Aweso aelekeza mabadiliko ya mfumo na utendaji mamlaka ya maji Ushirombo

Aweso aelekeza mabadiliko ya mfumo na utendaji mamlaka ya maji Ushirombo

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameitembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Ushirombo (UWASSA) Wilayani Bukombe mkoa wa Geita kujionea hali ya utendaji na utoaji huduma ya Maji wa wananchi na kupokea taarifa ya utendaji kazi sambamba na kujionea mazingira ya watumishi.

Waziri Aweso akiwa eneo la ofisi za Mamlaka hiyo baada ya tathimini na kutoridhishwa na utendaji wa kazi amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuiweka Mamlaka ya Maji Ushirombo katika uangalizi maalumu na kumpa maagizo ya kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika namna ya kuboresha na ustawi wa Mamlaka hiyo ya Maji.
IMG-20250327-WA0043.jpg
IMG-20250327-WA0041.jpg
IMG-20250327-WA0044.jpg
IMG-20250327-WA0042.jpg
 
Back
Top Bottom