future and every saint had an evil past.....wahenga walinena jama....
 
Amependeza, kabwana kama katoto fulani hivi. Kuna watu wanapenda kuchafulia wenzao majina si juzi tu walisema kafumaniwa

Anyways ubarikiwe kwenye ndoa yako.

hako katoto ni rahisi kukaweka sawa, kufumaniwa sio tatizo hapo.
 
Yaani kuna negative comments nyingi kwenye post hii kuliko positive comments.. Tukumbuke hakuna alie msafi au kukamilika machoni pake Muumba wetu.. Bibie ameolewa mnamsema vibaya na wengine mkimuombea aharibu mapema ili nafci zenu ziridhishwe na unabii wenu wa kiza..! Mmesahau anaejiona msafi ndio awe wa kwanza kumrushia neno baya huyu dada..
Kila la kheri Bi Rahma katika maisha yake ya ndoa.. Akiunganishacho Mungu binaadam hana uwezo wa kukitenganisha..

Ya kweli haya,mbona wenzetu wana talaka na wengine kuwa na vyuo vingi ni ufahari..
 
Ili uvae make ikupendeze lazima uikubali reality

Hivi mtu mweusi mashavu kuwa pink maana yake nini?

Pink is meant for light skin ambao wakicheka ama tabasamu mashavu yao yanakuwa pinkish, kama ku-enhance smile.

Hakuna kitu sipendi kama mweusi aweke mashavu ya pink

Ila kiukweli im am so happy with my choice not to wear makeup. Aunty Ezekiel you look far way beautiful bila mikorogo hiyo. Make up zinazeesha.
 
Ya kweli haya,mbona wenzetu wana talaka na wengine kuwa na vyuo vingi ni ufahari..

Mkuu Mbona hata Wakristo talaka inatambulika ila ni pale tu uzinzi unapokuwa umethibishwa kufanyika.. Hayo ya vyuo vingi ni maridhiano na aliewahi mji.. Maana kuna sheria ambazo baadhi ya wanaume wakware wanaikiuka katika kuweka vyuo vingi...
 
Ila kiukweli im am so happy with my choice not to wear makeup. Aunty Ezekiel you look far way beautiful bila mikorogo hiyo. Make up zinazeesha.

tupo pamoja, huyu dada ni mrembo sema hayo ma makeup yameharibu kabisa kabisa.
 
nadhani wa kwenye picha ni mpambe.......SIAMINI AU NDIO FREE MASON?
Huyo Demonte ni nani jamani mbona kama katoto au ni baby face tu?ajipange kweli kweli!!huyo ni msanii hadi kwenye maisha ya kila siku!!kila la kheri
 
Mkuu Mbona hata Wakristo talaka inatambulika ila ni pale tu uzinzi unapokuwa umethibishwa kufanyika.. Hayo ya vyuo vingi ni maridhiano na aliewahi mji.. Maana kuna sheria ambazo baadhi ya wanaume wakware wanaikiuka katika kuweka vyuo vingi...

All in All,huyo kijana ipo siku isiyo na jina, ATAJUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUTA KUMFAHAMU huyo binti.............
 
Wamependeza, tunawatakia kila la kheri kwani wamefanya jambo jema, nami naungana na mchangiaji mmoja kuwa ndoa si maigizo, pendaneni,vumilianeni,heshimianeni na mujue hakuna u-super star kwenye ndoa mkifahamu kuwa nyie ni mwili mmoja hakika ndoa yenu itakuwa ya furaha.......MUBARIKIWE
 
Hongereni kwa kukubaliana kuwa mwili mmoja, ila isije ikawa ndo yale ya paka kufungwa na panya sehemu moja???
 
nilisikia mume aliyefunga naye ndoa sio alibadili jina mumewe alikuw Dubai kwa hiyo imesemekana ndoa batili tutasikia mengi......kila la heri
 
Back
Top Bottom