Baada ya ACT-Wazalendo kujiunga katika SUK huko Zanzibar, CHADEMA kinakwenda kuwa Chama Kikuu cha Upinzani Zanzibar

Baada ya ACT-Wazalendo kujiunga katika SUK huko Zanzibar, CHADEMA kinakwenda kuwa Chama Kikuu cha Upinzani Zanzibar

Hali ya maisha ikiwa ngumu kiasi cha kutosha(zaidi ya hapa), hatutahitaji mwanasiasa wa kusema tuandamane kuwakataa watawala, bali tutaingia barabarani bila kuambiwa na mtu na hizo siku zaja.
Pumbvuuu wewe
 
Waswahili wana msemo: "atafutae hachoki, akichoka amepata". Msemo huu utajidhirisha huko Zanzibar kuanzia sasa ambapo Wazanzibar wanaotafuta ukombozi kwa mara ya pili, watatafuta ukombozi huo kupitia chama tofauti na ACT Wazalendo na chama pekee kitakuwa ni CHADEMA unless CHADEMA nao waonyeshe udhaifu wa kuungana na CCM Bungeni au nje ya Bunge..........
Mkuu, Kishina cha Mshahara, Salary Slip, kumbe wewe huwajui Wazanzibari. wao wanachagua mtu sio chama sio sera!. Uamuzi wa ACT kujiunga na SUK, is the best decision.

Uamuzi wa Chadema kuendelea kususa, na kuwasusa kila halima, they have every thing to lose and nothing to gain, kwa Chadema kukubali matokeo, they'll have everything to gain and nothing to lose!. Wanaihitaji sana hiyo ruzuku, na hakuna mkate mgumu mbele ya chai!

P
 
1607272589495.png

 
Mm nnavojua wazanzibar wapenda mtu na sio chama especially Maalim Seif
 
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa uamuzi wa ACT leo umekipoteza kabisa hicho chama na watu wamejuta kuamini kuwa ACT ni chama cha upinzani.

Kwa wale tunaokumbuka namna kilivyoanzishwa ili kujaribu kudhoofisha CHADEMA lakini ikashindikana hatushangai kuona kamati kuu inatoa maamuzi kama hayo.

CHADEMA endapo watacheza karata zao vizuri na kusimamia uamuzi wao wa kutokuwa sehemu ya wabunge walioshiriki kwenye wizi wa kura wataendelea kuwa chama kikuu cha pinzani na chenye kukubalika bara na visionair.

Sharti moja wapo waamuwe haraka kuwatosa madiwani pamoja na huyo mbunge mmoja kama wa dawa. Hakika wakitoswa hao chama kitakuwa kimejipatia umaarufu mkubwa wa kusimamia katiba ya chama pamoja na sheria na katiba ya nchi.
 
Chief weka ukereketwa pembeni na uone hali halisi. CHADEMA NA CUF hawakua wakiamiana, na sasa CHADEMA na ACT-ZANZIBAR au CUF MAALIM hawaamiani kwa sababu kuu moja, UDINI (UISLAM). Wazanzibar hawaimini kabisa CDM sababu wanaamini ni chama cha Kikristo, kwao bora CCM kuliko CDM. Hivyo suala la CDM Zanzibar isahau. Jambo la pili, Wapemba wanamuamini sana Maalim, hivyo Maalim ataacha mrithi wake.

PS: Chadema na ACT ni kama paka na nyoka, wao kwa wao ni maadui, ila wakimuona panya wote wanamuwinda.
 
Hizo ni ndoto za mchana, wenye mamlaka ya kuchagua kipi kiwe chama kikuu cha upinzani wameamua kwenda na ACT
 
Kutafuta ukombozi kupitia anaekutawala ni sawa na kulima mpunga katika shamba la jirani yako ambae mna uadui.
Ngoma inaendelea kukosewa.
 
Hilo swala ni sawa na kula chakula kupitia mkundu.
 
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo, ila natafautiana na wewe unaposema Chadema itachukua nafasi ya ACT. Ni kweli kwamba Chadema wataweza kujiongezea wafuasi kidogo kutokana na hili ila si kwa kiwango kikubwa.

Pamoja na kwamba hadhi ya maalim Seif itashuka kwa kiasi kikubwa lakini sidhani kwamba wazanzibari watavutiwa na Chadema. Kwa sababu wazanzibari si watu wa kuamini chama kwa haraka haraka. Wazanzibari wanaweza kumuamini Lissu kama Lissu na si chama chake.

Wazanzibari walihamia ACT kwa kumfuata Maalim Seif. Kikubwa kwa wazanzibari kwa sasa ni mamlaka ya nchi yao. Yaliotokea Chadema yanajulikana kwa viongozi wake kuwa waunga juhudi kwa wingi wao, hili limewafanya wazanzibari waliowengi kutoamini Chadema. Na kwa maana hii hawawezi kutofautisha baina ya Chadema na ACT.
 
2025 takua ngumu sana kwa upinzani, binafsi nimekata tamaa na nadhani ni wananchi wengi wamekata tamaa na huu upunzani wa Tanzania, nina uhakika hawajui wanachosimamia mpaka sasa

Kwa kifupi, 2025 wanachama wengi wa upinzani hawatajisumbua kupiga kura wala kushabikia siasa, na kwa mtaji huu ccm itatawala kwa mabavu milele

Mpinzani wa kweli nchi hii ni Lissu tu, atlist anatia moyo, hao akina Zitto ni mapandikizi ya ccm na wachumia tumbo wa kiwango cha lami
 
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo, ila natafautiana na wewe unaposema Chadema itachukua nafasi ya ACT. Ni kweli kwamba Chadema wataweza kujiongezea wafuasi kidogo kutokana na hili ila si kwa kiwango kikubwa...
Muda utasema. Uzuri siku hazigandi.
 
Sidhani kama Wazanzibar wataendelea kumuanini tena. Yaliyofanyika mwaka huu huko Zanzibar yanatisha hivyo haingii akilini kuungana na walifanya unyama ule.
I hope unatania. Mnajua kama chama mna matatizo makubwa sana kwasasa?
 
Back
Top Bottom