Aziz Ali wa Gerezani na Mtoni Dar es Salaam

Atakurushia sababu kama laki za kujustify hilo jina la Qafir
Hakuna jina la ki qafir,kuna majina Mazuri na Majina Mabaya,Kwenye uislamu hata kama ukiitwa rose ama joseph,ama diamond ama Edward ruksaa alimradi jina hilo liwe lina maana na asli nzuri,majina yasiyotakiwa ni yale yasiopendeza ama kutokuwa na maana mujarrab kama vile Shida,Masumbuko,Chuki,punda,(ashakum si matusi)[emoji482],mashaka etc,acha kueneza chuki baina yetu waislamu na wakristo ni ndugu moja watoto wa baba mmoja tusikwazane
 
mkuu sikia mimi sina tatizo na historian wala history kitu ambacho hatuendi sawa ni style yake ya kuchomeka watu wasio na kichwa Wala mbele pengine hawakuhusika kabisa tena utakuta ndio walikuwa mashushu au wanafiki kwa wazungu katika harakati za Uhuru vibaraka huwepo... Sasa kuna walioondolewa kabisa na wengine waliostukiwa kwa sababu mbali mbali ikiwemo hiyo ya udini ambao mtoa Mada ndio msingi wake mkubwa Wa thread zake humu... Hao watu vibaraka walianzisha hadi vyama pinzani before uhuru... Ila Nyerere alikomaa na alikuwa hapendwi kwa kiswahili cha bara na kujua kwake kiingereza na ukristo wake Nyerere sasa huyu amerithi chuki tena nadhani ile misemo ya Mfumo kristo ndio Hawa walidhania Nyerere angejaza watu Wa msikitini kwenye serikali huku elimu hamna.. Hizo history za Uhuru na wapigania zipo mashuleni zimejaa waingereza wanazo Nyerere kaandika vitabu na kuna speech record TBC tele so acha uoga na story za huyu mzee hii nchi imepata Uhuru kwa kiongozi Ukristo. Yeye inamuuma. Anachofanya ni kutranslate vitabu na kuandika kwa kiswahili huku aliwachomekea sifa wahusika ambazo hazina misingi... Ati tayari akiwa mkristo oh mwafrika Wa kwanza kununua gari kujenga nyumba ya vitae n.k

Me sina chuki nae ila yeye anachuki na christian. Tulioleta Uhuru historia ndio ilivyo haibadilishiki hawezi rejesha ile hali yao ya chuki hadi wakristo kuishi kariakoo ni mission kota tu iliwezekana ila Tajili mkubwa Rupia anamuelewa
 
I don't get you!
Unamlalamikia mwenzio mdini wakati wewe unafanya the same!
Historia yako wewe ni ya ukristo na jamaa ya uislam!
Hebu changanyeni hizo historia 2 tupate version ya Tanzania!
Huwezi kubeza mchango wa waislam na uislam ktk uhuru wa Tanganyika! Lakini huwezi pia kukataa kuwa wakristo walikuwepo mstari wa mbele ktk uhuru!
Mapambano mazima hayakujengwa kwa misingi ya dini, nadhani uafrica ulitawala Zaidi ya kitu chochote, leo nyie vijukuu na vitukuu wa wapigania uhuru mnatazamana kwa dini mlizo rithishwa na wakoloni!
Ila I don't see you ukisema history, nakuona ukipinga tu!
Ukombozi wa kisiasa hauwezi kuwa na watu wawili, lazima kulikuwa na teams za kutosha!
upinzani ktk siasa usichukuliwe vibaya hata kidogo na hata kama mtu alikuwa mamluki lkn bado anapaswa kutajwa kwenye historia kwa nafasi yake!
 
Wenye kuelewa walielewa

Mohamed anajulikana wewe hujui
 
Rose...
Unayo historia kinyume ya hivi?
Iweke hapa tuisome ikiwa unayo.

Sheikh Mohamed Said, hilo ombi ulilompa huyo Bi-mkubwa itapita Miaka 2000 mingine pasipo kuleta Historia tofauti na hii.
Na Yesu pia atarudi na kuingia hapa JF baada miaka 2000 mingine na Historia ataikuta hii hii.
Kinachotokea kuuchukia ukweli, Khalas.Neno Uislam kwa upande wa wenzetu ingewezekana Kwao walitamani lisitajwe popote inapotajwa Tanzania, huo ndio ukweli, ndio maana Sheikh Mohamed Said ukileta habari hizi watu wanakuona mdini, wanaweka ukweli pembeni wanasogeza jirani Udini, hawaleti historia yao ili tuone uongo wa Mohamed Said.
Nnazo picha za Miaka ya 1950 Nyerere yupo mitaa ya Magomeni, Mwinyimkuu au Takadiri kwenye ile picha Dini tofauti alikuwa Nyerere peke yake, na ni picha ambazo zilihusu harakati hizo za mambo ya vyama.
Mnaompinga mpinge tu, lakini huu ndio utabakia ukweli mpaka mtapoleta nanyi Historia ya Uhuru inayopingana na Mohamed Said kuwa waislam hawakuhusika na chochote kuhusu uhuru wa Tanganyika.
Baada ya hapo sasa tutaamini kweli Mohamed Said mdini maana kaleta Historia wengine kawaacha.
Mwenyezimungu akufanyie wepesi Sheikh Mohamed Said.
 
Amina, Sheikh apewe wepesi. Kuna figisu nyingi sana zimefanyika kuficha ukweli.
 
Amina, Sheikh apewe wepesi. Kuna figisu nyingi sana zimefanyika kuficha ukweli.
Lipyoto,
Kila aliyekisoma kitabu cha Abdul Sykes au kusikia historia hii kwa mara ya kwanza alipigwa na butwaa.

Baada ya mshtuko huo wapo waliokasirika na wapo pia waliofurahi.

Mimi sishangai hapa ninapoona hizi hamaki na wakati mwingine matusi.

Wangependa tubaki na ile historia rasmi iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.
 
Mzee wangu Mohamedi Said nakualika ufike katika kijiji chetu cha Moa, Tanga, kijiji maarufu sana kwa mwambao wa kaskazini mwa Tanga, sikua nikijua kuwa Aziz Alli alitokea kijijini kwetu, Subhana Llaah, njoo kuna mzee mmoja ni babu yangu amezaliwa kunano mwaka 1926 au 1927. Bado yu hai na nguvu tele, ana mambo mengi sana unaweza kustafid.
 

Duh unaona maajabu ya mtandao hayo akhi
dangadunguri.Maalim Mohamed Saidi kanifungua macho Na historia ambayo nilikuwa siijui.MwenyeEZMungu amlinde maalim wetu Mzee Mohamed Saidi Na husda Na kila balaa
Amen.
 
Danga...
Ahsante sana kwa mwaliko.
Nimewahi kufika Moa na kwa kweli ni kijiji cha kiasili.

Nimeona ule msikiti pale na gati ambalo kwa wakati
ule nilipofika lilikuwa limemezwa na bahari lakini bado
linaonekana.
 
Waafrika wanafika sana, walikuwa wanawapinga makaburu halafu wanajibebesha majina ya kikaburu. Mbona makaburu hawakujiita Totsi, au Vusi?
Miafrika tuna mapepo wachafu vichwani
Buibui,
Waafrika kulipa majina ya watawala wao si kwa sababu walikuwa wanafiki.

Hii ni moja ya majanga ya ukoloni.
Hebu angalia hili.

Kleist Sykes katika mswada wake aliandika kuhusu maisha yake na vipi baba yake alikuja Tanganyika akiwa askari mamluki anasema kuwa Herman von Wissman aliweka mkataba nä Affande Plantan kuwa wakiiteka Tanganyika wataitawala kwa ushirika kati ya Wajerumani na Wazulu.

Nani hii leo anaweza kuamini ulaghai kama huu.

Sasa tuangalie nini kilifuata baada ya ushindi wa Wajerumani dhidi ya Abushiri bin Salim Al Harith na Chief Mkwawa.

Wajerumani wakatengeneza jeshi wanaliita Germany Constabulary na Mkuu wa Jeshi hilo akawekwa Affande Plantan.

Jeshi hili likawekwa katika kambi.
Watoto wote waliozaliwa katika kambi za Wajerumani walipewa majina ya Kijerumani.

Lakini wazee wao hawakuridhia wakawa wanawapa majina yao ya asili.
Ndiyo maana unakuta Kleist jina lake ni Abdallah.

Schneider ni Abdillah nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…