Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa

Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa

Kesi Leo Leo imeishia?. Ila ya yule mfiraji analindwa pamoja na Gekul. Kweli hii Serikali ya kijinga Sana.
Kama mshitakiwa kakiri kosa kesi iendelee kuthibitisha nini!!, ukikiri kinachofuata ni mvua tu hakuna ziada.
 
Kijana Shadrack Chaula (24) mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amehukumiwa faini ya Shilingi Milioni 5 au kifungo cha miaka miwili jela akishindwa kuilipa faini hiyo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Kusoma hukumu hiyo, bofya hapa ~ Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela

Wakili aelezea
Wakili Michael Lugina ambaye ni mmoja wa Mawakili waliokuwa wanajitolea kwenda kumsaidia Kisheria, Shadrack Chaula amesema “Tumepata taarifa ya hukumu kabla hatujafika kukutana na mhusika, kwanza inawezekana ikawa moja ya kesi iliyoendeshwa kwa haraka zaidi Nchini kwa kuwa sio kawaida.

“Tunasubiri kupata ripoti ya hukumu ili tuone mwenendo wa kesi na hukumu ulivyokuwa na kama hatua zote zilifuatwa kisha tutafanya maamuzi ya kukata rufaa.”
Hii nchi imefika pabaya sana ni afadhali kukimbilia kwenye kundi la simba, chui, fisi, mamba na chatu porini utasalimika lakini sio watu waliopewa dhamana ya kulinda uhai, mali za mwananchi na kuzuia uharifu...period.
 
Kama mshitakiwa kakiri kosa kesi iendelee kuthibitisha nini!!, ukikiri kinachofuata ni mvua tu hakuna ziada.
Nani kakuambia kakiri kosa...alichofanya siyo kosa...umeisoma hukumu au mawazo yanatoka kwenye masaburi?
 
Wameamua kufanya haraka kabla ya mawakili waliouitolea kufika huko. Wanajua wazi hakuna kesi hapo kama kina utetezii unaoeleweka. Kuanzia sasa hili liwe fundisho kwa mawakili wote wanaojitolea kutetea haki kuwahi mapema kwa wateja wao.
Itakuwa ni mchezo umechezwa na serikali hii ya hovyo
 
Wakili Michael Lugina ambaye ni mmoja wa Mawakili waliokuwa wanajitolea kwenda kumsaidia Kisheria, Shadrack Chaula amesema “Tumepata taarifa ya hukumu kabla hatujafika kukutana na mhusika, kwanza inawezekana ikawa moja ya kesi iliyoendeshwa kwa haraka zaidi Nchini kwa kuwa sio kawaida.
👊👊🙏🏼
 
Hii kesi ingizwe kwenye guines book of world record 😄

Ova
 
Back
Top Bottom