Kuna siku niliandika hapa mara tu baada ya mandonga kupigwa pambano la kwanza na kupata umaarufu yanga walimchukua awe icon yao pia.Sisi wapenzi halisi wa ngumi tunachukizwa na Upuuzi na dharau ambazo wanazifanya Azam katika mchezo wa Ngumi. Huu si mchezo wa Maigizo. Mtakuja sababisha mtu adhurike au afe ulingoni.
Lakini pia hiyo tabia kuna watu wataacha kabisa kufuatilia mchezo wa ngumi. Sababu inaonekana kabisa mnamtengeneza Mandonga kwa kudhani mna upromote mchezo. Kumbe mnaua mchezo. Muulizeni Liquid.. yu wapi sasa? Watu watafikia hatua watadharau kila kitu.
Huu ni mchezo serious ufanyeni uwe serious please. Msilete maigizo kwenye mchezo wa ngumi. Si tayali mnazo tamthiliya nyingi tu? Zinatosha. Mchezo huu upeni heshima yake watu tutaupenda.
Nilisema kwa vile hawa utopolo wameamchukua ili watafute sifa kama ilivyo kawaida yao,ataanza kushinda kimchongo mchongo na kweli pambano lililofuata alishinda kimchongo mchongo.
Pambano hili,ni la mchongo ule ule.Gsm abakize haya mambo kwenye mpira huku mtu atauliwa siku moja