Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Waswahili wana msemo: "atafutae hachoki, akichoka amepata". Msemo huu utajidhirisha huko Zanzibar kuanzia sasa ambapo Wazanzibar wanaotafuta ukombozi kwa mara ya pili, watatafuta ukombozi huo kupitia chama tofauti na ACT-Wazalendo na chama pekee kitakuwa ni CHADEMA unless CHADEMA nao waonyeshe udhaifu wa kuungana na CCM Bungeni au nje ya Bunge.
Maalim Seif sasa ameshapoteza ushawishi kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuwa sehemu ya makubaliano ya kuungana na watesi wao, na zaidi Maalim umri umeshamtupa mkono hivyo wananchi hawawezi tena kumtegemea kuongoza mapambano ya 2025 katika kutafuta dola hivyo Maalim ameshafika mwisho kisiasa.
Kwahiyo, kama ambavyo Wazanzibar walimfuata Maalim ACT, ndivyo sasa watajikuta hawana option zaid ya kusimama na CHADEMA huko Zanzibar wakati wowote kuanzia sasa ambapo tunaweza kushuhudia bendera za ACT-Wazalendo zikishushwa katika maeneo mbalimbali huko Zanzibar na Siku zijazo CHADEMA ndio ikawa mbadala wa ACT kama ambavyo ACT ilivyokuwa mbadala wa CUF.
Pia, Wazanzibar sasa wanakwenda kuacha na siasa za kuwa wafuasi wa mwanasiasa fulani na sasa watakuwa wafuasi wa taasisi za kisiasa(vyama vya siasa) kama ilivyo huku Bara ambapo mwanasiasa wa upinzani akihama upinzani na kujiunga na CCM, ushawishi wake nao unafutika kama tulivyoona kwa Dr. Slaa na sasa Halima Mdee na kundi lake.
Mungu ana makusudi na kila jambo, hivyo maamuzi ya ACT kujiunga katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar, yanaweza yakawa ni faida kwa CHADEMA na pigo kwa ACT na viongozi wake.
Wanachopaswa kufanya CHADEMA ni kuendelea kuikataa CCM na makandokando yake kama walivyofanya kwa kuwakataa kina Halima Mdee na kundi lake kwani adui wa CCM kisiasa (CHADEMA), ndio atakuwa/ataendelea kuwa rafiki wa Wazanzibar walio wengi, na rafiki wa CCM kisiasa(sasa ACT), ndie atakuwa /ataendelea kuwa adui wa Wazanzibar walio wengi.
Muda utathibitisha.