Baada ya Humphrey Polepole kufanya shambulio zito la ghafla la kisiasa kitaifa na kimataifa dhidi ya utawala wa sasa wa Mama Samia, tayari ndani ya CCM kuna maumivu makali ikiashiria kisu kimetua kwenye mfupa. Kwa sasa ndani ya CCM hakukaliki, na mpango uliopendekezwa kufanyika kwa haraka ni kumvua uanachama Humphrey Pole Pole.
Soma Pia: Humprey Polepole ajiuzulu Ubalozi, Asema hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba na chama
Mchakato uliopangwa ni kumuita haraka kuja kujieleza (jambo ambalo huenda Polepole atalikaidi, maana anaweza asirejee sasa hapa Tanzania na pia halitabadilisha chochote) na baada ya hapo itatangazwa kuvuliwa uanachama.