Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Mchambuzi,
Mkuuwangu nimekuwa nakufuatilia sana kwa muda na naona unashusha vigongo vizuri sana ambavyo sisi wana Chadema ndio tunaviamini, sasa nashangaa sana unaposema unatatizwa na Itikadi ya Chadema ilihali mambo mengi ya Azimio la Arusha tunayasisitiza na isitoshe ktk uwajibikaji maswala ya Zakumi ndiyo yatakuwa kipimo cha uongozi. Mimi nadhani darasa hili lina mazuri yake na pengine William kaiweka mada hii bila kujua itatufikisha wapi ama alikusudia kuona tofauti zetu ktk mjadala mzito kama huu. Na nakuhakikishia mawazo yako yanaweza tu kupokelewa Chadema maana ndio chama pekee kinachosisitiza DIRA kwanza (wazo langu) na UWAJIBIKAJI Zakumi). Hawa wanaopinga Miiko na maadili wamejaa huko uliko na sii ajabu William anatetea mawazo baada ya kulishwa sumu hii.
 
Last edited by a moderator:

Dear my friend enemy.......!!!

hapo kwenye red ndipo ambapo ulipomaliza kila kitu kwenye hii thread!!

Nyerere alitaka kila mmoja awe mcha Mungu, muadilifu na walipoharibu alijitahidi kuwabadilisha kwa kuwatoa shirika moja na kwenda jingine...hapa Nyerere anaonekana au alifanyika kama PRIEST, PADRE au sheikh!

Utawala wa sheria ungekuwa implemented tangu kipindi kile leo tungekuwa mbali sana,

tusingesikia mawaziri wanafanya haya na bado wanadunda mtaani

Azimio la Arusha ni IMANI!! NI AGREEMENTS...NI MOTO

Lakini katu azimio la rausha haliwezi kubadilisha tabia ya WATU, haliwezi kumbadilisha fisadi asiwe fisadi, halina NGUVU HIYO..HALINA UWEZO HUO

Sheria ndiyo kila kitu!!! nashangaa baadhi ya watu hawapigi kelele kwa nini watu hawaendi jela....!!!!

The AA was just wrong if not idiotic idea!! halikuwa na meno wala nguvu yeyote...

Taifa haliendi hivyo...kwa Nyerere prisons was meant kwa watu wa hali ya chini na sio viongozi
 

Mkuu wangu Mkandara,

Upo sahihi kwani kama mtu ukiamua kuangalia maslahi ya taifa hili, hakuna taasisi ya kisiasa iliyopo mstari wa mbele hivi sasa zaidi ya Chadema. Kadri siku zinavyozidi kwenda, Chadema wanazidi kubaini maeneo ambayo yatakisaidia kama chama kupewa imani ya muda mreru na umma iwapo kitafanikiwa kushika madaraka ya nchi hii, kwa mfano kupunguza kasi ya kupingana na ufisadi majukwaani na badala yake kuhakikisha kwamba mchakato wa katiba mpaya ambao ni dhahiri Chadema ndio walio ushinikiza, unaingiza masuala ambayo ndiyo yatatupatia viongozi bora, wenye uzalendo, uwajibikaji na uadilifu kwa taifa lao. Na mengi ya haya yapo katika azimio la arusha na inatia sana moyo kuona hata wanachadema wengi wanaliona Azimio la Arusha kama suala lisilo partisan. Msimamo na mtazamo huu ni muhimu sana kwa maendeleo na mafanikio ya Chadema.

Pamoja na uanachama wangu wa CCM, binafsi nakubaliana na Chadema katika maeneo mengi sana,kuanzia umuhimu wa kuheshimu nguvu ya umma, umuhimu wa kuharakisha mabadiliko nchini kwetu kabla hali haijawa mbaya zaidi, na ukweli kwamba CCM kama chama kimefilisika kifikra. ili mradi nina uwezo wa kusema yote haya hivi sasa, sioni kama nitafanya tofauti na haya nikiwa mwanachama wa chama kingine cha siasa. Lakini ikitokea kwamba kama mwanachama wa CCM ninapata vikwazo kujadili mambo ya msingi kwa maslahi ya taifa letu, nitakuwa tayari kusikiliza ushauri utakaonisaidia kuondokanana vikwazo hivyo, ikiwa ni pamoja na kuhamia chama kingine cha siasa, especially Chadema au CCK. Vinginevyo sina uzoefu wowote wa kiuongozi katika siasa za Tanzania, zaidi ya kuwa mwanachama wa kawaida wa CCM kwa miaka 18 sasa ninaelipenda taifa langu na nilyekuwa tayari kulilinda, na bado sijapata kipingamizi cha aina yoyote cha kunizuia kusema kweli na pia kuweka maslahi ya taifa letu mbele ya maslahi ya CCM, hata kama ni kukubaliana kimsingi na wanachama wa vyama vingine vya siasa, hasa Chadema na CCK
 

Mkuu Waberoya. Vyema.

Kama umefuatilia mjadala huu, mkuu Mchambuzi alitoa pendekezo kidogo kwamba mjadala huu uwe katika misingi ya NIA,MCHAKATO na MATOKEO ya azimio. Ila mzee W. J. Malecela naona bado yupo katika misingi 2 ya mwisho. Kama nia ni kujadili azimio kwa malengo ya kusaidia taifa letu,ni vyema kujadili pia suala la NIA ya azimio.

Kwani mjadala wa NIA ndiyo utaweza kuonyesha wapi tulikosea kama taifa ili tuparekebishe na wapi tulipatia basi tupaboreshe zaidi.

Sasa kwenye hoja yako ya azimio kukosa nguvu wala uwezo kama wa kisheria,mkuu unaonaje sasa kama katika kipindi hiki,tukitumia baadhi ya misingi mizuri ya azimio katika mjadala wa katiba mpya? Tukiweza kuweka hiyo misingi katika katiba,ambayo ni sheria mama,tutakuwa by default tuipa nguvu na meno misingi ya azimio ambayo haikuwa na meno.
 
Last edited by a moderator:

ha ha ha!! Z10 nimekukubali

waeleze hao ndugu wapendwa kuwa Miiko na maadili havifundishwi ukubwani!!

Afadhali AA lingekuwa ni somo la maadili kwa wanafunzi wa shule za msingi...kufundishwa uraia mwema, maadili na miiko....maana kila mtu ni kiongozi ati!

Tabia hii ya kipi kianze na kiwekwe wapi ndio quality ya kiongozi, kwa mfano kuna vitu vilitakiwa vifundishwe tangu utotoni!1

1. Usimamizi na utunzaji wa mazingira yetu' vitu kama Enviornmental impact assessment ni kitu ambacho kila mtu anapswa kujua.......mfano mtu kutupa chupa ya maji hovyo...ni tatizo la malezi

2. customer care na usimamizi wa biashara; ni vitu vinapaswa kufundishwa kuanzia utotoni.....

3. maadili na miiko ( ambayo itaunganisha wananchi na kujenga uzalendo) knyume na hapo ndio unapata AA la nyerere au semina chakavu za ngurdoto!! what a shame

Tuna tatizo la msingi sana la kitaifa
 

Nia ilikuwa nzuri lakini wrong timing to wrong people

maadili na miiko inatakiwa kufundishwa kuanzia utotoni!

ukubwani ni sheria tu inachukua mkondo wake! kufanya AA kuwa ni dira was totally wrong!

nashukuru umekubali kuwa lilikuwa halina meno......sheria ni meno, katiba ni dira..what else do you need here?? why are u busy trying to modify something which was not supposed to exist in the first place

AA ndio inafanya leo hii mawaziri wasiende jela...AA limejenga utamaduni huo...maana kama ingekuwa kwenda prison, asingebaki waziri, wakurugenzi, makamishna........it has been culture to leave criminals leaders free!!

watu wanaogopa kuwashtaki akina mkapa, lowassa, chenge, n.k simply kwa sababu tangu enzi hizo si kawaida kuwashtaki na kuwafunga viongozi

ninachosema ni kuwa msingi wa taifa ili ulitakiwa uwe kwenye sheria!! tungejengwa hivyo viongozi leo wasingekuwa na guts za kuiba hivi........AA liliweka msingi huu wa kuwaona viongozi malaika (always innocent)

unless mtu aseme under AA viongozi wangapi walienda jela baada ya tamko....au mwingine aseme hakukuwa na ufisadi kipindi hicho??
 
Paragraph ya mwisho mkuu wangu umeniacha nje kidogo, Ikiwa leo upo CCM miaka 18 na ushauri wako haujafanyiwa kazi isipokuwa chama kinazidi kwenda nje unafikiri ni lini watakusikiliza maana nijuavyo kumsikiliza mtu haina maana kupewa tu nafasi usikike kisha chama kiendelee na fikra zake. Hata unapompa mtu ushauri sii muhimu yeye akusikilize bali afanye ulomshauri. Lakini akifanya kinyume lazima ujitenge na vitendo vile na sio tena kutafuta uwakili wa hoja ambayo wewe unapingana nayo.

Labda nikukumbushe tu kwamba sisi wote tulikuwa CCM na binafsi yangu nilijiunga chama hicho toka mwaka 1973 nikiwa sekondary japokuwa CCM jina. Lakini baada ya kuona chama kinapoteza mwelekeo (dira) na hasa baada ya kipindi cha pili cha Mkapa nilishawishika hii sii dini niitakayo wala mafundisho yake hayalengi uokovu bali kunipoteza, hivyo sikuona sababu kabisa ya kutembea na msalaba kifuani ilihali sikubaliani na mafundisho yake, nikahama japokuwa kwa uchungu mkubwa sana.

Mtu unaingia chama kwa sababu unakubaliana na itikadi zake, sera zinaweza badilika kulingana na umuhimu wa mahitaji (priorities) wakati muafaka, lakini kama chama kinahalalisha ufisadi, sidhani kama yote uloandika yatawezekana. Binafsi yangu siamini kabisa kwamba unaweza kulijaza pakacha linalovuja hata utumie uangalifu wa aina gani. Ziba ufa kabla hujajenga ukuta hii ndio imani yangu na kutetea zaidi kupiga vita Ufisadi ambao sii Ufa tu bali mirija inayonyonya nguvu zote za wananchi kuhamishia kwa watu wachache. Tunachokiona leo ni maendeleo ya vitu na sii ya watu jambo ambalo linaturudisha ktk utumwa. Karibu Chadema mkuu wangu usipoteze muda wako wakati ni huu.
 

- Mkuu huwezi kuchanganya Azimio na Sheria, huwezi kuchanganya Sheria na miiko ya uongozi, Sheria kwenye maendeleo ya taifa inasimama peke yake, ikishaingiliowa na anything else, ndio mwisho wake wa function, and then unapata mafisadi, wanaoiba lakini wanadai sheria ipo wapi?

- Sasa after all this misery ya taifa letu kwa sababu ya Azimio, bado unasema turudi kulisoma vizuri Azimio tena, please mkuu unasema wasomi wote tuliowahi kwua nao, hawakulielewa Azimio ila sisi ndio tunaweza?

- I mean unasema tujadili nia ya Azimio na huku unajua wazi kwamba Azimio limekuja baada ya Mwalimu kwenda China na kurudi akaamua hataki tena vyma vingi vya siasa, ndio akaleta hili zimwi, limetumaliza Taifa mpaka hatuelewani, waliolishanglia kwa maneno huku wanaiba wakawa ndio wapenzi wa Azimio na Mwalimu, waliolikataa wakasingiziwa majungu weee, sasa tizama mnatuambia eti ni aya Azimio ilikuwa safi no it not!

- Nia ya anything ikiwa mbaya na matokeo yatakwua mabaya pia!

William.
 

Mkuu Mkandara,

Kimsingi naelewa hoja yako, naomba muda niifanyie kazi.
 

- Sasa ninaweza kupumzika, I mean kumbe kuna na wengine wanaoamini ninavyoamini, sawa sawa Azimio was dead hata kabla hata ya kuanza!

William.
 


Mark my words again. Nostalgia is not a good guide to economic and social policies. Mjadala wa Azimio la Arusha unakuja baada ya viongozi wa sasa kushindwa katika kutimiza matumaini ya watanzania. Swali la kujiuliza je tukiwaondoa hawa viongozi wa sasa na kuwarudisha Nyerere, Kawawa, na Sokoine na kuwapa Azimio la Arusha kama guidance to economic and social policies watafanikiwa? jibu ni hapana kwa 100%.

Hata wao hili mambo fulani hili yafanyike ilibidi wawe pragmatic na kukiuka Azimio lenyewe. Kwa mfano ilibidi watu walazimishwe kwenda kwenye vijiji vya Ujamaa. Ilibidi vilevile wachukue mikopo yenye masharti magumu. Operasheni maduka ilibidi isimamishwe. Na kuna kipindi serikali ilipoteza umaarufu wake na waziri mkuu Kawawa ikabidi atolewe kafara. Na kufikia 1984 uhusiano na Kenya ukarudishwa.

Vilevile inawezekana historia ya siasa za Tanzania bado inakusumbua. Si kweli kuwa kati ya 1961-1967 Tanzania ilikuwa ni nchi ya kibepari. Mkonge ulikuwa chini ya mabepari or makabaila so to speak. Lakini uzalishaji wa mazao mengine ulikuwa chini ya wakulima. Korosho, kahawa, pamba yalikuwa ni chini ya wananchi. Hivyo tulikuwa na mixed economy. Hata Nyerere mwenyewe amelikubali na ameliandika. Na mwaka 1967 hatukwenda moja kwa moja kwenye Ujamaa na hatukuwahi kufika huku. Ukitaka kulielewa suala hili vizuri ongea na mwanazuoni Companero ambaye nimebadilishana naye mawazo kwa zaidi ya miaka saba sasa.

Kilichofanyika kuanzia mwaka 1967 ni majaribio tu ya social engineering with mixed or with disappointing results. Sababu ya kutokuwa na mafanikio ni nyingi. Miongoni mwa hizo ni ukosefu wa intellectual, human and financial capital. It's very easy to say Pesa sio Msingi wa maendeleo. However, in this age of globalization, without money you are as good as nothing.

Tatizo jingine, the leadership underestimated the complexities of the problems they were trying to solve, and also the social dynamics of the people they were trying to empower. Mtanzania masikini anapokushangilia kwa kumkemea mzungu mnyonyaji haina maana kuwa huyu masikini akipata nafasi hataacha kunyonya. Being perfect humans, we were our own stumbling block.

Kuhusiana na kuwa ujamaa ulikuwa una-deliver kuanzia 1967-1977. Hili ni suala la debate kubwa. Data zote zinaonyesha kuwa uzalishaji ulishuka kwa kiwango kikubwa wakati misaada kutoka nje na matumizi ya jamii yaliongezeka. Cha kusifia hapa ni juhudi za mwalimu. Alihakikisha kuwa misaada inatumika katika matumizi mazuri na ya jamii. Hakutumia misaada kwa manufaa yake au ya familia yake kama viongozi wengine barani Afrika.

Kwa nyinyi mnaopenda materials, mchango mkubwa wa mwalimu ni Azimio la Arusha. Kwa sababu mnaona kuwa njia moja ya kufanikiwa kwa watanzania kimaterials ni through Azimio la Arusha.

Kwa mimi ninayependa Liberty, mchango mkubwa wa mwalimu ni uhuru. Sikuhitaji Azimio la Arusha to do what I do now for living.

Cau

Z10
 
- Sasa ninaweza kupumzika, I mean kumbe kuna na wengine wanaoamini ninavyoamini, sawa sawa Azimio was dead hata kabla hata ya kuanza!

William.
Hujaelewa mkuu wangu usikurupuke. Alichosema @Wabeloya ni kwamba Dira (Azimio) anamfunzwa kwa mtu tokeo akiwa mtoto, akisha kuwa kinachofanyika ni sheria tu (msemo wa samaki mkunje akingali mbichi) maana huwezi kuwa na sheria kama hukuwa na azma. Sasa kama wewe unapingana na hata kumfunza mtoto yalikuwa makosa utaweza vipi kusimamisha hizo sheria. halafu bado hujanijibu Sheria utaisimamisha vipi ikiwa huna miiko?

Unajua mchanganya sana mambo, kwa mfano unaweza kumfunza mtoto kwa kumkataza mabaya na asipofuata ukamcharaza bakora.. tatizo linakuwa maamuzi ya kumchapa mtoto bakora, tukasema ilikuwa abuse ama sii malezi mazuri, lakini sio kupinga hata kumkata mtoto kufanya vibaya..Sasa mnapozungumzia Azimio la Arusha ni pale mnapoona bakora zinawacharaza na kusema hata hayo mafunzo yake hayana hivyo kuwekewa miiko ni makosa, hapa ndipo tusipokubaliana.
 
Sehemu kubwa ya hoja zako nimeshazijadili in one way or another na kutoa maoni yangu, kinachoendelea kwa sasa ni sisi tu kutofautiana kimtazamo. Lakini kubwa na muhimu zaidi ni kwamba tumezidi kupoteza mwelekeo kwani inaonyesha kwamba suala la NIA ya Azimio La Arusha tumekataa kuipa nafasi.

Kuhusu mimi kutojua historia ya nchi yangu pale niliposema Tanganyika ilikuwa nchi inayofuata mfumo wa kibepari kuanzia uhuru hadi 1967, nadhani wewe ndio haujawa makini kuielewa hoja yangu ya msingi. Mwaka 1961 tulipopata uhuru, tuliendeleza mfumo ule ule wa kikoloni ambao ulikuwa na msingi mmoja mkubwa - kuwaunganisha au kuunganisha uchumi wetu moja kwa moja kwenye mfumo wa kimataifa wa kibepari kwa kuzalishia mataifa makubwa mazao ya kilimo - kufanya koloni letu liendelee kuwa chanzo cha malighafi, cheap labour na soko la bidhaa kutoka nje. All in all, our economy had all essential features za capitalist mode of production. Ilipofika mwaka 1967 ndipo mwalimu alipokuja na sera iliyolenga to de-link our economy from this unfair integration of our economy into the capitalist world. The bottom line here ni kwamba - haupo sahihi unapopingana na hoja kwamba mwaka 1961-1967 Tanzania haikuwa inafuata mfumo wa kibepari kama ilivyokuwa kwa kenya, zimbabwe n.k.
 
Bro

Inaonesha ni jinsi gani kwenye hiyo quote ulivyo mtetezi wa wa Azimio kuliko mengine kwa sasa, binafsi sidhani kama hiyo argument yako hipo interested na CHADEMA in general as an alternative for what we have currently, or what they stand for. Right now it's just about your beloved Arusha Declaration.

Kibaya zaidi mme jikita kwenye miiko tu ya uongozi and nothing else out of the seriousness of the declaration. Kuna njia nyingine nyingi tu za kuzuia au kuweka misingi imara ya uongozi. If anything the latest parliament sitting imetufunza kitu, kuna wabunge wameshachoka na upumbavu lakini where the power lies it is a problem.

Sasa hata kama kesho ukiliweka Azimio la Arusha, JK ndio raisi wa nchi hii nothing will change kutokana na madaraka yake na fikra zake. Kwa maana hiyo, haya mambo ya miiko yenu ya Azimio la Arusha ni hadithi za kubembelezana. What we want outside Azimio ni sheria ambazo zitatungwa kutokana na makubaliano ya mikataba kati ya watawala na watawalia. And this is where the need of the new constitution arises.

Labda mtuelezee kwenye dunia isiyotaka mambo ya kubembelezana Azimio litatusaidia vipi in terms of accountability. Maana watu wamekazana na miiko as if it is the magic wand. Wakati realistically kama watu wengi wanaopinga hili Azimio huko nyuma wanavyosema hizi ni hadithi za kubembelezana na zipo full of optimitism without facts.


Taifa lako lina matatizo chungu mtele na Azimio la Arusha aint one ukilipekua deep down na kufuata sera za maendeleo Azimio la Arusha not only damages individual creativity but also creates lines of economical failures. Ntakuelewa kama unataka mfumo wa kijerumani lakini Azimio ni failure and need no more consideration, for the future of our country.
 

- BOB, kukurupuka hapan, Waberoya anakuabaliana na hoja yangu ya msingi kwamba ili tuendelee tunahitaji Taifa linaloheshimu Sheria, sio miiko ya uongozi kwa sababu matatizo ya Azimio ni more that miiiko ya uongozi. Sheria popote duniani husimama yenyewe, ukishaihusisha na siasa au anything else kama Azimio linavyotaka, ndio unapata yanayotukuta hapa Tanzania, yaani confusion.

- Nia na madhumuni ya Azimio ilikuwa kuimarisha utawala wa chama kimoja tu, sio kuikwamua Taifa kutoka kwenye umasikini, jana nimepita Embassy Hotel, nimesikia huzuni sana kwa sababu it is dead, WHY? Kwa sababu serikali haiwezi tena kumiliki Hotel kama under Azimio, sasa kwa sababu imekaa muda mrefu sana bila kuguswa itaishia kuuzwa kwa bei ndogo sana, ndio matokeo ya Azimio, kujenga bila mpango wa matunzo!

- Tusipokubaliana ni hoja yangu ya msingi kwamba Azimio la Arusha, ndilo chanzo cha matatizo yote kiuchumi na kisheria tuliyonayo Tanzania, ni vyema lilifutwa na Mungu atujalie lisirudi tena, maana ndilo limetufikisha hapa tulipo hili taifa tumekwama. Sasa kuna ninyi mnaosema kwamba hailkusomwa vizuri, I mean the author wake mwenyewe lilimshinda mpaka anaacha uongozi, alikuwa haelewi kilichotokea na Azimio lake, ni vyema tukaendelea na ubepari.

William.
 


Waberoya,

Waliweza kupitisha AA kwa sababu kwa miaka hile walikuwa madarakani, walitumia nguvu, walikuwa ndio wenye shule kushinda wale wenye kupinga siasa za nchi bila kuulizwa au kupingwa.

Kwa sasa nashukuru Mungu nikiona posti kama zako za kuonyesha kuwa we have people with intellectual capital ya kuweza kushusha data kutetea LIBERTY.
 


Mchambuzi,

Nilieleza suala la nia lakini naona tunapishana kwenye lugha. Kufupisha maelezo ningeomba katika paragraph za mwanzo za majibu ya posti hii unukuu NIA kutoka kwenye Azimio la Arusha lenyewe. Na baadaye paraphrase kwa maneno yako. Kila document ina preamble au mission statement. Karibu.
 
Kama kweli usemayo ndivyo basi Waberoya naye ameshindwa kuelewa kwamba huwezi kuweka sheria pasipo ku AZIMIA jambo unalotaka kulifanya maana hata mbuzi utamfunga kamba shingoni kwa sababu unataka kumlisha nje ya zizi lake na katika mazingira yapi.
Mnachoshindwa kuelewa nyie nyoite ni kwamba AZIMIO ni la WATU sio vitu bado unachanganya vitu, hiyo Embassy Hotel haihusiani na matokeo ya Hotel hiyo leo hii, sawa kabisa na azma ya kufunga ndoa. Ndoa ipo kwa ajili ya watu na zinatungwa sheria kuilinda ndoa, hivyo kuharibika kwa ndoa haina maana kwamba hoja ya kufunga ndoa ni absurd ati kwa sababu asilimia 70 ya ndoa huharibika. Wenye kuharibu ndoa ni wahusika wenyewe sio ndoa yenyewe au kwa sababu Yesu hakuoa. Utanisamehe kutumia mfano huo kwa maana watu wanatafuta sababu nje kabisa ya mada nzima.

Labda nikuulize hivi unayajua mashirika mangapi ya Hotels Marekani ambayo yamekufa kabisa japo ndani ya Ubepari..Unayajua mashirika mangapi ya biashara yamekufa na kutokana na Ubepari, in hundreds zinafungwa kila siku na ku run bankrupt au kwa sababu hazitangazwi?..Je, haya unaweza yatolea mfano kama ndio athari za Ubepari - hapana na wala kufa kwake hakuhusiani kabisa na Declaration of Independence. Ubepari sio wa WATU bali ni mfumo wa uchumi kibiashara ambao unazo sheria zake kama biashara na sii watu, na ubepari una principals zake za kibiahsra ambazo sisi watu tutatakiwa kuzifuata na sio Ubepari kutufuata sisi maana ubepari sii wa watu bali vitu. Sijui kama naeleweka?

Nimemsoma hata Eric hapo juu kasisitiza Sheria lakini naye anashindwa kuelewa kwamba hata huyo Kagame mbali na sheria anazotumia za ubabe ameweka Azimio na viongozi wote wanajua haramu ni nini na ukifanya kinyume sheria itafanya nini.

Kwa mfano, katika kulinda Usawa wa Wananchi wake Azimio lilisema hivi:- "Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha ustawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa."

Hapa unaona Azimio linamlenga kila MTU, kumkanya MTU kumnyonya mwingne hii haina maana hatuwezi kufanya hivyo kwa kupitia Ubepari... tunaweza kabisa na ndio maana yule balozi wetu kule DC alikuwa hamlipi kijakazi wake mshahara tosha kaingia hatiani.. Neno kunyonya mtu sii la Ujamaa pekee hata ktk Ubepari linakatazwa na hakuna mahala linapingana na utajiri wa mtu isipokuwa pale utakapo wanyonya wengine. Leo hii Tanzania tuna vijakazi wanafanya kazi kwa Tsh 30,000 kwa mwezi maana sii haramu tena kunyonya mtu mwingine ati maadam anakubali kazi basi hakuna kosa!... hivyo ina maana hatuna sheria pia.. Sasa unaposisitiza sheria wakati hakuna haramu ni sheria gani unayoizungumzia?.

Mkuu wangu sheria ni za kidunia na zipo kulinda vitu vyote maliasili na rasilimali zote na ndio maana tuna mhimili wa mahakama ndani ya utawala. Azimio sio siasa hata kidogo ila ni mwongozo ambao utajenga utawala bora unaoheshimu sheria na tunaposema utawala ni pamoja na mahakama, serikali, Bunge na wananchi wanaoongozwa. Hivyo tofauti na sheria, Azimio linawalenga watu wenyewe ambao ndio msingi wa UHURU na Liberty.

Sijui kama unakumbuka vizuri kwa nini Azimio la Arusha liliandikwa au labda nikuulize hivi Je, sisi tulipata Uhuru ili iwe nini yaani Liberty concept yetu ilikuwa nini? What did affirm to be the principle of our Nation.
 

mkuu,
kwa hiyo tatizo siyo azimio la arusha ila watekelezaji wa azimio hilo.
naamini kabisa laiti kama utekelezaji ungekwenda kama azimio lilivyoelekeza basi azimio linabadilisha maisha ya watu na mienendo yao,na linaweza kabisa kuleta matokeo mazuri katika jamii husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…