Mkuu wangu nakuelewa sana unachojaribu kusema. Dhambi zipo na hazitaweza kwisha lakini unapoharamisha dhambi ndipo unapoweza kutunga sheria kupambana nazo. Kwnai majambazi hawapo au wezi sii wapo na hawatakwisha mbona tunaweka sheria wakati haya ni maamuzi ya watu ambao mnadai wako huru.. Hakuna sheria inayotungwa pasipo kuwepo Dira ambayo hutunga mwongozo. AA sio Biblia au kura ila ni mwongozo kama Katiba maana Biblia na Kuran zimeandikwa baada ya imani za dini kufundishwa tena kwa karne nyingi zimepita, waumini walijua wanasali kwa ajili gani wanaabudu nini na hatua gani wazifuate ili waokoke kinyume cha sheria za Romans kina Pilato.
Katiba ndiyo inatunga sheria wakati dira ndiyo blueprint inayotangulia katiba maana huwezi andika katiba kama huna kitu mkononi, na katiba hubadilika kulingana na mazingira ya kidunia japo safari ni ile ile naha ktk dini toka Abraham hadi leo hii kuna vitabu kibao vimeandikwa vya sheria na tofauti. Sheria za imani ya dini zilitungwa baada ya imani hizi kuwepo kwa muda mrefu sana na zimewekwa kutokana na matukio, siku kwa siku, mweuzi hadi miaka sheria ziliendelea kutungwa ili kulinda waumini wake kutokana na all evil around them ikiwa wanataka kwenda Mbinguni. Jiulize kwa nini tunataka kukusanya mawazo ya watu kabla ya kuandika katiba mpya?.. kaa sii kujitmabua sisi ni nani, muungano wetu, kero zetu na kadhalika na tunaazimia kufanya nini.. Kwa nini tusitumie tu sheria kuandika katiba mpya au copy and paste.
Hivyo kwa muumini wa dini, dira yake ni maisha ya hapa duniani, hiyo safari ya kutoka hapa kwenda mahala pema peponi unatakiwa ufanye nini ili upate uzima wa milele na mwongozo na sheria zikawekwa kuwalinda waumini ili wapate kufika huko. Hivyo kinachotangulia ni who U are, WHY unabadilika toka ulivyokuwa na unataka kuwa nani.. Kitaifa tunasema kwa nini unataka kuwa HURU, ili uwe nani na kama ni Liberty ni mfumo gani utumike kulingana na mazingira yaliyokuzunguka, hivyo unaweza kutumia hata negative Liberty inategemea na WATU na ktk MAZINGIRA waliyopo, kisha sheria ina govern. Ukipoteza la kwanza sheria inakuwa haina msingi tena. Leo hii tunaweza mrudisha mkoloni tukatawaliwa na kwa sheria hizihizi zinazotumika leo, ila itapoteza UHURU wetu na tutajuliknana kama tunatawaliwa.
Sheria inalinda tu ile sababu ya WHY, kwa hiyo yule anayetembea nje ya ndoa kama AZIMIO linakataza watu kutembea nje ya ndoa na sababu zake, basi ni rahisi kutunga sheria lakini huwezi kuzuia watu wote wasitembee nje ya ndoa kwa sheria tu. Hata wizi na kifungoi cha miaka 10 au 20 inatokana na uzito wa crime yenyewe ktk jamii na why mwizi hatakiwi ndipo unapotunga sheria.
Yesu alisema wakati fulani kuwaambia waja wake kwamba walipomuuliza kaa kula chakula bila kunawa ni haramu, naye akawajibu sii kitu kinachoingia tumboni ndio haramu bali imani yake. Kwetu sisi waislaam tunaitafsiri hii kwa kusema kwamba binadamu tumeumbwa na madhambi, from out of our hearts come evil thoughts. Na huwezi kuyazuia haya ikiwa hujaazimia kufuata imani hiyo. Kifupi ni kwamba kama unaamini kula bila kunawa mikono ni haramu basi huna sababu ya kuuliza kinachoinmgia tumboni maana uharamu unaanza na fikra zako. Kwa mfano, haramu sii nguruwe wala nyama yake bali imekatazwa, kama una imani ya roho hutakula wala bila kuuliza isipokuwa kama huna imani na hujaazimia kuokoka utakula na utajijengea sababu zako..
So in short is to say, AA isn't the solution but a blueprint of who we are, our sovereignty and against what. Then Law should govern in contrast to any evil thoughts. Sheria pekee haina maana yoyote maana hata Uingereza Malkia yupo juu ya sheria, KIna Sultan wa Saudia wapo juu ya sheria lakini ukiwauliza watakwambia wanafuata sheria kuwa juu ya sheria..Sheria means nothing ikiwa hujui unachokitaka na ndio maana tunaburuzwa kwa kusoma sana sheria wakati roho zetu zinaamini Ufisadi sio kosa - Ujanja kuwahi!..