Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #161
Jaji...Mama yake alizalishwa na mzungu
Mama yake ni Mnyaturu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaji...Mama yake alizalishwa na mzungu
Umesoma kitabu gani ambacho kinawataja hawa wapambanaji kinagaubaga tunaomba tupe rejea blaa blaa hatutaki kusikiaMohamed Said unasema historia imewafuta kivipi?? Mbona mimi nimesoma historia na hawa watu wote unaowataja hapa wamo pia?? Mie ninachokipinga kwako ni umebase sana kwenye udini as if hao wengine wapagani na wakristo walikua magoi goi katika kutafuta huo uhuru. Kumbuka kua humo pia kuna wahindi na waarabu walikuwamo sijakuona ukiwataja kabisa dont say huwafahamu.
Angalizo: mimi ni muislamu ila udini noo kwangu.sisi ni watanzania na afrika ni moja.
Kina Sykes kiasili wao ni wafa
Sykes kiasili hawa ni wafanya biashara kujihusisha ktk Siasa ilikuwa ni kupitia Kulwa support harakati hizo financially. Hata leo sehemu kubwa ya familia hii ni wafanya biashara.
Mkuu Mohammed Said, ingawa ni nje ya mada, tunaomba kama unazo data nje ya zile nilizozikuta wikipedia, unipe wasifu wa huyu mtu TIP TIPU. historia yake inaonyesha ni mwarabu-mwafrika na kuwa kaburi lake alizikiwa Stone Town Zanzibar. Sasa sijaelewa huyu ni upande upi walikua na nasaba za kiafrika, kutoka mkoa gani hapa Tanzania? Na je uzao wake upo hadi leo hasa wale wenye asili ya Afrika, wako mkoa gani?
Nitashukuru sana
Lipyoto,Mkuu Mohammed Said, ingawa ni nje ya mada, tunaomba kama unazo data nje ya zile nilizozikuta wikipedia, unipe wasifu wa huyu mtu TIP TIPU. historia yake inaonyesha ni mwarabu-mwafrika na kuwa kaburi lake alizikiwa Stone Town Zanzibar. Sasa sijaelewa huyu ni upande upi walikua na nasaba za kiafrika, kutoka mkoa gani hapa Tanzania? Na je uzao wake upo hadi leo hasa wale wenye asili ya Afrika, wako mkoa gani?
Nitashukuru sana
Iparamasa,Mohamed said anafunguka!
Haya mambo ni makubwa,Iparamasa,
Hakuna jipya kaka yale yale ya siku zote.
Hebu angalia hii nyumba hapo chini:
![]()
Nyumba hii iko kwenye kona ya Mtaa wa Max Mbwana (Zamani Stanley Street kisha Aggrey Street)
na Mtaa wa Sikukuu.
Hiyo ni nyumba yao akina Syles wamejenga miaka ya hivi karibuni.
Hapo ilikuwa nyumba ya mwisho kujengwa na Kleist Sykes na baada ya kifo chake 1949 ilirithiwa
na mwanae Abdul.
Nyumba hiyo ya zamani ilikuwa na historia kubwa sana.
Harakati zote za siasa kuanzia 1950 zilikuwa zikifanyika hapo kwani kwa wakati wake hiyo ilikuwa
nyumba nzuri ya kupigiwa mfano.
Nyumba ya bati umeme na na maji ndani na ina ''sitting room,'' na vyumba vya kulala na jiko la
nafasi uani.
Hapa ndipo wanaharakati wakikutana kwa president wa TAA na wakati mwingine wakifanya party
ndogo ndogo za kazi au kula lunch ya pamoja au kwa mazungumzo tu ya kawaida.
Hapa ndipo alipokuwa akija Chief Kidaha Makwaia wa Shinyanga kwa mazungumzo na Abdul Sykes
kuhusu hali ya baadae ya Tanganyika.
Hapo ndipo Kasella Bantu alipomleta Mwalimu Nyerere kukutana na Abdul 1952, Nyerere akiwa
na barua kutoka kwa Hamza Mwapachu aliyekuwa bado yuko Uingereza masomoni.
Baada ya kuundwa kwa TANU 1954 na Mwalimu Nyerere kujiuzulu kazi ya ualimu alikuja kuishi na Abdul
kwenye nyumba hii kabla Mwalimu hajatafutiwa nyumba Magomeni Majumba Sita na Mzee Rupia.
Hakika nyumba ile iliyovunjwa na kujengwa hili ghorofa limekwenda na historia kubwa sana ya Tanganyika
ambayo si wengi wanaifahamu.
Iparamasa,Haya mambo ni makubwa,
Ni historia pana inayofanya mtu aitafakari historia aliyoilipia ada shuleni kama kweli ilibeba mambo yote
Nyakageni,Mzee shikamoo na heri ya mwaka mpya. Bandiko lako ni zuri sana. Na vipi kuhusu mchango wa baba yako mzazi. Kwa sababu aliishi jirani sana na huyu mtanzania mwenye asili ya kijerumani, Sykes. Na hawa akina Dully ni wajukuu au hawana undugu?
Slim5,Historia niliosoma katika 7+4+2 haifiki hata robo ya ninachopata kwa Al ahky Maalim Mohamed Said
Mungu akulipe kheri Mzee wangu.
Iparamasa,Haya mambo ni makubwa,
Ni historia pana inayofanya mtu aitafakari historia aliyoilipia ada shuleni kama kweli ilibeba mambo yote
Huvumi lakiniiiii, well, umo! Thanks for the unshakeable records.Walikuwa na dada yao woman police aliitwa Mwanakondo.