Uchaguzi 2020 Azimio: Bunge la Marekani laisihi Serikali ya Tanzania na wahusika wote kuhakikisha Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

Acha upumbavu wewe! Kwahiyo unaweza kumuua mtoto wako huku jamii ikikuacha tu kwakuwa ni mtoto wako? Hiki ndicho polepole kawatuma kuja kutetea ujinga?
 
Watanzania wakisema huwa hamuwasikii mnawateka, ngoja waseme wanaume labda mtawasikia.
 
Magu ameanza kuwekwa kwenye target na sasa ni suala la muda tu kwani marekani wanamchukulia kama mtu anayehatarisha maslahi ya nchi yao. Pia amewekwa kwenye kundi la akina Libya, Venezuela, Iraq nk. Kuna jambo kubwa linajiunda hapa nafikiri kama magu ni msikivu basi aschukulie mashara lakini navyomjua atadharau na mguu utaota tense.
 
@fazili

Lazima ujue hakuna heshima utakayogawiwa tu.. heshima inachukuliwa.

Na nchi zote zilizoamua kujisimamia kwao Ni threat.. ushawahi kujiuliza ikiwa kila nchi itaruhusiwa kujisimamia kwa uhuru uchumi wa mabeberu unakuwa katika hali gani!?

Hii haitakuwa laini, wala nyepesi but the end is worth it.
 
Magufuli alishalisemea hili muda mrefu na akarudia na kusisitiza kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki. Sasa marekani Wana Nini kipya?
Haiishii kwenye kulisemea magufuli haonyeshi kwa vitendo kuwa muumini wa anachokisema hebu fikiria mfano huu : mnaenda kuchukua fomu wewe na opponent wako halafu siku ya kurudisha fomu unatuma watu wako wamteke mpinzani wako ili asirudishe fomu kwa wakati. Ukisharudisha wewe yule opponent wako anapatikana akiwa nusu mauti halafu wewe unatangazwa umepita bila kupingwa je siasa hizi za kimafia ndio mnamsifu Nazo magufuli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…