Azam akipata leseni ya kuonesha EPL na UEFA, hawa DSTV kwisha habari yao

KwaninI unasema Dstv siyo Supersport?
Hili nalo ni tatizo lenu wabongo, tukisema azam ina Channels jumla 9 wataanza kubisha mana zingine hazitumii jina la azam.

Supersport kwenye dstv ni sawa na TBC kuwepo kwenye dstv.
 
Ligi Kuu tu hapa imewashinda. EPl wataweza

Kwa ligi kuu inakuwa ngumu kwa kuwa production, urushaji na usimamizi wa matangazo anafanya yeye Azam...

EPL ni kurusha tu...
 
Dah 😂
Cha msingi main point umeipata
 
Azam hawez hata siku Moja kuonyesha EPl aendelee na huto tumechi twenu za kichawi chawi
 
Kwa ligi kuu inakuwa ngumu kwa kuwa production, urushaji na usimamizi wa matangazo anafanya yeye Azam...

EPL ni kurusha tu...
Ccm wab0reshe kwanza viwanja ndipo azam wawekeze nguvu kubwa ya production kwenye viwanja bora
 
Kama isivyowezekana kwa Dstv kupata haki za matangazo ya ligi kuu ya Tanzania ndivyo isivyowezekana kwa Azam tv kupata haki za kuonyesha ligi kuu ya England na Uefa,,
 
dstv inaenda kununuliwa na canal+ huenda ikabadilika hivi karibuni
 
Hawawezi kupata, hawakawii kutoonyesha mechi live pale kunapukuwa na tukio kubwa la dini na kuonyesha lenyewe iliwahi kutoka mechi wanazoonyesha kupitia zbc2
Kwani Zbc2 ni Mali ya Azam ?
 
Kama kuna watu hufikiria hivyo basi ni wapumbavu wa hali ya juu aisee!
 
Aisee kumbe ndo watu wanaonaga hivyo 🤣
Azam inapendwa kwasababu ya garama zake unaweza lipia hata kwa siku,lakini pia uswahilini kwakua kuna michezo ya waturuki/Tamthiria zilizotafsiriwa/kuna hizo Sinema zetu.
KUna wapenzi wa mpira pia ligi kuu!
Mimi sioni sababu ya kujumlisha jamii nzima kwakua kuna mtu anachukua labda Azam kwa ajili ya Ligi kuu tu wala haangalii chochote kingine! Mwingine kwa ajili ya hizo sinema!
Ndivyo hivyo hivyo pia kwa Dstv kuna watu huchukua kwa ajili ya ligi za ulaya/Movie
Mana michezo ya dstv Maisha magic kiukweli hainaga uhalisia. Ila yote kwa yote Dstv wangeshuka kwenye level ya azam katika kujali kipato cha mswahili basi wala usingesema Azam ni ya uswazi
 
Azam hela gani anaweza kutokuwanayo? Hebu kuwa na heshima bro! Labda iwe kupata hicho kibali lakini siyo pesa!
Hela ya kufanya broadcast ya EPL anaweza kuwa nayo ila kumbuka hiyo ni biashara, anategemea irudi na Must lazima vifurushi vipande. Stress ya azam ni kushindwa kurudisha hela watakayo jumulia leseni kutoka EPL na pia hofu ya kupoteza wateja kutokana na kupanda kwa vifurushi. Hila kwa ufupi wanaweza 👊😁
 
Nchi za kusini mwa janga la sahara ni masikini mno hamna uwezo wa kulipia vifurushi......wakati wew unaona dstv vifurushi vyao ni ghali wenzio wanatengeneza hasara tu kwa kushusha gharama ya vifurushi vyao
 
Azam bado sana kwanza watangazaji wake asilimia kubwa wapo kishabiki halafu vifurushi vyake havilelewi ukilala ukiamka vinabadilika kila mara. Watatuletea Othman Kazi ambaye anaona anafahamu kila kitu cha urefa husu alikimbizwa. Azam wabaki hivi hivi na tamthilia tumezipenda ila kwenye mpira wa nje hapana acha DSTV ndiyo kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…