Mapinduzi ya Iran ya 1979 yalifanyika kwa sababu wananchi wengi wa Iran kwa kipindi hicho walikuwa wamechoshwa na utawala wa kifalme wa Shah Mohammad Reza Pahlavi, aliyekuwa akitawala kwa nguvu nyingi, ukandamizaji wa kisiasa, na kuonekana kuungana sana na nchi za Magharibi, hasa Marekani, ambayo ilionekana kuingilia masuala ya ndani ya Iran. Wananchi walichoshwa na Hali hiyo. Hasira kwa ukandamizaji, ukosefu wa haki za kisiasa, na hali ya kiuchumi iliyokuwa ngumu kwa kipindi hicho walikusanyika chini ya uongozi wa Ayatollah Ruhollah Khomeini ambaye alitaka serikali ya Kiislamu badala ya utawala wa kifalme. Finally, maandamano makubwa na shinikizo la umma yalimlazimisha Shah kutoroka nje ya nchi Januari 1979, na Khomeini na wafuasi wake walichukua madaraka, wakaunda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.