Aunty wa mjini alinisimulia alivyowekeza kupitia udangaji

Aunty wa mjini alinisimulia alivyowekeza kupitia udangaji

Kipindi ambacho jinsi ya mawasiliano ni barua tu, akaanzisha biashara ya nini akichukua mzigo Dubai?
eti spea za pikipiki, Sasa alikuwa anamuuzia Nani hizo spea wakati hakukuwa na pikipik nying mtaan!? Chache zikiwa na zile 110 za watumishi wachache wa serikali.
 
Aunty yuko kwenye 50’s lakini bado mzuri na anavutia. Anasema wakati akiwa form five walifanya shule ili organise fundraising dinner. Ilikua na fashion show. Baada ya kupita na mavazi tofauti mezani pale katika miondoko ya catwalk, mgeni wa heshima alimpenda. Mgeni wa heshima alikuwa Waziri. Enzi hizo hakuna simu za mkononi.

Waziri alimtuma dereva shuleni na kopo la biscuit, juice, matunda na pesa laki moja kwenye bahasha ya khaki. Ndani ya bahasha kukikua na barua kuwa anachohitaji awe anakwenda ofisini kwa Waziri. Baada ya kumaliza shule alikua free zaidi kwani chuo kidogo uko free hubanwi kama shuleni.

Safari zote za Ulaya alisafiri na Waziri, alitangulia airport wanakutana na Waziri huko huko. Wakati ofisini anasema anakwenda na mke wake. Huko Ulaya akipelekwa madukani ananunua viatu pair tano, handbags, perfumes vile vya majina makubwa. Akirudi anauza kwa wenzake na hela aliweza kununua kiwanja Kawe enzi hizo bado porini.

Alipoachana na Waziri, passport yake ilikua na mihuri na visa za nchi kama tatu. Ilimsaidia kupata visa kirahisi. Danga la pili lilikua mfanya biashara. Date ya kwanza mzee alimpa milioni moja ajiweke sawa kimavazi. Anasema alitumia kama laki moja na nusu kwa nguo ili danga lione mabadiliko nyingine alianza kununua spare za pikipiki Dubai. Enzi hizo laki nane inatosha mtaji.

Alikuja kuolewa na kuwa na familia lakini kila danga lina kumbukumbu inayoonekana katika maisha yake.
Hivi kuwa na duka la spea za pikipiki ni mafanikio ya kujigamba mbele za watu?
Japo stori ni ya kutunga lakini bado haina sense.
 
Back
Top Bottom