Aweso amesema baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wanafanya kazi wanavyotaka wao na wengi wao wameonesha hawana uwezo wa kufanya kazi.
“Niliwauliza mmoja mmoja, huduma inayotolewa kwa wananchi na Mwauwasa inaridhisha kila mmoja akasema huduma hairidhishi na kwa kuwa walisema hivyo na ukweli unafahamika kuanzia leo nawasimamisha waondoke ofisini,” amesema Aweso.
Waziri Aweso, anafikia uamzi huo baada ya kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Jiji la Mwanza wakilalamikia ukosefu wa maji safi na salama.
Ukosefu wa maji kwa wananchi unatajwa kuchangiwa na watumishi kutowatumikia wananchi kwa kuangalia changamoto zinazowakabili za kuwapa huduma ya maji safi na salama.
Aweso anasema wananchi wamekuwa wakiomba kuunganishiwa maji lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa ya kuwaunganishia maji.
Pia amegusia vitendo vya baadhi ya watumishi idara ya ufundi kushindwa kutekeleza kazi yao kwa kufika katika maeneo mbalimbali ya wananchi kuangalia hali ya matengenezo ya mambo Badala yake wanaendekeza rushwa.