Azam FC yamtambulisha FEI TOTO, asaini mkataba wa miaka mitatu, afafanua fedha alizochangiwa na wadau

Azam FC yamtambulisha FEI TOTO, asaini mkataba wa miaka mitatu, afafanua fedha alizochangiwa na wadau



Mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa #AzamFC, Feisal Salum (Fei Toto) amesema fedha ambazo alichangiwa wakati wa sakata lake la kimkataba dhidi ya #Yanga, atazipeleka Msikitini, Kanisani na kwa Watoto Yatima.

“Namshukuru Rais Samia kwa kulimaliza hili jambo, nawashukuru viongozi wa Yanga na mashabiki wake, pia kuhusu zile fedha ambazo nilichangiwa siwezi kuzirudisha kwa waliotuma kwa kuwa siwafahamu hivyo nitapeleka kwa watu wenye uhitaji.”

Mara baada ya kutambulishwa Fei Toto na kusaini mkataba wa miaka mitatu, amekabidhiwa jezi namba 6 ambayo atakuwa anaivaa akiwa Azam FC
IMG-20230608-WA0065.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye Utopolo Wameupyata Mkia. Ubwabwa na Juice ya Ikulu imewaponza.
 
Azam fc nilikuwa nawapa sana credit. Ila kwa uhuni walioufanya kwa huyu dogo na pia kwa klabu ya Yanga; hakika nimewadharau sana.

Maana wangetumia njia kama hii ya mazungumzo, wala huyu dogo asingekaa miezi 6 nje ya uwanja.
 
Kwa hiyo yanga hizi akili walikua hawana..mpaka waambiwe....na kupewa instructions na mama???Yaani mpaka wasemwe kama watoto...
Hongera kwake Fei...kapigania alichoona kinafaa kwa utashi wake...angekuwa ni nidhamu ya uwoga na unafiki angebaki analalamika tu...bila chochote.Bila shaka hakujua wapi atatokea....
 
Akiwa Azam ataitwa, Feisal salum ibn Al abdallah Al rahman.

akiwa yanga ataitwa, fei Toto. 😄😄😄😄😄
 
Kikubwa asome vyema mkataba ikiwezekana wauandike kwa kipemba asome mstari kwa mstari...
Fei anajua kusoma basi. Kama KKK tu ya shule ya msingi aliambulia sifuri kila somo, ndiyo aweze kuusoma na kuuelewa mkataba ulioandikwa na mwanasheria msomi?
 
Azam fc nilikuwa nawapa sana credit. Ila kwa uhuni walioufanya kwa huyu dogo na pia kwa klabu ya Yanga; hakika nimewadharau sana.

Maana wangetumia njia kama hii ya mazungumzo, wala huyu dogo asingekaa miezi 6 nje ya uwanja.
Mmewaita Azam ili ionekane mme mmuza akat ametoka km vile akivyotakaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Eti dau haliwekwi wazi, ni 112M woiiiiiiii
 
Back
Top Bottom