AzamTv wametudanganya kuhusu kuonesha michuano ya Euro

AzamTv wametudanganya kuhusu kuonesha michuano ya Euro

AzamTv walitangaza kwa mbwembwe watarusha michuano ya Uefa Euro. Cha kushangaza jana hamna mechi waliyoonyesha.

Na leo mpaka sasa hakuna mechi wameonyesha. Nawauliza nyie Azam Tv utapeli mtaacha lini?

Au Euro ishaisha??

Anyway, imebidi nilipie DStv tu
Mbona mechi ziko live ZBC2 ambayo ipo kwenye decoder ya Azam. Au lazima uzione Azam sports?
 
Lipia DSTV acha ubahiri ata kifurushi cha buku 10.
 
nawashangaa sana watu wanaotumia azam tv kwanza hakuna kitu sipendi kama maigizo yaliotafsiriwa.... tumieni dstv mbali na hapo bora uweke bundle lako uzame jf
 
Sasa kuna shida gani akirusha mechi za simba na yanga tu, na kuna ulazima gani wa kurusha mechi ndogo ambazo hazina watazamaji wengi, au sheria ndio zinataka hivyo kwamba ukichagua ligi fulani basi ni lazima urushe mechi zote za hiyo ligi
Huwa unatazama Everton Vs Norwich? Au Parma Vs Empoli? Basi zote zinaoneshwa tu.

Kuangalia Simba na Yanga matokeo yake siku wakipigwa na Prisons mashabiki wanakua kama wehu hawaamini. Ila kwa mpenzi wa soka anaepata kuwatazama hata mara moja moja hashtushwi na matokeo ya aina hiyo.

Kingine inasaidia kuzitangaza timu nyingine kitaifa na kimataifa. Hapo Kenya saizi hadi Mtibwa Sugar wanawajua.
 
Duuh kumbe dstv kifurushi cha elfu kumi tu, mnaangalia mechi za ulaya na hamsemi, ni channel gani hiyo
Sijui ni kwanini sehemu nyingine wamewapa rights TV za kulipia kama DSTV. Europe haya mashindano yanaonyeshwa kwenye TV za bure kama kombe la dunia linavyoonyeshwa. Taznania hii michuano ilitakiwa kuonyeshwa na TV ya Taifa.
 
Huwa unatazama Everton Vs Norwich? Au Parma Vs Empoli? Basi zote zinaoneshwa tu.

Kuangalia Simba na Yanga matokeo yake siku wakipigwa na Prisons mashabiki wanakua kama wehu hawaamini. Ila kwa mpenzi wa soka anaepata kuwatazama hata mara moja moja hashtushwi na matokeo ya aina hiyo.

Kingine inasaidia kuzitangaza timu nyingine kitaifa na kimataifa. Hapo Kenya saizi hadi Mtibwa Sugar wanawajua.
Oohh nimekuelewa mkuu ila swali langu ni kwamba kwanini wasiwaruhusu wote dstv na azam kuonesha hizo mechi kwa kadiri kila mmoja anavyotaka, halafu wangeacha wateja wenyewe ndio wachague kwani cha muhimu si ni kodi tu au, ndio nikauliza au sheria za bongo haziruhusu kisimbuzi zaidi ya kimoja kurusha mechi za ligi ya hapa
 
Sijui ni kwanini sehemu nyingine wamewapa rights TV za kulipia kama DSTV. Europe haya mashindano yanaonyeshwa kwenye TV za bure kama kombe la dunia linavyoonyeshwa. Taznania hii michuano ilitakiwa kuonyeshwa na TV ya Taifa.
Mkuu ngozi nyeusi tuna shida sana, hapo unakuta ndio hivyo kulindiana maslahi tu, ili serikali ipate kodi
 
Mkuu Hamia DSTV tena kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh elfu Kumi tuu unatazama mechi zote 54 LIVE HD kwa

DSTV leseni ni Dola mil 600 kwa msimu...yale ni maji marefu mkuu....watu hawajiulizi kwanini Middle East yote na Pesa yao ya mafuta ni BEIN sports pekee ndiyo wanaonesha Premier League na UEFA champions league....
Huko Dstv quality yao ya matangazo iko poor
 
Back
Top Bottom