Tetesi: Baada ya CCM kupigwa kwenye mshono, sasa yajipanga kumvua uanachama Humphrey Polepole

Tetesi: Baada ya CCM kupigwa kwenye mshono, sasa yajipanga kumvua uanachama Humphrey Polepole

Ujinga sio tu mzingo bali mtaji watu
Wabongo tuna idadi kubwa sana ya wajinga, ndio maana kunakuwa na hizi imani za kuamini sana hivi viutabiri uchwara ili wapate matumaini...
 
Baada ya Humphrey Polepole kufanya shambulio zito la ghafla la kisiasa kitaifa na kimataifa dhidi ya utawala wa sasa wa Mama Samia, tayari ndani ya CCM kuna maumivu makali ikiashiria kisu kimetua kwenye mfupa. Kwa sasa ndani ya CCM hakukaliki, na mpango uliopendekezwa kufanyika kwa haraka ni kumvua uanachama Humphrey Pole Pole.

Soma Pia: Humprey Polepole ajiuzulu Ubalozi, Asema hawezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba na chama

Mchakato uliopangwa ni kumuita haraka kuja kujieleza (jambo ambalo huenda Polepole atalikaidi, maana anaweza asirejee sasa hapa Tanzania na pia halitabadilisha chochote) na baada ya hapo itatangazwa kuvuliwa uanachama.
Polepole anachapa viboko vya juu ya kiuno tu, ukishika anafuta ananza upya.
 
Back
Top Bottom