Baada utawala wa Syria kuanguka Israel wamekimbilia kuchukua maeneo katika miji mitano katika milima ya Golan ya Syria wanazidi kuongeza mgogoro

Abondwe tu
 
Wanawahi mapema tu kwani sianajuwa iran anawatafuta kimfumo. Yeye katangulia ngoja tuone moto.
 
Iran na Russia wapo likizo??
Nakumbuka Urusi ilitufanya kitu mbaya wakati wa vita na Uganda!
Russia alimuuzia Ndege vita iddi Amini!
Sisi alituuzia ant aircraft missile!
Tulipo ishiwa mabomu ya heat seeking missile's!; mrussi alikataa kutuuzia mabomu Hadi Kwa Hard cash au Mikataba migumu Kwa dhamana ya Mali Asili!
Huku Ndege vita za iddi Amini zinatamba Hadi Mwanza Visiwa vya Saa nane!
Lengo lake lilikuwa vita yetu na Uganda iwe Endelevu Ili auze silaha zake!
Kukosa Hekima ya J.K.Nyerere Kuomba msaada wa hayo mabomu Msumbiji na Algeria!; Ile vita ingekuwa ni simulizi nyingine!πŸ˜‡πŸ˜­
Hiyo Ilinikera Hadi Sasa kuichukia Russia....
 
Tatizo sio Israel tatizo ni Qatar, Turkey na Saud Arabia walimuahidi Mrusi maslaha yake yatabaki hivyo Assad lazima atoke. Pia Saud Arabia na badhi ya nchi za Gulf target yao ni kuimaliza Hamas na Hezbullah ili wao wabaki kwenye viti vyao, wanadhani kumkubatia US watakuwa kwenye safe zone. Hivyo ndivyo wafalme wa kiarabu wanadhani kama alivyo dhania Assad kuwa Mrusi atamlinda. Tokea lini wavaa misalaba na .ashiga zao wayahufi wakawa waminifu na wakweli?

Israel kaona hio ni fursa kwake kuvunja silaha za Syria, ili watakao tawala wawe wanakubali wanacho ambiwa na Israel.

Bashar Assad alipewa offer awachane na Iran na Urusi, na Syria itajengwa kuliko mwanzo akakataa, hicho ndicho kilicho mponza hakutegenea Mrusi na Iran watamuza vile.


Any way hatujui mipango ya Allah, si ajabu hawa ndio wakamuondoa Israel pale. We huoni Israel anapiga silaha na viwanda vya kutengeneza silaha, anacho ogopa ni kitu gani? Kaona hao jamaani hatari wameweza mpindua Assad kwa silaha walizo kuwa wanateka kwenye majeshi ya Assad, itakuwa balaa wakiwa na silaha kali. Israel alicho furahi hao ma rebels wa Syria kumpindua Assad, ni kuweza kukataa mawasiliano kati ya Syria, Hezbullah na Iran lakini hajui Allah naye huwa ana mipango yake. Ukizuia huku ana fungua huku, si ajabu tukasikia Egypt na Jordan wamepindua waislam hapo ndio patakuwa patamu.
 
Hiyo imeenda hiyo imeisha hiyo ukipoteza kwenye vita na kila kitu chako kinachukuliwa na aliyeshinda
 
Ayatolah kanishangaza sana leo, anasema Nchi majirani wa Syria zisiingilie mambo ya ndani ya Syria...amaa kweli Nyani haoni kundule.." si ni huyu huyu Mzee Ayatolah ndio huwa anaingiliaga mambo ya ndani ya Lebanon Yemen Iraq Syria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…