Aweso: IRUWASA ikamilishe mradi wa muda mfupi ndani ya mwezi, Vijiji vya Luhindo na Lulanzi vipate maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso​
Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Iring (IRUWASA) kuhakikisha katika kipindi cha mwezi mmoja inatekeleza mradi wa muda mfupi kuhudumia Kaya zipatazo 23 zinazokosa maji katika Vijiji vya Luhindo na Lulanzi wakati mradi mkubwa wa kuhudumia Mji wa Iringa Kilolo na Ilula unaoendelea kutekelezwa kwa gharama ya Tsh Bilioni 270 na unaotarajiwa kukamilika Mwaka 2029 ukiendelea.

Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, Eng. David Pallangyo amesema amepokea na kuahidi kutekeleza maelekezo ya Waziri kwa kutekeleza mradi mdogo wa muda mfupi kuhudumia kaya hizo na Utekelezaji umeanza mara moja.

Hoja ya awali ya Mdau ~ Lulanzi – Iringa: Hatuna maji, tukihoji Mamlaka ya Maji (IRUWASA) wanasema tusubiri Mradi mkubwa wa Mwaka 2029
​
Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, Eng. David Pallangyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…