Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa

Baada ya alichechoma picha ya Rais Samia kuhukumiwa Miaka miwili Jela, Wakili asema wanafikiria kukata rufaa

Kijana Shadrack Chaula (24) mkazi wa Kijiji cha Ntokela, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amehukumiwa faini ya Shilingi Milioni 5 au kifungo cha miaka miwili jela akishindwa kuilipa faini hiyo kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Kusoma hukumu hiyo, bofya hapa ~ Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela

Wakili aelezea
Wakili Michael Lugina ambaye ni mmoja wa Mawakili waliokuwa wanajitolea kwenda kumsaidia Kisheria, Shadrack Chaula amesema “Tumepata taarifa ya hukumu kabla hatujafika kukutana na mhusika, kwanza inawezekana ikawa moja ya kesi iliyoendeshwa kwa haraka zaidi Nchini kwa kuwa sio kawaida.

“Tunasubiri kupata nakala ya hukumu ili tuone mwenendo wa kesi na hukumu ulivyokuwa na kama hatua zote zilifuatwa kisha tutafanya maamuzi ya kukata rufaa.”
DAAH AISEEEE KWELI MAHAKAMA NI MALI YA CCM
 
Amuombe radhi bi Chura kiziwi na amsifu haswaaa...kwamba bila yeye Tanganyika itapotea,.. Bi Chura ndio Muarobaini wa Matatizo yote ya Watanganyika...kesho tu..anaachiwa chap
 
Hata asingekiri, bado hukumu ingekuwa hiyohiyo. Tunaujua udhaifu wa mahakama zetu kwenye suala linalohusu watawala.
acheni usenge basi,yule mtu kwanza anaonekana kama kuna fuse zimekatika kichwani sio mzima kabisa,unakili kosa unasema upewe adhabu yeyote wewe kama hakimu ungemfanya nini mtu kama huyu.
 
acheni usenge basi,yule mtu kwanza anaonekana kama kuna fuse zimekatika kichwani sio mzima kabisa,unakili kosa unasema upewe adhabu yeyote wewe kama hakimu ungemfanya nini mtu kama huyu.
Kwahiyo hiyo mahakama inafunga wehu?!
 
Back
Top Bottom