Nakuelewa kimsingi lakini nadhani kuna tofauti kubwa baina ya kuangalia Azimio la Arusha kwa outward orientation vis a vis inward orientation. Nadhani ume-base zaidi kwenye outward orientation, especially given the fact that unaangalia zaidi experience za wenzetu. Nitajaribu kufafanua kidogo baadae.
Tuanze na hoja yako ya NOSTALGIA. Hapa, it means you are trying to suggest kwamba we as Tanzanians should stop longing, or having desires of the past experience; I beg to disagree with you on that front. Una maana gani kwamba premises and variables za wakati ule zilizopelekea kuundwa kwa azimio la Arusha hazipo tena? Nchi zote zinapigana kutafuta au ku maintain aina mbili kuu za uhuru: Uhuru wa kisiasa na Uhuru wa kiuchumi; Mwalimu Nyerere alikuja na azimio la arusha baada ya kugundua kwamba uhuru wa mwaka 1961 ulikuwa ni wa kisiasa tu, kwani kiuchumi, bado tulikuwa hatupo huru. Tukirudi kwenye premises and variables unazo jaribu kuzijengea hoja - naomba nikuulize:
· Azimio la Arusha lilikuja katika kipindi ambacho karibia 90% ya watanzania walikuwa wanaishi vijijini; Leo hii, idadi hiyo ni karibia 80%; Je, hauoni kwamba we are living at times when the very same variables that led Mwalimu to architect Azimio La Arusha bado zipo relevant?
· Another key variable to analyze Hadi kufikia Mwaka 1967 ambapo kipindi cha 1961 1967 kilikuwa chini ya mfumo wa kibepari, Kilimo kiliendelea kuwa sekta kuu ya uchumi, je chini ya miaka 26 ya ubepari na soko huria (1986-2012) nini kimebadilika?
· A third variable worth our analysis - mwaka 1967, watanganyika wengi sana ambao by default wapo vijijini walikuwa na kiu ya kufaidi matunda ya uhuru, je hali hii imebadilika kwa kiasi gani kwa ndugu zetu huko vijijini ambao leo hii idadi yao inazidi milioni 30 kati ya karibia jumla ya watanzania milioni 46?
Naomba unifanyie analysis yako based on these three variables or more kama unazo kujenga hoja yako juu ya NOSTALGIA and the irrelevance of the premises and variables at this age ambazo kwa wakati ule zilikuwa relevant kupelekea kuzaliwa kwa azimio la arusha.
Kuhusu suala la communism experience katika nchi za ulaya ya mashariki, hoja yako ya msingi naielewa lakini ni muhimu ukatambua kwamba sisi hatukuwa wakomunisti bali wajamaa, na kuna tofauti kubwa kati ya vitu hivi viwili kisiasa, kiuchumi na kijamii. More importantly, Ujamaa wetu ulikuwa ni African based na tafiti mbalimbali zimeonyesha jinsi gani ujamaa wetu ulikuwa tofauti kabisa na ujamaa uliokuwa unaendelea katika jamii nyingine duniani. Ujamaa wetu ulilenga kuwarudisha watanganyika kwenye chungu kimoja na katika hali zao za awali baada ya production system and production relations zao kuvurugwa na mkoloni.
Kuhusu umuhimu wa uwepo wa taasisi mbalimbali za kusimamia haki, sheria, na uwajibikaji, upo sahihi kabisa juu ya umuhimu wake. Katiba mpya ndio solution yetu kuelekea huko. Lakini pamoja na hayo, tusipuuze jitihada za Mwalimu kuanzisha taasisi hizi from scratch pamoja na mapungufu mengi yaliyojitokeza. Muhimu zaidi, tuelewe kwamba Mwalimu alikuwa such a unique and charismatic leader such that hata wananchi hawakuwa na mawazo ya kutaka nchi iongozwe kwa mujibu wa katiba, na ndio maana Tanzania haikuwa na Katiba kwa miaka karibia 13 (1964 1977) and still many didnt bother kwani Ujamaa ulikuwa una deliver kisiasa, kijamii na kiuchumi kuanzia mwaka 1967 to around 1975. Na ni katika kipindi hiki nchi yetu iliweza kupata mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii pengine kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya nchi yetu if we take into account of the importance or an inclusive economic growth or pro-poor growth, or economic growth with human face. Economic indicators and Social indicators went hand in hand. Maendeleo yetu yalikuwa ya juu kuliko kipindi chochote in terms of progressive social indicators (afya, elimu..). We had an impressive economic performance katika miaka ya mid 1960s to mid 1970s - we recorded an average GDP growth of 6% na this growth was pro- poor kwani huduma za kijamii nazo zilikuwa juu.
Kimsingi, nakubaliana na wewe kwamba hakuna kiongozi wa miaka ya ujamaa ambae aliishi maisha yaliyokuwa yanahubiriwa kwenye azimia la arusha. Lakini kuna exceptions za watu kama Nyerere, Kawawa, Sokoine na wengine wachache. Kwa hawa, mbali ya kuwa na ulinzi na makazi mazuri, waliishi maisha ya kawaida sana na mara nyingi walikuwa watatekeleza Azimio la arusha kwa vitendo. Tofauti na enzi hizo, leo hii hata kupanda MTI mmoja au UA, viongozi wanawekewa mkeka, huku wamefunikwa na miamvuli. All in all, kufeli kwa ujamaa kulichangiwa pia na baadhi ya watendaji wa Mwalimu ambao walipewa dhamana ya kutekeleza azimio la arusha kupitia mashirika ya umma na taasisi.
Ni kweli kwamba Sweden ni nchi yenye mafanikio chini ya ujamaa kwa vielezo ulivyoweka, lakini kwa mtazamo wako, Je, sisi tuna nafasi gani ya kuweza embrace mengi ya sera zao chini ya katiba yetu mpya and become a socialist democratic state? Nadhani unaelewa umuhimu wa Tanzania ya leo ku lean towards the socialist principles for quite some time, huku ubepari na ujamaa viki co-exist na kuheshimiana.
Ni dhahiri azimio la arusha lilikuwa na mapungufu kadhaa lakini nina uhakika, ukilichukua sasahivi kasha ukalisoma mstari kwa mstari huku ukiweka Tiki kwenye mambo ambayo unadhani bado yapo relevant na kufuta yale yasio relevant, nina uhakika kwamba ukifikia mwisho wa zoezi hili, zaidi ya nusu ya mambo mle utayawekea alama kwamba bado yanatufaa nyakati hizi and thus find out kwamba your argument on 'NOSTLAGIA' kumbe ni self-defeating.
Mwisho,niseme tu kwamba moja ya makosa aliyofanya mwalimu ni pamoja na idea ya serikali kumiliki uchumi kwa kiwango cha 100%. Hata yeye aliwahi sema serikali kumiliki mashamba ya mkonge kwa asilimia mia ilikuwa ni kosa. Tukumbuke tu kwamba Zao la Mkonge wakati wa ukoloni lilipatia taifa zaidi ya 50% of fedha za kigeni, na hata mpaka miaka ya mid 70s, zaidi ya 30% ya pato hilo bado ilitokana na zao la mkonge.