#COVID19 Azim Dewji amvaa Gwajima sakata la chanjo, amwambia ana akili ya kuhubiri siyo Sayansi

#COVID19 Azim Dewji amvaa Gwajima sakata la chanjo, amwambia ana akili ya kuhubiri siyo Sayansi

Badoo sijashawishika kabisa nendeni mkachanjwee wenyewee mnaotakaa usilazimishe mtu kwanzaa serikali si ishasema kuchoma ni ihari sioni tatizo ngoja mkishachanja si tutakujaga kuchanja miaka mitano mbelee
 
Yeye anaongea kama nani kwenye nchi hii huyo dewji
 
Azim anamjibu Josephat.

Hee.....

Imegeuka vita vya kiimani??

Kwamba administration ikiwa hivi basi watu wa hivyo watetee tu kila kitu??

Hivi akili zetu tunazihifadhi wapi sisi??
 
Hao wanawaambiaga watu wasinywe SRV afu wao wanakula kwa siri.
 
Biolojia ya wapi hii....
Hata biology ya form two haisemi hivi, KAZI YA CHANJO NI KUPUNGUZA KWENDA KWENYE ATHARI MBAYA UKIWA UMEPATA MAAMBUKIZI,..........
usipotoshe walio soma Historia, hakuna kitu kama hichi duniani.
Duuh😲🤣🤣
 
Azim Dewji: Tunasema kwamba, kazi kubwa ya mkuu wa Dini ni kuongoza waumini wake sio kuwapotosha, unazungumza maneno ya kuwapotosha waumini na kuleta taharuki kwenye Jamii, hiyo haifai kabisa na isiendelee kufanyika hivyo, sisi hatutakubali.

Kwa njia moja au nyingine unawatukana waliobobea kwenye fani hiyo kwamba kamati iliundwa, waliofanya utafiti wewe unawaona hawana akili. Saa nyingine naweza kusema labda wewe ndio huna akili ya sayansi, wewe labda una akili ya kuhubiri peke yake kwa hiyo usijaribu kuwatukana wenzako.

Mwisho Azim amemwambia mchungaji Gwajima amuheshimu Rais na kiongozi wa chama ambacho kimemlea na kumpatia ubunge kwani bila chama cha CCM asingepata ubunge na wengine kama yeye hajampigia kura Gwajima bali alipigia chama.

PIA, Soma> Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama


Mungu ELOHIM ni mkuu kuliko hiyo saysansi unayoibabudu bila hata kuijua dewji. Ishia basi!
 
Hahahaha Nchi imekuwa na miruzi miiingi sana siku hizi toka amekufa yule jamaa yetu mwamba, siku hizi kila mtu kambale mamba...
 
Nilichojifunza, Watanzania ni moja ya jamii wajuaji saaana duniani halafu mwisho wa siku tunabaki wapumbavu na wamwisho..

Kenya, Uganda na Rwanda wamechanjana wala hakukuwa na kelele, chanjo imekuja Tanzania dah nongwa na miruzi imekuwa mingi hatari....

Tuacheni ujuaji, waliochanjwa duniani wote mazuzu hawana akili bali watanzania ndio watu wenye akili....tupeni basi solution ya Corona watu wasife wala kuugua mnaleta blah blah..
 
Ila anaweza sema alikua anaongea kama mbunge na sio mchungaji.

Mbunge hana madaraka ya kusema alichosema, yeye ana position ipi kusemea Covid-19 kuwaambia watu wasichome. Who is he? Mkuu wa nchi kashalisema vema sana kuhusu Covid-19. Ni hiari yako kuchanja, sasa Gwajima anatisha watu who is he? Ni kumfukuza huyu CCM haraka sana.
 
Mwanzo walisema chanjo ije mwenye kutaka kuchanjwa na achanje na asiyetaka apite hivii, leo imekuja mnataka mtulazimishe wote kuchanjwa.
 
Back
Top Bottom