Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Mwana,
Hawa watu wameacha historia zilizotukuka na ndicho kilichonifanya
mimi ninyanyue kalamu kuandika historia zao.

Mengine ya Dossa hayajaelezwa.
Hamza amefariki.
 
Mwana,
Ikiwa unaona nimekosea katika maelezo yangu nakutaka radhi.
 
Naam, huyo ni Kaka'ngu si kama unavyobwabwaja.

Jee, umewahi kumsoma Dossa Aziz nje ya hapa?
Maalim Faiza,
Mimi huwahurumia sana hawa ndugu zetu.
Kwao tusi ni kitu chepesi sana.

Lipi katika haya linalomfanya yeye atutukane?
Sisi tumshukuru Allah kuwa mama zetu walitufunza adabu toka udogo wetu.

Ningependa kumwambia huyu ndugu yetu kuwa hapa si mahali pa matusi ila
ni mahali pa fikra.
 
Huyo Wa kutuaminisha mpiganaji hakuwa Rambo pekee ndio huyu bwanako?
Duduwasha,
Ungeliweza kusema hayo uliyosema bila kutukana.

Punguza ghadhabu la unaona historia hii inakuchoma sana
mimi nakushauri acha usisome hizi, ''post,'' lakini haijuzu wewe
kuandika matusi.
 
Duduwasha,
Hapana sijashindwa kukujibu.

Ila wakati mwingine huwa kuna maswali siyajibu kwa kumfanyia staha
muulizaji.

Mjadala una sheria zake na kubwa ni kumuheshimu unaejadiliananae.
Huwa nikiona kujibu kwangu kutamfedhehesha muulizaji hubakia kimya.

Haya ndiyo mafunzo alonipa maalim wangu Sheikh Haruna aliyenifunza
mbinu za mnakasha, yaani, ''debate.''

Hebu pitia upya majibu waliyokupa wenzangu utaona nini walikwambia.
Naamini hujapendezewa na kauli zao.
 
Naam, huyo ni Kaka'ngu si kama unavyobwabwaja.

Jee, umewahi kumsoma Dossa Aziz nje ya hapa?
Ndio Dossa Aziz nilishawahi msoma katika historia zaidi ya hapa, na hata huyu Aziz Ally nilishamsoma pia.. hapa ni ongeza ongeza tu lakini karibu wote hawa wamo kwenye vitabu vya historia. Mtu ambae hajui labda sijui alisomea wapi Tz hii.
 
Tunaomba "citation" ya ulipowasoma nasi tukajisomee tuone kilichoandikwa kuhusu wao.
 
Duduwasha,
Ungeliweza kusema hayo uliyosema bila kutukana.

Punguza ghadhabu la unaona historia hii inakuchoma sana
mimi nakushauri acha usisome hizi, ''post,'' lakini haijuzu wewe
kuandika matusi.
Mkuu achana nae huyo hawezi kubadilika, badala ya kujenga hoja yeye kaona kutukana watu ndio solution,nadhani malezi aliyoyapata katika makuzi yake ndio tatizo.
 
Usiombe utukanwe na wamama wa kiswahili hasa wa pwani

Unaweza kutukanwa mpaka utapike mwezi mzima.

Sijui matusi wajifunzia wapi wale wanawake wallah.
 
Weweeeee......bibi

Nimekisoma kitabu cha huyu mzee mwaka 2014, s'thing like Life n Times of Abdulwahid Sykes

Alichofanya ni kuzungumzia pre independence era yaani before 1961, kuhusu movements za ASP

Ila angalia contents zake kule utagundua anawapraise waislam over wakristo na wakristo waliotajwa ni wachache mno na kwamba waliwezeshwa na waislam kufanya waliyoyafanya including nyerere.

Katika kile kitabu nilimuuliza mwaka huo huo huyu Mohammed maswali kadhaa kabla ya kuanza kusoma kitabu chake cha pili nlikikuta Magomeni ila sijakimaliza.

Kila ukimuuliza anasema hiyo ndio historia ilivyo n finally as a defence for himself anasema nitafute historia ya kweli inayopingana na yake.

I'm not an Author, but I need to understand hence I do asking whenever I find controversal ideas.

Cc: Mohammed said
 
Azarel,
Ukweli ni kuwa vile nilivyoandika ndivyo ilivyokuwa lakini kama kuna mtu anaona vinginevyo yuko huru na yeye kueleza ayajuayo.
 

Hebu nikupe somo hapo zamani za kale kipindi cha ukoloni hapa kwetu watu waligawanywa matabaka matatu wazungu waarabu wa asia na waafrika weusi ambao ndio wenyeji weusi mtu anaposimulia historia ya taifa letu akatumia neno mwafrika wa kwanza anamaanisha mtu mweusi wa kwanza katika makundi hayo matatu yaliyotajwa na hamaanishi afrika yote ......maana anazungumzia kwa tanzania kutokana na watu walivyokuwa wamegawanya kwa rangi zao sjui nini kinakuwa kigumu kuelewa hapo
 
Ndio Dossa Aziz nilishawahi msoma katika historia zaidi ya hapa, na hata huyu Aziz Ally nilishamsoma pia.. hapa ni ongeza ongeza tu lakini karibu wote hawa wamo kwenye vitabu vya historia. Mtu ambae hajui labda sijui alisomea wapi Tz hii.
Mauza...
Unaweza kweli umewahi kumsoma Dossa Aziz lakini ameandikwa,
ile Waingereza wanaita, ''in passing,'' yaani katajwa bila kushereheshwa.

Wazalendo hawa wametajwa kwa heshima na hadhi zao zote na kama
wanavyostahili kutajwa ndani ya kitabu changu, ''The Life and Times of
Abdulwahid Sykes...''
.
Fanya utafiti hili utalitambua.

Ulipata kujua kuwa ni Abdul Sykes ndiye ailiyeasisi TANU na harakati
alizianza toka Burma katika Vita Vya Pili Vya Dunia?

Ulipata kusoma popote pale kuwa ilikuwa Chief Kidaha Makwaia ndiye
aongoze TAA kisha ndiyo waunde TANU na kudai uhuru?

Hii historia haikuwa inajulikana na wengi.
Haya ndiyo tunayojadili hapa jamvini.
 
Hizi historia za wazee waislam wa kariakoo....wanywa kahawa na kupiga soga kwenye vibaraza kawasimulie wajukuu zao ambao hawazijui...uhuru wa tanganyika ulianza kutafutwa si na ukoo wa skyes&azizi ally.....ulianza tangu wageni ...wareno....waarabu....wajerumani na waingereza walipotuvamia!tumejifunza shuleni!ni aibu kwa mtu mzima kama wewe kutaka kupotosha ukweli....na kulazimisha hao wanywa kahawa&wapiga soga kwenye vibaraza ndo walioutafuta uhuru wa tanganyika!
 
Napenda uandishi was Mohammad Said,tatizo anaweka sana dini mbele kama vile uislam ndio uliopigania Uhuru wa Tanganyika,badilika kaka
History mbona iko wazi aseme wakristo wakati hawakuwepo unataka akufurashe wewe
 
We sio mwislam kwenda zako sasa unataka akufurahishe ww na magalatia wenzako nyie si mlikua upande wa wazungu
 
Hebu tuambie na ww hao watu kwa majina ila mzee rupia hakuna asio mjua
 
Na kama ni uongo ilikua na haja ya nyerere yy mwenyewe kupinga kama ni uongo anakuja mtu ambae kwanza hana hata muongo mmoja ndani ya jiji hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…