Azam akipata leseni ya kuonesha EPL na UEFA, hawa DSTV kwisha habari yao

Azam akipata leseni ya kuonesha EPL na UEFA, hawa DSTV kwisha habari yao

Kwa hayo usemayo ndio uifananishe na Azam?
Ndio haifanani ila vinazidiana km umeangalia Azam kisha umeangalia DSTV havifanani hata kidogo kuna utofauti especially kwenye suala la movie uzuri wa DSTV ina Channels nyingi nyingi nyingi za kila aina ndio maana nimekwambia kuna Channels mpaka hizo za Pirates
 
Itawavutia wengi kwa maana atapata package ya michezo ya nyumbani na ligi maarufu za epl na uefa.

Dstv impoteza ubora alafu bado ni very expensive, haijalishi hata ukiweka kifurushi cha juu, utaambulia vitu vya ajabu, muvi za kujirudia rudia, angalau hata hii mbc ya azam unapata muvi za awali ila hadimu na kutojirudia.
Mjinga wa mwisho wewe. Kwa kuwa umekulia uswahilini huko unataka na sisi tuwe na uswahili kama azam. pambaf
 
Kuna tofauti kati ya kufanya production na broadcasting (kuonyesha).

Production ni kuzalisha, yani kupeleka vifaa na wataalamu kwa ajili ya kuzalisha hicho kinachoonekana kwenye tv.

Broadcasting ni kuonyesha tuu na sio lazima kufanya uzalishaji.

Kwenye kombe la dunia lililopita, TBC alifanya broadcasting (kuonyesha) tuu.

Kwenye ligi ya Tz, azam anafanya zote mbili yani production na broadcasting, yani anapeleka wataalamu kwa ajili ya mechi (production) na pia yeye azam anaonyesha (broadcasting) hizo mechi.

Kitakachofanyika ikiwa kama atapata kibali cha kuonyesha EPL au UEFA, Azam yeye atafanya broadcasting (kuonyesha tuu) kama alivyokuwa anafanya TBC kwenye kombe la dunia na sio kufanya uzalishaji. Hapa hakuna cha kusema ety azam ana camera mbovu wala mitambo mibovu ila kinachotakiwa ni kuonyesha hizo mechi kwa HD tuu na hata hvy channel zote 9 za azam tv ni HD.

Kwahy ishu ni pesa tuu ili kupewa hicho kibali, ila kwa kuwa azam anaonyesha tamthilia za kibongo bc watu wanaichukulia poa ila azam tv n kampuni kubwa mno hapa Afrika.
Hili somo nilitaka kuwapatia wadau hapo juu waliouliza kuhusu Azam ana camera mbovu n.k

Nadhani hapa umewaelewesha kitaalamu na wataelewa.
 
Kuna muda mnamkandia kuwa ana camera mbofu, channel zake hazina picha kiwango cha HD. Kuna muda DSTV anasifiwa kweli kweli. Utasikia wengine wanasema kama azam asingekuwa na kibali cha kuonyesha ligi yetu, ningetupa king'amuzi. Sasa hapa wewe unasema kuwa kama Azam akipata kibali cha kuonyesha epl na uefa, DSTV kwisha.
Mnatuchanganya sisi wenye startimes mjue. Hebu kuweni na msimamo, azam na dstv nani mkali na sisi tuhamie huko.
Ni aibu sana kulinganisha DSTV (dude kuuubwa) na Azam.
 
Kuchezesha timu saa nane mchana na jua kali,,lakini simba na yanga hazijawahi kucheza mechi saa nane
Dah kazi ipo 😂 tena kazi ipo kubwa sana 😂

Kwahy umesema azam ndo anapanga ratiba, mechi zichezwe saa ngapi 😂
 
Amini kuna watu hawajaelewa kwa sababu wameamua kutokuelewa.
Serious? Basi waambie hivi.

hao DSTV wanapokuwa wanaonyesha mfano UEFA au EPL haimaanishi wamepeleka camera zao ulaya kwenda ku record (produce) hiyo match ndio sisi wateja wao tuone bali ni kwamba wao wananunua matangazo kutoka TNT sports,BBC au Amazon
 
Dah kazi ipo 😂 tena kazi ipo kubwa sana 😂

Kwahy umesema azam ndo anapanga ratiba, mechi zichezwe saa ngapi 😂
Kama sehemu ya mdhamini lazima aone haki kwa timu zote zinafuatwa,,,
 
Kuchezesha timu saa nane mchana na jua kali,,lakini simba na yanga hazijawahi kucheza mechi saa nane
Broadcasters huwa wana makubaliano na ligi husika kuhusu ratiba za mechi na wanashirikiana ku schedule tarehe na muda wa mechi kulingana na mahitaji ya mechi husika. Kuna factors nyingi zinazo determine mechi ichezwe lini na saangapi zikiwemo za kiusalama, hali ya hewa, broadcasting, shughuli za kijamii/kiserikali n.k

Hivi unajua kuwa mechi za mapema za EPL siku ya Jumamosi ambazo huku huwa tunaziangalia kuanzia saa 9 mpaka saa 12 jioni kule Uingereza huwa hazirushi kwenye TV tokea kuanza kwa EPL 1992? Hii iliwekwa ili kulinda mahudhurio viwanjani ku boost mapato ya vllabu.

So unaona factors kama hizo? Najua nimekuchanganyia mambo mengi lakini najua pia itakusaidia kuelewa kwa nini mechi fulani ichezwa mda fulani na nyingine mda fulani siku fulani.
 
Jamaa anakuambia azam ndo wanatoa kibali 😂
Umenielewa vibaya sijasema Kwamba Azam ndiye anayetoa kibali.
Ila nilichomaanisha ni Kuwa Kwa Sasa aliyepewa kibali cha kuonesha League kuu Kwa Sasa ni AZAM.

Swali lako lilikuwa Kwamba "Leo", na Mimi nikakujibu Kwa Leo haitowezekana Kwa kuwa AZAM ndiye aliyenakibali, alichopewa Kwa mkataba na Makubaliano maalumu ambayo Anayatekeleza.

Ni Sawa na kuuliza feisali Leo feisali ukimtaka Leo, unaenda kuonana na Meneja wake mnamalizana ama Team aliyopo ambayo ndiye mwenye mkataba naye? Jibu ni TEAM.

Huwezi kwenda kuonana na TFF Kwa Leo ili Hali mwenye leseni hiyo Yuko Kazini Kwa Makubaliano na mikataba ya Maandishi. Lakini swala la kuvunja mkataba na Kununua hati miliki unaweza kulifanya Kwa kuonana na mwenye hati na leseni hiyo Kwa wakati huo.

Kwa mujibu Wa Sheria za Tanzania mmiliki WA hati ya Kiwanja ama eneo husika ni Serikali, aliyenunua eneo Hilo ni Mkodishaji Kwa Serikali Kwa muda Wa Miaka 99. Lakini Je, mbona Mimi nikikitaka Kiwanja hicho siendi kukinunua Kwa Serikali na badala Yake ninaenda kwa ambaye amekodishiwa? Na Makubaliano hayo pia yataheshimika na Serikali pia ambaye ndiye mmiliki.

Sijui tutaelewana hapa!!.
 
Usifananishe dstv na hiyo takataka, na mitamthilia yenu ya kutafsili
 
Kutokana na facts Fulani Fulani, na mambo mengineyo ya kibiashara, na mambo ya mzawa as first priority na Ushirika na ubia alionao AZAM Na Serikali Kwa mambo mengi.
Ni Ngumu Serikali kumnyanga hati miliki ya Maudhui hayo AZAM na kumpa DSTV.
Hili Hali AZAM anahiitaji hiyo biashara na hayuko teyari kuvunja mkataba na Yuko teyari Kurenew mkataba wake.

Na Kwa Sisi watanzania ni Heri AZM hasinganganywe hiyo hati miliki na Kupewa DSTV. Kwa maana hati miliki alipewa DSTV Tutakuwa tunalipia gharama kubwa kufuatilia ligi kuu Kwa kulipia vifurushi Kwa fedha ambayo Kwa Azam ni kitonga kwetu.
 
Serious? Basi waambie hivi.

hao DSTV wanapokuwa wanaonyesha mfano UEFA au EPL haimaanishi wamepeleka camera zao ulaya kwenda ku record (produce) hiyo match ndio sisi wateja wao tuone bali ni kwamba wao wananunua matangazo kutoka TNT sports,BBC au Amazon
Yah upo sahihi mkuu, watu wakiangalia mechi kwenye supersports/dstv wanadhani wao ndio wanaofanya production za hizo mechi kumbe nao pia wanapewa feed (video) kama ambavyo azam anapewa feed (video) za mechi za Laliga na Bundesliga.
Mfano EPL kuna makampuni kama matano hv ndo yanafanya production ikiwemo TNT, SKY SPORTS n.k ila Supersport/dstv anaonyesha tuu na hakuna mechi hata moja aliwahi kufanya production.

Kutokana na facts Fulani Fulani, na mambo mengineyo ya kibiashara, na mambo ya mzawa as first priority na Ushirika na ubia alionao AZAM Na Serikali Kwa mambo mengi.
Ni Ngumu Serikali kumnyanga hati miliki ya Maudhui hayo AZAM na kumpa DSTV.
Hili Hali AZAM anahiitaji hiyo biashara na hayuko teyari kuvunja mkataba na Yuko teyari Kurenew mkataba wake.

Na Kwa Sisi watanzania ni Heri AZM hasinganganywe hiyo hati miliki na Kupewa DSTV. Kwa maana hati miliki alipewa DSTV Tutakuwa tunalipia gharama kubwa kufuatilia ligi kuu Kwa kulipia vifurushi Kwa fedha ambayo Kwa Azam ni kitonga kwetu.

Wabongo wengi wanaichukulia simple azam TV kisa tuu wanaonyesha tamthilia, lkn azam TV n kampuni kubwa grade one kwenye rates za CAF, na ndio mana mechi zote za CAF zinazochezwa Tanzania zinafanyiwa production na azam TV.

Kwenye ufunguzi wa AFL ile mpaka rais wa FIFA alikuja Tz, ile production imefanywa na azam TV japokuwa kulikuwa na baadhi ya watu kutoka kwenye kampuni iliyokuwa na haki ya kufanya production ya mechi za AFL, pia official broadcaster ilikuwa ni kampuni kutoka France, ila production nzima ilifanywa na azam tv na mechi zote za CAF zinazofanyikia Tz bc azam ndo anafanya production.

Sasa mbongo kisa anaona tamthilia ambazo yeye hazipendi bc anaiona azam ni kituko.
 
Ligi Kuu tu hapa imewashinda. EPl wataweza
Kwa kisimbusi chao isije ikatokea..kibovu chama cha quality ya chini.
Kwa taarifa yako hawawezi kupata mkuu. Yan azam ipo nchi maskini watu hawamudu hata kulipia vifurushi
Azam hela gani anaweza kutokuwanayo? Hebu kuwa na heshima bro! Labda iwe kupata hicho kibali lakini siyo pesa!
Huu wimbo unahitaji remix sasa!! Kila siku story ni hizi hizi, EPL rights sio ndondo cup kwamba kila mtu anaweza kununua
Hela ya kuipata hiyo leseni ya kuonesha hizo mechi kutoka kwenye mashindano, na ligi ghali kabisa duniani; wanayo?
Azam TV kupitia channel yake ya Utv, kila jumamosi wanaonyesha mechi moja ya EPL, haya nipeni utofauti wa hiyo mechi ikionyeshwa Supersport VS azam
 
Back
Top Bottom