jamaikatz
JF-Expert Member
- Jul 11, 2023
- 400
- 1,429
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ametoa kauli nzito akidai kuwa Marekani iliingilia kwa haraka operesheni ya kijeshi ya Iran kwa sababu waliogopa Israel kuangamizwa kabisa.
“Marekani iliingilia kwa sababu waliona mradi wao wa Kizayuni ukiporomoka mbele ya macho yao. Walijua wazi kuwa bila msaada wao wa haraka, utawala bandia wa Israeli ungefutwa kwenye uso wa dunia,” alisema Khamenei.
Kiongozi huyo ameendelea kusisitiza kuwa nguvu za kijeshi na ushawishi wa Iran katika ukanda huo ni wa kiwango cha juu, na kwamba Marekani inatambua ukubwa wa nguvu hizo.
Kauli hii imezua mjadala mkubwa duniani, huku wengine wakiona kama onyo kali kwa Marekani na washirika wake, hasa ikizingatiwa mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati.
Je, una maoni gani kuhusu kauli hii ya Iran dhidi ya Marekani na Israel?