Ayatollah Khamenei kuongoza Sala ya ijumaa Leo na kutoa hutuba nzito

Ayatollah Khamenei kuongoza Sala ya ijumaa Leo na kutoa hutuba nzito

Wadau hamjamboni nyote?

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei anatarajiwa kuongoza sala ya Ijumaa na kutoa hotuba ya hadhara ambayo wengi wanadhani inaweza kueleza mipango Iran baada ya shambulio kubwa la kombora dhidi ya adui yake Israel.

Hotuba hii adimu ya Khamene itakiwa ni ya kwanza baada ya takriban miaka mitano na inakuja siku tatu kabla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza, vilivyoanzishwa na shambulio la kundi la kigaidi la Wapalestina lililoungwa mkono na Iran tarehe 7 Oktoba.

Kiongozi huyo mkuu, ambaye ana mamlaka ya juu kabisa nchini Iran, ataongoza Waislamu katika sala kwenye msikiti mkubwa wa Imam Khomeini Grand Mosalla katikati ya Tehran, kwa mujibu wa tovuti yake rasmi.

Sala hiyo itafuatia "sherehe ya kumbukumbu" saa 4:30 asubuhi kwa Hassan Nasrallah, kiongozi aliyeuawa wa kundi la kigaidi la Hezbollah lenye uungwaji mkono wa Tehran nchini Lebanon.

Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, ambao wanamtii Khamenei, walisema mashambulio ya makombora 200 siku ya Jumanne yalikuwa ni kulipiza kisasi kwa kuuawa kwa Nasrallah pamoja na kamanda wa Walinzi, Abbas Nilforoushan, katika shambulio la mwishoni mwa Septemba huko Beirut, na kuuawa kwa kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, huko Tehran mnamo Julai.

Khamenei mara ya mwisho aliongoza sala ya Ijumaa mwezi Januari 2020 baada ya Iran kufyatua makombora kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Iraq, kufuatia shambulio lililomuua kamanda mashuhuri wa Walinzi wa Mapinduzi, Qassem Soleimani.

===================================================

Iranian Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei is set to lead Friday prayers and deliver a public sermon that could shed light on the Islamic Republic’s plans after a massive missile attack on enemy Israel.

Khamenei’s rare Friday sermon — a first in almost five years — comes three days before the one-year anniversary of the Israel-Hamas war in Gaza, triggered by the Iran-backed Palestinian terror group’s October 7 attack.

The supreme leader, who wields the highest authority in Iran, will lead Muslims in prayer at the Imam Khomeini Grand Mosalla mosque in central Tehran, his official website says.

The prayer will follow “a commemoration ceremony” at 10:30 a.m. local time for Hassan Nasrallah, the slain leader of Tehran-backed Lebanese terror movement Hezbollah.

Iran’s Revolutionary Guards, who answer to Khamenei, said Tuesday’s barrages of some 200 missiles were in retaliation for Israel’s killing of Nasrallah alongside Guards commander Abbas Nilforoushan in a late September strike on Beirut, and of Hamas leader Ismail Haniyeh in Tehran in July.
Khamenei last led Friday prayers in January 2020 after Iran fired missiles at a US army base in Iraq, in response to a strike that killed revered Revolutionary Guards commander Qassem Soleimani.


Wazee kwa miwasho, si muda ataungana na Nasilallah.
 
Sio raisi huu muda ni wa kuishi kwa maandaki km 100 kwenda chini,vichwa vinatafutwa kwa hudi na uvumba na hatutumii simu ni mwendo wa barua tu
Na hata huko chinibya mahandaki yuko na wayahud wanao subiri tu order ya kumuondoa. Kwakifupi hayupo salama
 
Ndani Ya Huo Msikiti Leo Utakuta Mapandikizi Ya Israel, US, UK Tele
Anaweza Asimeze Mate Yakawa Machungu
Huyu ndiye mwanaume hasa anatangaza kabisa atakuwa msikiti upi na sio kama panya wengine kama kina Netapaka wanaishi kama nguchiro.

Hao mapandikizi wakijulikana ni mwendo wa kutia vitanzi tu Iran hana mzaha na mashoga.

Mashushushu kibao wa Israel wamepigwa kitanzi pale Iran baada ya kugundulika wanafanya kazi ya ushushushu.
 
Na hata huko chinibya mahandaki yuko na wayahud wanao subiri tu order ya kumuondoa. Kwakifupi hayupo salama
😂😂😂 Wayahudi weusi buana. Hivi kama Mazayuni yangekuwa na uwezo wa kumuua Ali Khamenei unadhani hiyo fursa wangeichezea?

Ayatollah ndiye anayeamrisha Israel ashambuliwe halafu unazungumza mambo mnayopigana kamba na wachungaji wenu uchwara.
 
Ni swala la Muda tu, ataliwa MTU Kichwa.Nahisi tarehe 7 October litakamilishawa hili.
 
😂😂😂 Wayahudi weusi buana. Hivi kama Mazayuni yangekuwa na uwezo wa kumuua Ali Khamenei unadhani hiyo fursa wangeichezea?

Ayatollah ndiye anayeamrisha Israel ashambuliwe halafu unazungumza mambo mnayopigana kamba na wachungaji wenu uchwara.
Ayattoúllah hawezi kuuwawa bila kibari cha Marekani.

Marekani wana spare uhai wa Ayattoullah kwa malengo yao ya kisiasa.
 
Ubabe sio kuuwa viongozi kama ndio tungeona mussa na Ukraine vita ni sayansi nani yupo juu tutamuona akimbutua mwenzie😭😭 sio unamvizia adui yako kalala unampiga jiwe au boom afu majinga mazezeta wanakusifia wkt njia iyo ni ya mnyonge asie na mguvu kupigana waziwazi ukapewa jina zuli la UGAIDI mpaka sasa Iran ndio super powerful. atumii ugaid kukupiga vitoto ndio ukikibutua kinakimbilia mawe😂😂😂😂😂😂 kazi kwenu Israel aka jehova tumtazame kuwa ni katoto mbele y Iran atatuambiya mwenyewe kwa jinsi atajibu.tuupe muda heshima😟😟
 
Kitendo cha mwanaume kusimama na kuhutubia DUNIA na uzi umekimbiwa na mayahudi wa mchamba wima.
 
Ayattoúllah hawezi kuuwawa bila kibari cha Marekani.

Marekani wana spare uhai wa Ayattoullah kwa malengo yao ya kisiasa.
Ndiyo yalikuwa mahubiri ya Gwajima jumapili iliyopita?😂😂😂

Maana jamaa kwa fiksi tu kwa waumini wake hajambo na mnavyomuamini sasa.😂😂

Iran is there to stay. Huyu ndiye mwanaume halisi wa Mashariki ya Kati.
 
Wakati anatoa hotuba yake leo ya Ijumaa, Ayatollah ilionekana pembeni yake kuna bunduki.

Iliashiria nini kwa kiongozi huyu mwenye miaka zaidi ya 80?? Lengo lilikuwa nini?? Kuna wajuzi wa kijasusi humu watatujuza ! Karibuni!

lcimg-248c9b56-414d-4992-87e6-f16dcad5c251.jpeg

Ali Khamenei standing by a rifle :Reuters

Ayatollah.jpg


Rifle in his hand, Iran's Supreme Leader warns Israel 'will not last long'​

 
Back
Top Bottom