Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka watoa huduma binafsi ya visima kutoa huduma hiyo kwa kuzingatia taratibu za uuzaji zilizowekwa kisheria ikiwemo maji bei elekezi na kuhakikisha maji hayo yana ubora.
Amewataka wamiliki wa visima binafsi na vya umma kuendelea kutoa huduma hiyo kwa ufanisi hasa kwa kipindi hiki cha upungufu wa maji ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma.
Mhe. Aweso ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea matengenezo ya bomba kubwa la maji la inchi 72 inayoendelea katika kata ya Wazo, Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Serikali inatambua ushirikiano mzuri uliopo na wamiliki wa visima kwa kuwa ni muhimili mkubwa utakaosaidia upatikanaji wa huduma muda wote hasa katika kipindi hiki cha upungufu wa maji.
"Niwatake watoa huduma binafsi wa visima kutoa huduma kwa weledi kwa bei elekezi iliyowekwa kisheria, pia nitoe wito kwa wakuu wa wilaya kusimamia utoaji wa huduma kwa wananchi." amesema.
"Nipende kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali iko kazini katika kupambana ili huduma ya maji iweze kurejea katika hali yake ya kawaida, zipo jitihada mbalimbali zinaendelea ikiwemo kukamilisha mradi wa maji Kigamboni- utakaohudumia maeneo ya katikati ya mji, tunatarajia mradi utazalisha lita milioni 70 hivyo kupunguza changamoto ya maji kwa kiasi kikubwa," ameeleza.
Ameongeza kuwa mkakati wa muda mrefu uliopo ni ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha maji Kidunda utakaoongeza upatikanaji wa maji kwa maeneo ya Jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani.
@wizarayamajitz
@jumaa_aweso