Aziniye na mwanamke hujiangamiza mwenyewe

Aziniye na mwanamke hujiangamiza mwenyewe

Mtoa mada ana zile imani za kishamba kabisa zilizopitwa na wakati.

Hawa ni watu ambao, chanzo cha maarifa yao ni kanisani ama msikitini tu.

Hawatafuti maarifa nje ya hapo.

Wanacholishwa na wachungaji au mashehe ndio wanameza hicho hicho, na mara nyingi wanalishwa matango pori.

P didy kazini na kila mwanamke maarufu unaemjua, net worthy yake ni 1 bilion USD.


Hizo ni takribani trillioni tatu za kitanzania.

Ukikuta mwanaume mwenye hela hafanyi ngono na watu mbalimbali huyo atakuwa na matatizo ya nguvu za kiume.

Matajiri wanafanya umalaya wa ajabu, na hawajawahi kupata hiyo mikosi anayoisema mtoa mada.
Hoja dhaifu
 
Kaka zangu chukueni hii....

Unapozama kwenye himaya ya mwanamke, ukiibuka pale lazima kuna kitu unaondoka nacho.

Waweza kuchukua baraka au mikosi na nuksi kwa huyo mwanamke.

Kuna mwanamke, mke mwema aliyeandaliwa na Mungu mwenyewe kwa ajili yako, huyo mke mwema ukizama kwake tu unajikuta unafanikiwa na vitu vinatembea na kusonga mbele.

Kuna mwanamke mwingine hakuandaliwa kwa ajili yako ukizama tu kwake kwa tamaa zako za kimwili kisha ukaanzisha naye mahusiano ya kimapenzi utajikuta umepigwa pin ghafla vitu vinaanza kukwama, kila kitu kinavurugika.

Umepewa mke mwema halafu hutulii kwa mkeo, kila siku unahangaika na wanawake ambao hawakuandaliwa na Mungu kwa ajili yako. Kwa nini kujiangamiza?

Hebu tulia na mkeo uliyepewa na Mungu, acha kuonja onja wanawake wa wengine, kumbuka sex ni jambo la kiroho sana, ikiwalala hao wasio wako basi unakuwa umeunganishwa na roho chafu ambapo zitakuandama daima, na hayo maangamizi yanakuwa ni yako peke yako.

Kisima cha MKEO ndiyo kisima cha baraka zote kwako, umheshimu mkeo na utabarikiwa. .

Kwa wale ambao hamjaoa tumieni akili zenu vizuri kwa kujiepusha na uzinzi, oeni mtulie na wake zenu.

Mit 6:32
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Kwa Wakristo hakunaga Baraka kwenye Zinaa...! Huko ni kumkufuru Mungu.
 
P diddy bado anakula bata?
Hali bata, na kuna matajiri wengi tu wanafanya ngono za kila aina na wanakula bata hadi mwisho.

Anachosema mleta mada, ni kwamba unakuwa na mikosi ya kukosa hela, hazungumzii kufanya jinai.

P didy anaweza kuwa na matatizo yake mengine, yaliyomsababisha kufanya jinai.

Kuelewesha mbongo ni kazi, hivi utakuwa umeelewa kweli?
 
Back
Top Bottom