Mohamed Said unasema historia imewafuta kivipi?? Mbona mimi nimesoma historia na hawa watu wote unaowataja hapa wamo pia?? Mie ninachokipinga kwako ni umebase sana kwenye udini as if hao wengine wapagani na wakristo walikua magoi goi katika kutafuta huo uhuru. Kumbuka kua humo pia kuna wahindi na waarabu walikuwamo sijakuona ukiwataja kabisa dont say huwafahamu.
Angalizo: mimi ni muislamu ila udini noo kwangu.sisi ni watanzania na afrika ni moja.
Mauza,
Zungumza jambo unalolijua na kama wewe wewe ni Muislam
kama unavyosema utakuwa unajua kuwa Allah kaonya mtu
kulisema jambo ambalo hana ujuzi nalo.
Nakuona umelishikilia sana hili la udini wakati mimi nimeandika
kitabu cha historia hii na kimefanyiwa mapitio na mabingwa wa
historia ya Afrika kama
John Iliffe,
Jonathon Glassman na
James Brennan na hakuna hata mmoja kauona huo udini unaodai
wewe.
Catalogue ya Library of Congress inakieleza kitabu kama, ''Political
History.''
Mimi nimefanya utafiti na si wa kitabu hiki tu nimeandika ''paper,''
na huo udini unaoutaja wewe nimekutananao kwingi lakini si kwa
Waislam.
Fanya rejea kwa
P Van Bergen (1981),
Sivalon (1992) na
Njozi
(2002).
Fanya rejea hizo kisha rejea hapa jamvini utuambia kipi umekiona.
Ikiwa unawajua Wapagani, Waarabu na Wahindi katika historia ya
TANU tupe habari zao ili tujifunze lakini mimi nimewataja wote
waliokuwapo ulingoni wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.
Ila nitakufahamisha kuwa wasio Waafrika walifunguliwa milango
kujiunga na TANU 1958 katika sakata la Kura Tatu.
Ila ndugu yangu nakuonya kwani wengi wamesababisha kuangamizwa
kwa wenzao kwa kusema wasiyoyajua.
Iko siku nitakupa kisa cha
Rajab Diwani na
Selemani Kitundu hadi
leo wametangulia mbele ya haki lakini madhila waliyoacha nyuma bado
yanakumbukwa.
Ndipo nilipokupa indhar mwanzo kabisa kuwa usiseme jambo usilolijua
kwa kutafuta sifa ukidhani utaonekana, ''Muislam mwema.''
Historia ya uhuru wa Tanganyika ina wengi mfano wa wewe na wote
wamemaliza maisha yao kwa majuto.
Nahitimisha kwa pale ulipozungumza, ''Afrika ni Moja.''
Nakufahamisha kuwa
Ali Juma Ponda na
Hassan Suleiman wakiwa
viongozi wa African Association 1945 walipata kuandika waraka muhimu
kwa Watanganyika wenzao wakiwaeleza kuhusu umoja wa Afrika.
Kushoto wa kwanza ni Ali Juma Ponda
Watafiti wa Chuo Cha Kivukoni hawakuwataja hawa popote katika kitabu
chao cha Historia ya TANU.
Labda hawakuwa wanawajua.